Ads Top

TAZAMA PICHA ZA TUKIO LA KIGAIDI LILILO TOKEA SIKU MBILI ZILIZO PITA NAIROBI NCHINI KENYA KWENYE JENGO LA GHOROFA NNE LENYE MADUKA WESTGATE



 Askari kanzu na mtutu wake mkononi akimuokoa mtoto na mwanamke kutoka eneo la tukio katika picha hii nadra ambayo inaeleza kila kitu.


 Askari Kanzu akimuokoa mtoto


 Askari kanzu wakitafuta magaidi chumbha hadi chumba






 Askari kanzu na mtutu wake mkononi akishikilia tumbo baada ya kujeruhiwa





Watu wakitembea kwa magoti na mikono mbele ya mwenzao mmoja ambaye inaonesha ameshakufa












Hali ilivyokuwa ndani ya jengo lililovamiwa na magaidi.

KUNDI la Alshabaab, limethibitisha kuhusika na shambulio la kigaidi lililotokea jana kwenye jengo la ghorofa nne lenye maduka la Westgate jijini Nairobi, nchini Kenya. Alshabaab kupitia kwa afisa wake mmoja, imethibisha hilo na kueleza kuwa shambulio lilikuwa na kulipiza kisasi baada ya Kenya kujihusisha na vita ya Somalia.

Walioshuhudia tukio hilo wanadai watu waliovalia magwanda yalioonekana kama ya kijeshi huku wengine wakiwa wamefunika nyuso zao walivamia jengo hilo huku wakifyatua risasi. Maduka hayo ya Westgate hutendelewa sana na matajiri pamoja na wageni kutoka nchi mbalimbali.
Kupitia mtandao wao wa Twitter, Al Shabaab imesema kuwa Kenya ilijidai kutosikia onyo hizo, na kuendelea kuwaua waislamu wasio na hatia nchini Somalia, na shambulio la Westgate ni tone tu katika bahari ya mfano wa yanayowakumba wasomali nchini Somalia. Taarifa kutoka Ikulu ya nchini Kenya, zinadai kuwa mmoja wa watuhumiwa aliyekamatwa katika tukio hilo  alifariki kutokana na majeraha yake. 
Magaidi wapatao kumi walivamia jengo la kifahari la Westgate J/mosi mchana la kuwapiga risasi kiholela Wakenya waliokuwa wanaendelea na shughuli zao za kawaida.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.