Ads Top

HATIMAE CHANZO CHAJULIKANA NI KUHUSU VURUGU ZA MBAGALA KUFUATIA KUKOJOREWA KWA KITABU CHA QURAN

MTOTO anayedaiwa kudhihaki kwa kukikojolea kitabu kitakatifu cha Quran (jina linahifadhiwa) ameponzwa na ujumbe wa simu uliosambazwa jijini Dar na kulifanya tukio hilo kuwa kubwa zaidi. Watu waliounasa ujumbe huo wamesema kuwa mara baada ya kutokea kwa tukio hilo, baadhi ya Waislamu wa Mbagala jijini Dar, walianza kuwataarifu wenzao wanaoishi katika vitongoji mbalimbali kwa kutumia SMS.
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wakijihami kwa mawe wakati wa vurugu hizo

Baada ya kupata taarifa hizo, Waislamu walianza kulizungumzia tukio hilo misikitini Ijumaa iliyopita na kukusanyana kwenda Mbagala kwa ajili ya kumsaka mtoto huyo. Habari zaidi zinasema kuwa mtoto aliyekidhihaki kitabu hicho aliponzwa na tambo zake kuwa hakuna kitakachomtokea baada ya kufanya kitendo hicho.

Gari lenye namba za usajili T 665 ATQ baada ya kuchomwa moto na waandamanaji hao.
 

Baada ya kukutana kukatokea mabishano kati yao huku yule wa Kikristo akisema kitabu kile kilikuwa ni majini na yule wa Kiislamu akikitetea. “Mtoto wa Kiislamu alimkanya mwenzake kwamba asikichezee kitabu kile kwani anaweza kugeuka nyoka, ndipo mwenzake alipokichukua na kukimwagia mkojo, kisha kukitemea mate,” alisema jirani huyo.
Baadhi ya waandamanaji wakiwa wamewekwa chini ya ulinzi.

mali kadhaa yakiwemo makanisa na magari yalikuwa yamevunjwa na imeripotiwa kuwa jenereta moja kubwa la umeme la Kanisa la Sabato limeibwa na baadhi ya watu hao waliokasirishwa na kitendo kilichofanywa na mtoto huyo.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.