Zaidi ya watu 200 raia wa Sudan Kusini wamezama katika ajali ya boti kwenye mto Nile wakikimbia vita vinavyoendelea katika mji wa Malakal
Taarifa hii ni kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Sudan Kusini.
Boti hiyo iliyozama, ilikuwa imewabeba watu
wengi kupindukia. Watu hao walikuwa wanatoroka vita vinavyotokota katika
mji wa Malakal.
Mapigano yalizuka Sudan Kusini mwezi Disemba
mwaka jana baada ya Rais Salva Kiir kumtuhumu aliyekuwa makamu wake wa
Rais Riek Machar, kwa kuwa na njama ya kumpindua.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu 1,000 wameuawa tangu ghasia kuanza nchini humo
HABARI NA BBCswahili.com
HABARI NA BBCswahili.com
No comments: