Ni miezi sita sasa baada ya wanamgambo wa kiislam wa kundi la Boko Haram kuwateka wanafunzi wasichana Zaidi ya 200 kaskazini mashariki mwa Nigeria, wasichana watatu ambao wametoroka wamezungumza katika mahojiano maalum na idhaa ya Kiswahili ya BBC
Tukio hili linakuja wakati serikali ya Nigeria ikiwa katika
makubaliano ya kusimamisha mapigano dhidi ya Boko Haram hatua itakayo
saidia kuwaachilia huru wasichana waliotekwa na kundi hilo.
''
nilikuwa nataka kurukia nje wakati msichana mwenzangu aliponikamata kwa
nyuma na kusema watakupiga risasi kama utafanya hivyo. Nikasema, nini
utofauti wataniua mimi hapa na kuacha maiti yangu
ikusachukuliwa
nilikuwa nalia na kuomba mpaka tulipoifiki kambini"
Anasimulia msichana
mmoja alitoroka mikononi mwa Boko Haram
Akizungumza katika
mahojiano maalum na idhaa ya Kiswahili ya BBC, Msichana huyu anakumbuka
jinsi alivyokuwa nyuma ya Lori wakati wapiganaji wa Boko Haramu
walipomteka yeye na wasichana wengine.
Zaidi ya wasichana 200 kati
miongoni mwa waliotekwa lakini wale waliokimbia walibahatika
kutoingia katika hofu kubwa kwenye mikono ya watekaji.
Shirika la
kimataifa la kutetea haki za binaadam la Human Rights Watch limesema
wanawake wanaoshikiliwa na kundi la Boko Haramu wamekuwa wakinyanyaswa,
kubakwa na hata kulazimishwa kuolewa.
Katika ripoti mpya ya
shirika hilo inasema Wanamgambo hao wa Kiislam wamewateka wanawake
Zaidi ya 500 na wasichana tangu mwaka 2009.
Serikali ya Nigeria
hivi karibuni imetangaza makubaliano ya kusimamisha mapigano dhidi ya
Boko Haram ambayo hatua itakayawafanya wanamgambo hao kuwaachilia huru
wasichana hao waliotekwa huko Chibok.
Lakini Boko Haram wenyewe
hawajawahi kuthibitisha makubaliano yoyote ya kusitisha mapigano na
hakuna dalili zozote za kuachiwa kwa wasichana haohivi karibuni.
Lakini kwa wale waliobahatika kutoroka, matatizo ya kisaikolojia bado yanawasumbua.
Habari na BBCswahili
No comments: