Ads Top

TAARIFA: WANAJESHI WA 3 WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA NA RAIA 1 WAFA KATIKA AJALI YA KIFARU MTWARA


 

Kifaru kilichokuwa kikisafiri kutoka Mtwara kwenda Lindi kikiwa kimeacha njia na kugonga nyumba usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Mnolela Lindi vijijini, kusababisha vifo vya watu watatu katika ajali hiyo.Na Mpiga Picha Wetu


 WATU wawili wamekufa papo hapo na saba wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea katika Kijiji cha Mnolela Manispaa ya Lindi ikihusisha gari la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
 

Ajali hiyo ilitokea katika Barabara ya Mingoyo, baada ya kifaru cha jeshi  kugonga nyumba na kusababisha kifo cha Somoe Kamteule aliyekuwapo ndani. Pia askari mwenye namba Mt 10728 Pascal Komba alikufa katika ajali hiyo.



Gari hilo ni la Kikosi Namba 83, ambalo liliacha njia na kugonga nyumba mbili  na raia na kusababisha vifo hivyo. Dereva wa gari hilo alikuwa askari Shandili Nandonde. 




Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Lindi, Renata Mzinga alisema ajali hiyo  ilitokea jana saa 11.30 alfajiri. Gari hilo lilikuwa likitoka mkoani Mtwara  kwenda Nachingwea. 



Aidha Kamanda huyo alitaja waliojeruhiwa ambao ni askari wa JWTZ kuwa ni  Simon Edward, Feruzi Hadji, Omary Makao, Mbaruku Duchi, Simon Masele,  Shadhili Nnandonde na mwingine aliyefahamika kwa jina moja Ndekenya.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.