Ads Top

MICHEZO & BURUDANI

 Hata hivyo shirikisho hilo la FIFA limesema kuwa kwa sasa haliwezi kusema lolote kuhusu suala hilo, hadi uchunguzi utakapo kamilika.
FAM limedai kuwa Keshi alitoa matamshi ya ubaguzi dhidi ya kocha wake Tom Sainfiet raia wa Ubelgiji.
Katibu mkuu wa FAM, Suzgo Nyirenda ameiambia BBC, kuwa matamshi hayo ya ubaguzi hayafai kuwepo katika michezo katika dunia ya sasa.
''Tunahisi na shambulio dhidi ya kocha wetu na tutamtetea kwa hali na mali, bila kuzingatia uraia wake na rangi ya ngozi yake'' Alisema Nyirenda.
''Tumetuma ushahidi wa yale Keshi aliyoyasema na tunatarajia kuwa FIFA itachukua hatua kali dhidi ya kocha huyo wa Nigeria Stephen Keshi'' aliongeza Nyirenda.
Kesi hiyo inahusiana na matamshi ambayo Keshi aliyatoa kufuatua wito wa Malawi wa kuhamisha mechi yao ya kufuzu kwa kombe la dunia mwaka wa 2014, kutoka mji wa Calabar kutokana na sababu za kiusalama.
Katika mahojiano na runinga moja ya Uingereza, Keshi alisema ''Nafikiria kuwa kocha huyo wa Malawi ni wazimu''.
''Ikiwa anataka kuongea na FIFA, basi ni lazima arejea kwao nchini Ubelgiji. Yeye sio mtu wa Afrika, ni mzungu mweupe, ni lazima arudi kwao Ubelgiji'' Alisema Keshi katika mahojiano hayo.
Maafisa wakuu wa shirikisho la mchezo wa soka nchini Nigeria pamoja na kocha huyo hawajasema lolote kuhusiana na madai hayo ya kocha wa Malawi Saintfiet na FAM.
Mechi hiyo kati ya Malawi na Nigeria mjini Calabar itaamua nani atafuzu kwa raundi ya mwisho ya mechi ya kufuzu kwa fainali hiyo barani Afrika.
Mabingwa hao wa Afrika wanahitaji kutoka sare ya aina yoyote ili kufuzu ili hali Malawi inahitaji ushindi ili isonge mbele.

Klabu za Chelsea na Manchester United zimeminyana uwanjani Old Trafford. Pande zote mbili zimekosa kufunga bao, na hivyo kutoka sare ya bila kwa bila


Jinsi mambo yalivyokuwa uwanjani Old Trafford

Matokeo hayo yanamaanisha kwamba mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza, wote wamepoteza pointi katika siku kumi na sita za kwanza wa msimu huu, na zinaifuata Manchester City iliyopoteza pointi pia kufuatia mechi dhidi ya Cardiff.
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho aliiambia BBC Sport " Hakuna Upande uliostahili kushinda na kushindwa vile vile, unataka kushinda lakini pande zote zilikua na ulinzi mkali. Na kwa mashabiki najua angalau bao moja lingewafurahisha, iwapo ungekuwa mchuano mzuri''.

Mkufunzi wa Manchester United David Moyes
Naye meneja wa Manchester United, David Moyes alisema, alivunjika moyo kwa sababu hawakuzoa pointi yoyote, lakini ndivyo ilivyo na hawana budi kujifunza kutokana na hali hiyo.
Chelsea kwa sasa inaongoza ligi kuu kwa pointi saba, ikifuatwa kwa karibu sana na Liverpool na Tottenham, zote zikiwa na pointi sita. Machester United inashikilia nafasi ya nne ikiwa na pointi nne.
Klabu ya Barcelona imeiambia Manchester United kuwa haina nia ya kumuuza nyota wake Cesc Fabregas

Cess Fabregas

Klabu ya Barcelona imeiambia Manchester United kuwa haina nia ya kumuuza nyota wake Cesc Fabregas.
Manchester United, imethibitisha kuwa iliwasilisha tena ombi la kumsajili mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni thelathini, lakini ripoti zinasema kuwa ombi hilo limekataliwa.
Rais wa Barcelona Sandro Rossel, amekariri kuwa klabu hiyo haina nia ya kumuuza mchzaji huyo kwa klabu yoyote.
Kocha wa Manchester United, David Moyes amenukuliwa akisema huenda wasifanikiwe kumsajili mchezaji huyo.
Hata hivyo Moyes amekiri kuwa naibu mwenyekiti wa klabu hiyo Ed Woodward, angali anafanya kila juhudi ili kuhakikisha kuwa wamemsajili mchezaji huyo.
Mara ya kwanza United iliwasilisha ombi la kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka ishirini na sita kwa kitita cha pauni milioni ishirini na tano, lakini pendekezo hilo lilikataliwa na Barcelona.



David Moyes Kocha wa Manchester United

Siku mbili tu baada ya United kuwasilisha ombi hilo, Woodward alikatiza ziara yake nchini Australia na kurejea nyumbani kuongoza mikakati ya kumsajili Fabregas, kabla ya muda wa mwisho wa usajili kukamilika.
Barcelona haijatoa taarifa yoyote, lakini kuna habari kuwa huenda matatizo yanayokumba klabu hiyo kwa sasa yamechangia pakubwa uamuzi huo kukataliwa.
Kocha wa Barcelona Tito Vilanova alijiuzulu kutokana na matatizo ya kiafya.
Haijulikani ikiwa uamuzi wa Chelsea wa kutaka kumsajili mshambulizi wa Manchester United Wayne Rooney umechangia klabu hiyo kutaka kumsajili Fabregas.

 

Ngassa atua Jangwani, asaini mkataba wa miaka miwili


Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrance Mwalusako (kushoto) akimkabidhi Mrisho Ngassa jezi wakati akimtambulisha rasmi jana, baada ya kusaini Yanga mkataba wa miaka miwili.Picha na Michael Matemanga  

Dar es Salaam.Wakati winga Mrisho Ngassa akisaini mkataba wa miaka miwili wa kuicheza Yanga, kiungo Haruna Niyonzima ametoa saa 24, kwa uongozi wa mabingwa hao kumalizana naye kabla ya kutimkia timu nyingine.

Uongozi wa Yanga jana umemtambulisha rasmi Ngassa kumrejea kundini baada ya kumaliza mkataba wake na Azam ambao walimpeleka kwa mkopo Simba kwa muda wa mwaka mmoja.

Habari ambazo Mwananchi ilizipata zimesema kuwa tayari uongozi wa Yanga umeshampa kitita cha Dola 10,000 kati ya Dola 30,000, mshambuliaji huyo ambaye aliondoka kwa mbwembwe kwenda Azam kwa dau la Sh50,000 milioni.

Chanzo hicho kimedai kuwa Ngassa bado anaidai klabu hiyo ya mtaa wa Jangwani kitita cha Dola 20,000 ambacho aliahidiwa kukabidhiwa mara atakapotua rasmi ndani ya klabu hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Ngassa ambaye alikabidhiwa jezi iliyokuwa na jina lake na Katibu mkuu wa klabu hiyo Lwaurance Mwalusako alisema, “Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kurudi tena Yanga, klabu ambayo nina mapenzi nayo

tangu utoto, nawashukuru viongozi wa Yanga waliopigana hasa rais Kifukwe (Francis) kuhakikisha wananirudisha kundini.

“Nilipokuwa Azam, Simba nilicheza kwa uaminifu mkubwa, lakini viongozi hawakuwa na imani na mimi kwa vile nina mapenzi na Yanga, ni kweli naipenda Yanga, lakini hata siku moja sikucheza kiuunazi, nilicheza kwa uaminifu kwa vile mpira ni ajira yangu, mapenzi yanafuata lakini viongozi hawakuliona hilo.

Kuhusu kusaini mkataba na Simba ambao alipewa dola 25,000 pamoja na gari aina ya Verosa Ngasa alisema “Sina mkataba na Simba na sijawahi kusaini mkataba na Simba, mkataba wangu ni Azam na Azam waliomnipeleka Simba kwa mkopo.

Akifafanua jambo hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Abdallah Binkreb alisema “Sh 25 milioni zilizotolewa na Simba ilikuwa ni ada ya kumtoa Azam kwenda Simba na gari alilopewa ilikuwa ni ushawishi tu ili akubali kucheza Simba klabu ambayo hakuwa na mapenzi nayo.”Naye

Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hanspop
alisema,“Mkataba wetu na Ngassa upo wazi tena unasema wazi utaanza pale ambapo mkataba wake na Azam utakapomalizika, hatujaingia mkataba juu ya mkataba kama Yanga wanavyodhani.

“Yanga wamezoea fujo wanafanya mambo kama vile TFF ni mali yao wanajua watabebwa, kwanza wao ndio waliomwambia Ngassa siyo mali kitu, ameshuka

thamani wakati ule sisi tulitaka kutoa milioni 20 wao wakaambiwa waongeze tano iwe sh 25 milioni ili wamchukue, walikataa na kusema hana thamani ya hela hiyo imekuwaje sasa? alisema kwa kuhoji.
Wakati Ngassa akitua Jangwani kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Niyonzima alisema ametimiza malengo yake ya kuipatia Yanga ubingwa na kilichobaki sasa ni kutimiza malengo yake ya kutafuta mafanikio mengine.

“Nilipokuja Tanzania nilikuwa na ndoto ya kuipatia Yanga ubingwa, hilo limetimia sasa ninaanza ndoto za kutafuta masilahi yangu,” alisema Niyonzima. na kuongeza:

“Tumekuwa katika mazungumzo na Yanga kwa wiki mbili sasa lakini, tukayasitisha kwa sababu ya mechi ya Simba, niliwapa siku mbili baada ya mechi hii ili wanipe jibu kamili vinginevyo natimkia timu nyingine.”

Niyonzima alisema si chezi soka la mapenzi ingawa ameishi na wanayanga vizuri, kila mtu nampenda na hata familia yake inapenda kuishi na wanayanga.

“Mimi sina tatizo na Yanga, nimeishi nao vizuri, ila masilahi yangu ni zaidi ya Yanga, wakishindwa, kunipa ninachokitaka, nitakwenda popote nitakapopata masilahi, iwe Simba ama Azam niko tayari kwenda kama tu wataweka dau kubwa mezani,” alifafanua Niyonzima.

Klabu ya Real Madrid imethibitisha kuwa kocha wa timu hiyo Jose Mourinho ataondoka kwenye kibarua cha kuifundisha timu hiyo mwishoni mwa msimu.

 
Jose Mourinho

Rais wa klabu ya Real Madrid,Florentino Perez amewaambia waandishi wa habari jumatatu jioni kuwa Mourinho hatofukuzwa bali wamekubaliana kumaliza mkataba wao na kocha huyo raia wa Ureno.

Aidha Madrid, imeongeza kuwa haijaanza mazungumzo na kocha yeyote kwaajili ya kuchukua nafasi ya Mourinho lakini vyanzo mbalimbali vya habari za michezo zinamtaja kocha wa PSG ya Ufaransa, Carlo Ancelloti kuchukua jukumu la kuifundisha Madrid msimu ujao.
Duru za kimichezo zinasema, Jose Mourinho huenda akarejea nchini Uingereza kuifundisha klabu yake ya zamani ya Chelsea baada ya kuwepo makubaliano baina yake na uongozi wa klabu hiyo.
 Hatimae meneja Rafael Benitez ataondoka Chelsea akiwa na tabasabu baada ya timu yake kubeba ubingwa wa Kombe la Europa League kwa kuifunga timu ya Benfica ya Ureno 2-1 usiku wa Jumatano katika uwanja wa Amsterdam, Uholanzi.


Rafael Banitez na kombe la Ligi ya Uropa baada ya Chelsea kufunga Benfica
 Hii ni baada ya Branislav Ivanovic kufunga bao maridadi kwa kichwa wakati wa muda wa ziada wa majeruhi.


Lakini baada ya kuifunga Benfica mashabiki hao hao ambao walikuwa hawampendi Benitez waliishangilia ushindi wa timu yao kwa vifijo na nderemo huku wakisahau chuki waliokuwa nao kwa kaimu meneja huyo.

Mwaka jana Chelesea ilishinda Kombe la Klabu bingwa bara Ulaya na mwaka huu wamebeba kombe la Europa League.

Bao lakwanza la Chelsea lilifungwa na mshambulizi Fernando Torres nao Benfica wakapata lao kupitia mwaju wa penalti uliofungwa na Oscar Cardozo.

Ushindi wa Chelsea unamfanya Rafael Benitez kuwa meneja wa nne kushinda kombe la Klabu Bingwa Uropa na la Europa League zaidi ya mara mmoja.

Wengine amabo wamewahi kushinda kumbe hilo zaidi ya mara moja ni Giovanni Trapattoni: 1977 (Juventus); 1991 (Inter); 1993 (Juventus) ,Luis Molowny: 1985 & 1986 (Real Madrid) Juande Ramos: 2006 & 2007 (Sevilla).

Ligi kuu soka nchini England inazidi kuelekea ukingoni kwa timu kucheza michezo yao ya mwishoni,



Anderson(kulia) akichuana na Azpilicueta(kushoto)

Jumapili ya leo kulichezwa michezo miwili pekee,
Manchester United walikuwa nyumbani kuwakaribisha Chelsea The blues kwenye uwanja wa Old Traford, wakati Liverpool walikuwa kwenye uwanja wa nyumbani kupambana na watani zao wa jadi, Everton.
Katika mchezo ambao BBC Ulimwengu wa soka ilikuwa ukiutanga moja kwa moja, United walijikuta wakilala kwa bao moja ka bila katika mchezo ambao ulikuwa hauna mashamu shamu kama wengi walivyotarajia.
Bao hilo la Chelsea lilifungwa na Kiungo Mhispania Juan Matta dakika ya 87 baada ya kuachia shuti la wastani lililomgonga beki wa United Phil Jones na kuwafanya mashabiki wa United kukaa kimya uwanjani.
Katika mchezo huo United walimaliza wakiwa pungufu baada ya Rafael Da Silva kupewa kadi nyekundu dakika chache kabla ya mchezo kumalizkka baada ya kumkwatua beki wa Chelsea David Luiz ambaye ni mbrazil mwenzake.
Matokeo haya yanaifanya Chelsea kupanda hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kuu wakiwa na pointi 68 huku Arsenal wakishuka hadi nafasi ya nne na pointi 67 na Tottenham wakishika nafasi ya tano na pointi 65. Chelsea itapambana na Tottenham hapo jumatano usiku katika mechi itakayokuwa na upinzani mkubwa kwa timu zote mbili kusaka uwezekano wa kumaliza kwenye nne bora ya ligi kuu soka nchini England.
Katika mchezo mwingine wa mapema, Everton walikuwa wageni wa Liverpool katika mchezo wa watani wa jadi wa mji wa Merseyside.
Mapema Sylivan Distin alifunga bao kwa kichwa lakini mwamuzi Michael Oliver alilikataa kwa kuwa Victor Anichebe wa Evrton alimchezea vibaya golikipa wa Liverpool Pepe Reina.
Everton hawajawahi kushinda kwenye uwanja wa Anfield tangu mwaka 1999 katika mechi za watani wa jadi na Liverpool za ligi kuu soka nchini England.
Mechi ya leo ya sare ya Liverpool na Everton inatimiza idadi ya michezo 35 ya kutoka sare katika ligi kuu soka nchini England.
Ligi hiyo itaendelea tena hapo kesho jumatatu kwa mchezo mmoja kati ya Sunderland watakao wavaa Stoke City.

SIMBA YATINGA KATIKA NAFASI YA TATU 
 
 
 Kiungo Amri Kiemba alifunga bao moja na kutengeneza moja wakati Simba ilipoisambaratisha Ruvu Shooting kwa mabao 3-1 jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika harakati zake za kusaka nafasi ya tatu.

Kiemba alifunga bao lake kwa shuti la umbali wa mita 25 katika dakika ya 14, ambapo Shooting walisawazisha bao hilo katika dakika ya 52 kupitia Abdulrahman Musa kabla ya Kiemba kutengeneza bao la tatu lililofungwa na Rashid Mkoko katika dakika ya 89, wakati Christopher Edward alipachika bao la pili la Simba akimalizia mpira uliotemwa na kipa Benjamani Haule katika dakika ya 87.

Kwa matokeo hayo Simba imepanda hadi nafasi ya tatu ikiwa na pointi 42 na kuiacha Kagera Sugar katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo.

Kocha wa Simba, Patrick Liewig akizungumza baada ya mechi hiyo aliwasifu wachezaji wake kwa kucheza vizuri na kufanikiwa kupata matokeo hayo mazuri.

“Vijana wangu wanafuata maelekezo yangu vizuri, nadhani hiyo ndiyo siri ya mafanikio yetu kwa sasa,” alisema Liewig.

Ruvu Shooting waliianza mechi ya jana kwa kasi na kufika langoni kwa Simba katika dakika ya saba baada ya shuti la Musa kutoka sentimita chake katika lango la Simba.

Simba walijibu mapigo katika dakika ya 14 na kufanikiwa kupata bao la kuongoza lililofungwa na Kiemba kwa shuti la umbali wa mita 25, akimalizia vizuri pasi ya Felix Sunzu aliyempokonya mpira beki wa Shooting, Shaaban Suzan.

Kama hiyo haitoshi, Sunzu nusura aipatie Simba bao baada ya kuunganisha kwa kichwa krosi ya Kiemba na kugongesha mwamba katika dakika ya 21.

Katika mechi hiyo kipa wa Shooting, Benjamin Haule alifanya kazi ya ziada kuokoa shuti la Haruna Chanongo katika dakika ya 34.

Pia beki Said Madega wa Shooting alionyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea vibaya Chanongo katika dakika ya 45.

Simba katika mechi hiyo walitumia zaidi winga zao mbili zinazoongozwa na Chanongo na Ramadhan Singano kupitisha krosi za juu kwa Sunzu, wakati Shooting wenyewe walicheza pasi fupifupi kwa kasi, lakini walikosa umakini kwenye umaliziaji.

Kurejea kwa Sunzu kunazidi kuimarisha safu ya ushambuliaji ya Simba kabla ya mchezo wao wa mwisho wa msimu huu dhidi ya mahasimu wao Yanga hapo Mei 18.
Shooting walisawazisha bao hilo katika dakika ya 52 baada ya Musa kuwahadaa mabeki wa Simba kabla ya kufunga bao hilo.

Kocha Liewig alimpumzisha Sunzu na kumwingiza Mrisho Ngassa mwanzoni mwa kipindi cha pili mabadiliko yaliyokuwa na faida kubwa kwa Simba vijana hao wa Msimbazi.

Katika dakika ya 87 Simba walifanikiwa kupata bao kupitia kwa Edward akimalizia mpira uliotemwa na kipa Haule, ambapo wakati Shooting wakijiuliza Mkoko aliipatia Simba bao la tatu katika dakika ya 89 akiunganisha kwa kichwa krosi ya Kiemba.

Simba sasa imebakiza mechi dhidi ya Mgambo JKT hapo Jumatano kabla ya kuivaa Yanga hapo Mei 18    

Lionel Messi hangelizuia kichapo walichopewa Bercelona cha magoli matatu kwa yai na Bayern Munich ya Ujumani.

Wachezaji wa Bayern Munich
Haya ni kwa mujibu wa mchezaji mwingine wa Barcelona Gerard Pique.
Arjen Robben na Thomas Mueller walifunga bao moja kila mmojan naye Pique akijifunga mwenyewe na kuiwezesha Bayern kufuzu kwa fainali ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya kwa jumla ya magoli 7-0.
Pique amesema licha ya kuwa Messi ndiye mchezaji bora zaidi duniani kwa sasa, hilo halikuwa tatizo la kushindwa kwao.
Messi kutoka Argentina, ambaye amefunga magoli 54 baada ya kucheza mechi 45 msimu huu, alitarajiwa kucheza katika kipindi cha pili kama mchezaji wa ziada hasa baada ya kufunga bao kwenye mechi ya ligi kuu siku ya Jumamosi dhidi ya Althletics Bilbao.
Kocha wa Barcelona Tito Vilanova, amesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, alipata jeraha la paja wakati wa mechi yao siku ya Jumamosi na hivyo ingelikuwa hatari zaidi ikiwa angelicheza mechi hiyo akiwa na maumivu.

Real Madrid yaingia mkataba na Fly Emirates

 

Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania ieingia mkataba mpya wa udhamini a jezi na kampuni ya usafirishaji wa anga ya Fly Emirates . Mkataba huo utaanza kufanya kazi msimu ujao ambao Real watavaa jezi zenye nembo ya Emirates kwa muda wa miaka mitano .

Mkataba huu mpya unamaanisha kuwa Real itamaliza mahusiano yake na kuchezesha kamari za kwenye michezo ya huko Austria ya Bwin ambayo imekuwa ikidhamini Madrid kwa miaka sita iliyopita tangu mwaka 2007 ambapo Madrid ilikuwa

inapata Euro milioni 15 kwa mwaka .
Mkataba wa udhamini ambao Madrid imeingia na Emirates ni wa miaka mitano ambapo Emirates itawalipa Madrid Paundi milioni 25 kwa mwaka .
Mkataba huu utaofanya Real Madrid kuwa timu ya tatu kwenye orodha ya timu zinazodhaminiwa kwa fedha nyingi nyuma ya Manchester United wanaodhaminiwa kwa Euro milioni 33 na Fc Barcelona wanaodhaminiwa na Qatar Foundation kwa Euro milioni 30.

Teknolojia ya golini kutumika msimu ujao

Goal-line technology
Picha ya jinsi mpira ulivyovuka mstari,England Vs Ujerumani Kombe la dunia 2010.


