Ads Top

MWILI WA MAREHEMU JAJI MSTAAFU LEWIS MAKAME WAAGWA VIWANJA VYA KARIMJEE DAR ES SALAAM, LEO

 eneza lenye mwili wa Marehemu aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Lewis Makame likiwa  mbele ya viongozi wa Serikali, ndugu, jamaa na marafiki kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda akisaini kitabu cha maombolezo wakati wa kuuaga mwili wa Marehemu aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Lewis Makame leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimian na Mawaziri Wakuu, Wastaafu, Frederick Sumaye na Jaji Joseph Warioba (wapili kulia)  kabla ya kuzungumza kwa niaba ya serikali na  kutoa heshima za mwisho kwa Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,  marehemu Jaji Lewis Makame kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam August 22, 2014. Kulia nI jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed  Chande Othman.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na jaji Mkuu Mohamed Chande  Othman  (kulia) na Mawaziri Wakuu Wastaafu, Joseph Warioba (wapili kulia) na Frederick  Sumaye kabla ya kutoa salamu za Serikali na  heshima za mwisho kwa Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, marehemu Jaji Lewis Makame kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam August 22, 2014.
  Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pinda akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Lewis Makame leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho kwa Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Marehemu Jaji Lewis  Makame baada ya kuzungumza kwa niaba ya serikali kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam August 22, 2014. 

 Mmoja wa wafiwa akilia kwa uchungu wakati akiuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Lewis Makame katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpa pole Jaji Leila Makame Mgonya mmoja wa wana familia, wa  Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Marehemu Jaji Lewis Makame  baada ya kuzungumza kwa niaba ya serikali na kutoa heshima za mwisho kwa marehemu huyo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam August 22, 2014.
 Viongozi mbalimbali wa Serikali wakilisikiza wasifu wa marehemu aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Lewis Makame leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. 
 Ndugu, jamaa na marafiki wakiwa na nyuso za uzuni wakati wa  kuuaga mwili wa Marehemu aliyekuwa Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Lewis Makame leo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.Picha na Anna Nkinda- Maelezo na Ofisi ya Waziri Mkuu

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.