Mkuu wa kampuni ya Apple Tim Cook ametangaza jinsia yake akisema kuwa ''anajivunia kuwa shoga''
Bwana Cook alitoa tamko hilo ili kujaribu kuwasaidia watu
wanaong'ang'ana kutangaza jinsia zao katika ripoti iliochapishwa katika
gazeti la biashara la kila wiki la Bloomberg.
Amekuwa wazi kuhusu jinsia yake,lakini pia amejaribu kuweka maisha yake katika faragha hadi sasa alisema
nembo ya campuni ya apple
Wiki hii Bwana Cook alitoa changamoto kwa jimbo lake la Alabama
kuhakikisha kuwa haki za mashoga na wale wanaobadili jinsia
zinaheshimiwa.
''Mimi sijitambui kama mwanaharakati,lakini nimegundua nilivyofaidika na mikakati iliowekwa na wengine'',alisema bwana Cook.
''Kwa
hivyo iwapo watu wakisikia kwamba mimi ni shoga kutawasaidia baadhi yao, ama kumpa faraja yule anayejisikia mpweke ama kuwashinikiza wengine
kupigania haki zao, basi afadhali kutangaza maisha yangu ya
faragha''aliongezea.
Bwana Cook amesema amekuwa wazi kuhusu jinsia
yake na watu wengi wakiwemo wafanyikazi wenzake katika kampuni ya
Apple, lakini hilo halikuwa chaguo rahisi kutangaza hadharani kuhusu
jinsia yake.
No comments: