MKUTANO WA KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA MAFINGA
Katibu
Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapungia mkono wananchi
wa Mafinga wakati akiwasili kwenye uwanja wa Mashujaa .
Katibu
Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana na Bi.Mwigavillo Ngole
ambaye amesafiri mwendo mrefu kuja kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM
Wazee
wa Kimila wakiwa uwanjani kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana ambapo walimpa Uchifu na kumtambua kwa jina la
Galiendela Matuga .
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mufindi Johanes Kaguo akifungua
mkutano na kuhutubia wananchi wa Mafinga ambapo alielezea kero mbali
mbali zinazowakabili wananchi wa Mafinga kwa Katibu Mkuu wa CCM.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mafinga na
kuwaambia kuwa Mafinga hamna upinzani ila kuna manung'ung'uniko ya
wananchi ambao hawapati taarifa za kina kuhusu masula yanayohusu ugawaji
na upatikanaji wa vibali vya mbao.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu akihutubia wananchi wa
Mafinga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mashujaa
Umati wa watu waliofurika kwenye uwanja wa Mashujaa Mafinga kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
Katibu
Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa
Mafinga wilaya ya Mufindi ambapo aliwaambia viongozi kuwa mstari wa
mbele kusimamia haki na wajiepushe kuingia kwenye mambo ambayo
yatasababisha kushindwa kuwatetea wananchi wao.
Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mahamoud Mgimwa akihutubia wananchi wa
Mafinga kwenye uwanja wa Mashujaa ambapo alisema waombaji wa vibali ni
wengi kuliko uwezo wa serikali hivyo umeanzishwa utaratibu wa kila
aliyepata kibali asiombe mara ya pili.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akipitia taarifa mbali mbali zinazohusu wilaya ya Mufindi
Katibu
Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi hao
ambapo aliwatajia vijiji vitakavyopata umeme ,maji na umuhimu wa
kujiandikisha kwenye mfuko wa afya ya jamii.
Wananchi wakifuatilia mkutano
Kila mtu alikaa alipoweza kumuona Katibu Mkuu wa CCM Ndugu abdulrahman Kinana.
Watu walikuwa mpaka kwenye ukuta wa uwanja wa Mashujaa kumsikiliza Kinana
Katibu
Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya
uanachama wa CCM Bi.Leah Msese ,zaidi ya watu 400 wamejiunga na CCM
Mafinga.
No comments: