Ads Top

WANANCHI TINDE WATISHIA KUFANYA MAANDAMANO MAKUBWA KUWACHONGEA IGP NA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI

I
IGP MWEMA
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MH NCHIMBI

Na Antony Sollo Shinyanga.
Wananchi wa Kata ya Tinde tarafa ya Itwangi wametishia kufanya maandamano makubwa ambayo hayajawahi kutokea mkoani Shinyanga ili kuwachongea kwa Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania viongozi wa Wizara ya Mambo ya ndani pamoja na Inspekta wa Jeshi la Polisi Said Mwema kwa kuwatuhumu kuwa wamekuwa na mpango wa kuwahujumu wananchi hao kwa kushindwa kuimarisha ulinzi na usalama katika eneo hilo muhimu kwa kuwanyima gari la doria askari wa kituo cha Polisi Tinde Wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Wakiongea na mwandishi wa habari wa Anika Ukweli baadhi ya wananchi akiwamo Mzee mmoja ambaye hakutaka kuandikwa gazetini amehoji “Hivi IGP pamoja na Mh Waziri wa Mambo ya ndani hawaoni aibu kuwanyima askari wa kituo cha Polisi Tinde gari kwa ajiri ya kufanya doria katika maeneo mbalimbali?
Ni kwa nini Serikali hii ina ubaguzi kiasi hicho? nashindwa pia kuelewa kuwa kuna mpango gani mnaoufanya katika kuwajengea uwezo vijana hawa katika kituo hiki muhimu hapa Tinde.
Mimi nasema hivi kama Bunge hili litakwisha bila vijana hawa kupatiwa gari tutaandamana kumuona Mh. waziri mkuu ili kuwashtaki kwa kosa la kufanya njama kuwahujumu wananchi wa Tinde na vijiji mbalimbali vinavyozunguka eneo hilo kwa kuwanyima askari hawa gari kwa ajili ya doria ili kuwahakikishia usalama wananchi hawa” alihoji mwananchi huyo.
Inawezekana kuna mkakati uliondaliwa na viongozi hawa ili kuwapa mwanya majambazi waweze kufanikisha mipango yao, na kama sivyo,ina maana viongozi wa jeshi la polisi hawaijui jiografia ya Shinyanga na kama wanaijua basi ni makusudi,kwa kweli huwezi kuamini jinsi vijana hawa wanavyofanya kazi katika mazingira magumu huku wenzao wakila bata kwa kusindikizwa na magari mazuri yanayoonekana kusimama njiani kusubiri kutoza faini kwa madereva wazembe badala ya kufanya ulinzi wa raia na mali zao.
Tinde kuna mnada,kuna mazao mbalimbali,kuna watu wanaojua vizuri kufanya kazi zao kufanikisha maisha pamoja na maendeleo katika nyanja mbalimbali,lakini inashangaza kuona wananchi wa Tinde hawana msaada wowote toka ngazi za juu wanaopewa ili kuonyesha ushirikiano kati yao na Serikali yao.
Mwandishi wa Habari hizi alipotaka kujua kwa nini kituo hicho cha polisi Tinde hakina gari la doria alifika kituoni hapo ambapo alikosa ushirikiano toka kwa askari wa kituo hicho kwa kusema wao si wasemaji wa jeshi hilo kwa hiyo alielekezwa kuwa awasiliane na kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ambapo kamanda huyo hakupatikana mara moja kwa njia ya simu yake ya mkononi namba 0764 193 065 na kutuma ujumbe unaouliza kwa nini kituo hicho hakina gari ulikuja ujumbe uliosomeka kuwa Tuna gari kila siku, jambo ambalo linaendelea kutia mashaka kwamba je gari linalosemwa ni mali ya kituo cha Polisi Tinde au ni lile linalokuja kwa ajili ya kufanya doria na kurudi Mkoani! Naye Mbunge wa viti maalumu Mh. Azah Hillary alipotafutwa pia kulizungumzia suala hili simu yake ilikuwa ikitumika wakati wote ambapo simu ya Mh. Mbunge wa Jimbo la Solwa ilikuwa ikiita bila majibu juhudi za kutafuta nini ni chanzo cha eneo hilo muhimu kukosa gari la doria kwa askari wa kituo cha Tinde alimtafuta pia Diwani wa kata hiyo Mh. Jafary lakini naye simu yake ya mkononi namba 0783 821773 ilikuwa imezimwa.
Mwandishi wa habari aliyefika katika eneo hilo alijionea mambo mbalimbali yanayoendeshwa ikiwamo wananchi kutopata ushirikiano wa kutosha toka kwa viongozi wao ikiwemo kukosa ushirikishwaji katika mipango mbalimbali ya maendeleo hivyo wanamuomba Mh. waziri wa TAMISEMI ,Waziri wa Afya,kufika hapo pia ili wajionee wananchi wanavyonyanyaswa na wauguzi wa kituo cha Afya kwa kuandikiwa vyeti nakuelekezwa kwenda kunua dawa kwenye maduka binafsi badala ya kupata matibabu toka kituoni hapo lakini pia uchafu uliokithili katika wodi za wagonjwa,na pia kuona wakina mama wanavyojifungua katika mazingira hatarishi,gizani huku eneo hilo likiwa limesheheni utajiri wanahoji ni kwa nini wakapate dawa katika maduka ya watu binafsi dawa zinazoletwa kituoni hapo ni haki yao au zinakuja kwa hisani! Kama ni haki yao ya msingi kwa nini wapate shida wakati na wao wanastahili kupata huduma zinazotolewa na Serikali yao kwa raia wa Tanzania.
Mwandishi wa habari hizi ni Mwanaharakati na mtetezi wa haki za binadamu anapatikana kwa namba zifuatazo
0787 565 533,0713 565 533,0763 209 400
Email antonyjilala@yahoo.com

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.