Ads Top

VIWANJA VITAKAVYO TUMIKA KATIKA LIGI KUU TANZANIA BARA MSIMU WA 2013/2014

 http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2012/09/uwanja-mpya-utakao-tumika1.jpg
Ligi Kuu msimu wa 2013/14 itaanza Agosti 24 na itashirikisha timu 14. Timu hizo ni mabingwa watetezi  Yanga, Simba, Azam FC, Ashanti United, Tanzania Prisons, Rhino Rangers na Kagera Sugar, Mtibwa Sugar, JKT Ruvu, Ruvu Shooting, Mgambo Shooting, Mbeya City, JKT Oljoro na Coastal Union.

Vifuatavyo ni viwanja 10 vitakavyotumika kwa ajili ya mechi mbalimbali za Ligi Kuu msimu huu:

1.Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Sifa za uwanja huu:

Uwanja huu ulianza kutumika mwaka 2007. Uwanja huu una vipimo vya mita 105 kwa meta 68 na una milango 35 kwa ajili ya watazamaji kuingia na kutoka uwanjani. Una uwezo wa kuchukua zaidi ya mashabiki 50,000.

Klabu zitakazoutumia uwanja huu kama uwanja wake wa nyumbani ni Simba na Yanga.

2.Uwanja wa Ali Hassani Mwinyi, Tabora.

Sifa za Uwanja huu:

Ulijengwa mwaka 1987 chini ya usimamizi wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Lawrence Gama.

Una uwezo wa kuchukua watazamaji 30,000 na una milango minane kwa ajili ya kuingia na kutoka uwanjani.
Uwanja huu unamilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM)
Klabu itakayoutumia uwanja huu kama uwanja wake wa nyumbani ni Rhino Rangers.

3.Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Uwanja huu ulijengwa mwaka 1957 na unamilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Uwanja wa Sheikh Amri Abeid una uwezo wa kuingiza watazamaji 25,000 kwa wakati mmoja.

Klabu ya JKT Oljoro inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT),    itautumia Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kama uwanja wake wa nyumbani.

4.Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Sifa za uwanja huu:
http://michuzijr2.files.wordpress.com/2009/05/dsc04321.jpg

Unapatikana katikati ya jiji la Mbeya na ulijengwa mwaka 1977. Uwanja wa Sokoine una uwezo wa kuchukua watazamaji 20,000 na unamilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Klabu za Tanzania Prisons na Mbeya City zitautumia uwanja huu kama uwanja wao wa nyumbani.

5. Azam Complex- Chamazi, Dar es Salaam.

Sifa uwanja huu:
Ujenzi wake ulianza mwaka 2010 chini ya mkandarasi Kampuni ya Salehe Msahala Contractors Limited 
Uwanja wa Azam Complex una vipimo vya mita 110 kwa mita 71, pia una milango minne na una uwezo wa kuingiza watazamaji 7, 000 kwa mara moja.

Klabu zitakazoutumia uwanja huu kama uwanja wake wa nyumbani ni   Ashanti United, Azam FC na  Ruvu Shooting. Mmiliki wa uwanja huu ni klabu ya Azam FC.

6. Uwanja wa Mabatini, Pwani.

Uwanja wa Mabatini unapatikana katika mji wa Mlandizi uliopo Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani. Ni uwanja unaomilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kambi ya Ruvu.

Klabu ya Ruvu Shooting itautumia uwanja huu kwa ajili ya mechi zake za nyumbani isipokuwa zile itakazocheza dhidi ya Simba na Yanga.

7.Uwanja wa Kaitaba-Bukoba, Kagera.

Sifa za uwanja huu:

Una vipimo vya ukubwa wa mita 110 kwa mita 50. Ulijengwa mwaka 1957 na unamilikiwa na Manispaa ya mji wa Bukoba. Uwanja wa Kaitaba

Una milango minne na una uwezo wa kubeba watazamaji 5, 000 kwa wakati mmoja.

Klabu ya Kagera Sugar ndiyo itakayoutumia uwanja huu kama uwanja wake wa nyumbani.

8.Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Sifa za uwanja huu: 
Ulijengwa mwaka 1975 na Kampuni ya Amboni Plantation. Uwanja wa Mkwakwani una vipimo vya ukubwa wa mita 105 kwa mita 68, pia una milango saba na uwezo wa kuchukua watazamaji 20,000. Mmiliki wa uwanja huu ni Chama cha Mapinduzi (CCM).
Klabu za Coastal Union na Mgambo Shooting zitautumia uwanja huu kama uwanja wao wa nyumbani.
9.Uwanja wa Manungu, Morogoro.
Sifa za uwanja huu:
Ulijengwa mwaka 1988 ukiwa na vipimo vya ukubwa wa mita 100 kwa  75. Uwanja wa Manungu una milango minne na uwezo wa kubeba watazamaji 8,000. Mmiliki wa uwanja huu ni Kampuni ya Mtibwa Sugar. Klabu ya Mtibwa itautumia uwanja huu kama uwanja wa nyumbani, lakini itakapokabiriana na Simba au Yanga itatumia uwanja wa Jamhuri Morogoro. Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ulijengwa mwaka 1978 na unamilikiwa na  CCM na una uwezo wa kuchukua watazamaji 20,000.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.