Pistorius amekana kumuua mpenzi wake kwa maksudi
Jaji anayetoa uamuzi katika kesi ya mauaji inayomkabili Oscar Pistorius,
amesema upande wa mashitaka umekosa kuthibitishia kikamilifu shitaka
kuu la kwanza dhidi ya Pistorius kuwa alikusudia kumuua mpenzi wake
Reeva Steenkamp
Hata hivyo jaji huyo Thokozile Masipa amepinga ushahidi wa upande wa
utetezi kwamba mwanariadha huyo hakunuia kutenda uhalifu alipomuua
mpenzi wake Reeva.
Pistorius alikiri kumuua mpenzi wake Reeva
Steenkamp nyumbani kwake mwaka jana lakini amekana kumuua kwa maksudi ,
akisema alidhani kuwa mwizi alikuwa amevamia nyumba yake.
Upande wa mshitaka unasisitiza kuwa Pistorius alimuua Reeva kwa maksudi,baada ya wapenzi hao wawili kutofautiana.
Mandishi wa BBC anasema kuwa jaji Thokozile Masipa heunda akachukua hadi Ijumaa kumaliza uamuzi wake.
Pia atakuwa anaangalia kwa makini ukweli wa mashahidi waliotoa ushaidi wao katika kesi hiyo akiwemo Pistorius mwenyewe.
Pistorius huenda akafungwa jela miaka 25 ikiwa atapatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake.
Oscar Pestorius amekana mashitaka ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp katika siku ya wapendanao ya Valentine mwaka jana.
Mwendesha
mashitaka anasisitiza kuwa Pestorius alimpiga risasi aliyekuwa mpenziwe
Reeva baaya ya ugomvi baina yao lakini amejitetea akisema alimpiga
risasi kimakosa akidhani mwizi amevamia nyumba yake.
No comments: