Ads Top

WAGANGA WAWILI WA JADI AKIWEMO MFANYABIASHARA MMOJA WALIONASWA JIJINI MWANZA WAKIWA NA KIUNGO CHA MKONO WA KULIA WA BINADAMU

 Picha juu mmoha kati ya watuhumiwa akionyesha  Kiganja hicho kilihifadhiwa ndani ya chungu na picha ya chini kiganja chenyewe
  Watuhumiwa wakiwa na kiganja hicho cha binadamu.
  Ni unyama gani huu?
Ulinzi uliimarishwa katika eneo hili kuhakikisha taratibu zote zinafuatwa.
Wananchi wakiwa katika hali ya kutafakari juu ya tukio hilo la kusisimua.Picha Zote na Habari na Mdau Gsengo
WAGANGA wawili wa jadi akiwemo mfanyabiashara mmoja, wamenaswa jijini Mwanza, wakiwa na kiungo cha mkono wa kulia unaoamainika kuwa wa binaadamu.
Watuhumiwa hao waalikamatwa jana mchana majira ya saa 9 katika eneo la Ziwani na Uwanja wa Ndege wa Mwanza, kufatia taarifa za raia wema na kisha jeshi la polisi kuweka mtego kwa muda wa wiki nzima na hatimaye kufanikiwa.
  Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Joseph Konyo, akitihibitisha tukio hilo, alisema kwamba mkono huo uliokuwa umewekwaa kwenye begi na ambamo ulikuwa umefungwa kwenye kwenye mfuko mweusi wa plasitiki na kuviringishwa kwenye kalatasi nyeupe ya nailoni, umekutwa ukiwa mbichi.

Konyo ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoani Mwanza (RCO), alieleza kuwa watuhumiwa hao (majina yanahifadhiwa) wenye umri wa miaka 36 na 43 (ni waganga wa jadi wawili) na mfanyabiashara ana miaka 48.
Alisema kuwa, kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa katika jeshi hilo na kuweka mtego huo kisha makubaliano ya kununua viungo hivyo kutoka kwa watuhumiwa hao (wauzaji), walimhakikishia wanunuzi (polisi) kuwa wanaweza kupata kichwa, mikono, miguu na sehemu za siri za binaadamu endapo wangezihitaji.
  “Taarifa hizi ni za awali maana tukio lenyewe bado ni bichi kabisa na limetokea muda mfupi uliopita hivyo taarifa zaidi tutazitoa baada ya kukukamilisha upelelezi wetu ikiwa pamoja na kuwakamata watuhumiwa na kubaini binaadamu aliyeuawa na kukatwa baadhi ya viungo ambavyo waganga hao walidai wanaweza kuvipata.” Alieleza.
 Kamanda Konyo pamoja na kuwapongeza wananchi waliotoa taarifa zilizofanikisha mtego huo, alisema jeshi lake liko katika harakati za kupambana na mauaji na uhalifu wa kila aambapo tayari kikosi kazi kiko katika wilaya ya Magu kikishirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha kinawatia mbaroni watu wanaojihusisha na

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.