Klabu za ligi kuu soka nchini England zimepitisha sheria ya kutumia teknolojia ya camera katika maamuzi ya mchezo wa soka kuanzia msimu ujao.
Kampuni ya Uingereza ya Hawk-Eye imeshinda tenda na kupatiwa mkataba wa kufunga vifaa maalumu kwenye viwanja vyote 20 vya timu za ligi kuu nchini England.
Hawk-Eye itafunga kamera saba kwenye kila goli maalumu kwa kutambua kama mpira umevuka mstari wa goli na kumjulisha mwamuzi wa mchezo huo kupitia saa yake ya mkononi,na imesema inauhakika hakuna marejeo yoyote ya matangazo ya picha ambayo yatapingana na maamuzi ya teknolojia hiyo.
Kampuni hiyo ya Hawk-Eye inajulikana kwa kufunga teknolojia kama hiyo kwenye mchezo wa Tenesi na Kriketi,ambapo camera maalumu huweza kutambua iwapo mpira umegusa mstari ama la na kumjulisha mwamuzi na wasaidizi wake ndani ya sekunde chache.
Chama cha soka nchini England FA,kitafunga vifaa hivyo kwenye uwanja wa Wembley tayari kwa kutumika kwenye mchezo wa ngao ya jamii hapo mwezi wa nane mwaka huu.
Vilabu vikubwa vyote nchini England vimepiga kura ya kupitisha maamuzi hayo katika mkutano wao uliofanyika hii leo jijini London,Huku viwanja vingine vya timu 17 zitakazosalia ligi kuu na zile 3 zitakazopanda daraja vitawekewa teknolojia hiyo na shughuli nzima itachukua wiki sita kukamilika.
Msukumo wa kutumia teknolojia maalumu ya kutambua goli ilipata nguvu baada England kukataliwa goli lao la kusawazisha walipocheza na Ukraine,Mchezo ambao England walifungwa bao moja kwa bila kwenye michuano ya kombe la mataifa barani Ulaya mwaka 2012, Ambapo mwezi mmoja baadaye bodi ya vyama vya soka vya kimataifa (IFAB) katika kikao chake mjini Zurich kilipitisha teknolojia mbili ili zitumike kwenye michezo ya soka.
Nalo shirikisho la kandanda Ulimwenguni FIFA kupitia kwa rais wake Sepp Blater alisema kukataliwa kwa goli la Frank Lampard kwenye mechi ya robo fainali kati ya England na Ujerumani mwaka 2010 katika michuano ya kombe la dunia,kulichangia kwa kiasi kikubwa maamuzi ya shirikisho hilo kupitisha sheria ya matumizi ya teknolojia ya kutambua goli.
Chama cha soka cha England kimesema kingependa kuona teknolojia hiyo inaanza kutumika kwa vitendo haraka iwezekanavyo.

Kenya yaibana Nigeria nyumbani kwao

Timu ya Harambee Stars
Harambee Stars ya Kenya licha ya kupata mateso tangu wawasili nchini Nigeria kucheza na Super eagles katika mechi ya kutafuta kuingia katika kombe la dunia Jumamosi nusura wawaaibishe mabingwa wa Afrika kwa kutoka sare ya 1-1 huko mjini Calabar , Nigeria.
Kenya ndio iliyokuwa ya kwanza kufunga kupitia mchezaji Francis Kahata katika dakika ya 36 kipindi cha kwanza.

Licha ya Sduper Eagles kuwateremsha miamba yake yote kama vile John Obi Mikel na Victor Moses wa Timu ya Chalsea ya Uingereza lakini hawakufua dafu kwa kenya hadi katika dakika za majeruhi ya kipindi cha pili.
Katika dakika hizo za majeruhi mcherzaji Nnamdi Oduamadi aliiondolea Super Eagles aibu kwa kufunga bao na punde tu firimbi yamwisho kumaliza mechi ikapulizwa.
Mara ya mwisho kwa timu hizo kukutana ni katika mechi ya kirafiki mwezi Machi ,2011 Mjini Abuja ambapo Super Eagles ilifunga 3-0.
Wakati ambapo harambee Stars ya Kenya ilikuwa karibu sana kuifunga Nigeria ni katika mechi iliyochezwa Januari 12, 1997 wakati timu zote mbili zilitoka sare ya 1-1 mjini Nairobi. Lakini katika mechi ya marudio iliyochezwa Nigeria Juni 7 .1997 Nigeria iliizaba Harambee Stars 3-0. Hii vile vile ilikuwa ni mecchi ya kutafuta nafasi ya kucheza Kombe la Dunia la mwaka 1998.
Miaka iliyopita Nigeria imekuwa ikiipepeta Kenya . Katika mechi ya kutafuta nafasi ya kucheza kombe la dunia mwaka 1986, Harambee Stars walifungwa na Super Eagles 3-0 hii ilikuwa Juni 7, 1985 na baadae kukamilishi kibarua chao na kufaulu kuingia kombe la dunia kwa kuichapa Kenya 1-3
Wachezaji Harambee Stars: Arnold Origi, David Owino, Mulinge Munandi, David Ochieng, Brian Mandela, Victor Wanyama, David Gateri, Johanna Omollo, Jamal Mohammed, Dennis Oliech and Francis Kahata. Coach Adel Amrouche
Wachezaji wa Super Eagles: Vincent Enyeama, Solomon Kwambe, Godfrey Oboabona, Kenneth Omeruo, Elderson Echejile, Sunday Mba, Mikel Obi, Eddy Onazi, Obafemi Martins, Victor Moses and Brown Ideye

Waamuzi

Referee: Joshua BONDO (BOT)
Assistant Referee 1: Meshack MEDUPI (BOT)
Assistant Referee 2: Moemedi MONAKWANE (BOT)
Fourth official: Kutlwano LESO (BOT


Malawi yaifunga Namibia nyumbani

 Timu ya Malawi

Malawi ilikuwa na Jumamosi njema wakati waliposafiri hadi Mjini Windhoek,Namibia na kufaulu kuwachapa vijana wa nyumbani bao moja kwa sufuri katika uwanja wao wa Sam-Nujoma-Stadium .
Bao la wageni lilifungwa na Gabadin Mhango katika dakika ya 70 ya kipindi cha pili .
Namibia walijitahidi kukomboa bao hilo katika muda wa dakika 20 zilizosafilia lakini hawakufaulu.
Hata baada ya kuimuingiza mchezaji wake matata Tangeni Shipahu , Rudolf Bester na mshambuliaji Manfred Starke,vijana wa Namibia hawakuwa na lao.
Mechi kumalizika Namibia 0- 1 Malawi.

Waamuzi

Referee: Med SAID KORDI (TUN)
Assistant Referee 1: Bachir HASSANI (TUN)
Assistant Referee 2: Mohsen BEN SALEM (TUN)
Fourth official: Nasrallah JAOUADI (TUN)

 

MWENYEKITI WA SIMBA ISMAIL ADEN RAGE AWASILI KWA KISHINDO JIJINI DAR ES SALAAM AKITOKEA NCHINI INDIA,AZUNGUMZA NA WANACHAMA MAKAO MAKUU YA KLABU YA SIMBA

  Mashabiki na wachama wa Simba wakilisukuma gari alilopanda Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage wakati alipowasili Makao Makuu ya klabu hiyo jana akitokea India kwa matibabu..
 Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, akizungumza na wanachama  na mashabiki timu hiyo, ambao walifika Makao Makuu ya klabu hiyo, Msimbazi jijini Dar es Salaam, mara baada ya Rage kuwasili  jana  akitokea nchini India kwa matibabu.Picha na Francis Dande

TAIFA STARS YAIBUKA NA USHINDI ZIDI YA TIMU YA TAIFA YA MOROCCO KATIKA MECHI YAKE YA KUFUZU KUCHEZA KOMBE LA DUNIA MWAKANI NCHINI BRAZIL

Wachezaji wa Taifa Stars wakishangilia bao lao la kwanza lililofungwa na Thomas Ulimwengu.

TIMU ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo imeishushia kichapo timu ya taifa ya Morocco baada ya kuilaza kwa mabao 3-1 kwenye mechi iliyopigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mabao ya Taifa Stars yamefungwa na wachezaji wa TP Mazembe, Mbwana Samatta aliyetupia kambani bao mbili na Thomas Ulimwengu aliyefunga bao moja. Mchezo huo ulikuwa wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.

 Arsenal, Man Utd, moto mkali, Chelsea, City doro

DSC02407

*Timu nne bora zilizozoeleka zajikita kileleni

*Man United yavuna, Liverpool mambo bado

Mzunguko wan ne wa Ligi Kuu ya Uingereza umeshuhudia mwendelezo wa makubwa kadhaa, ukiwamo moto ulioanzishwa na Arsenal.
Timu ‘ndogo’ zilizokuwa zinashika nafasi za juu zimefurushwa, huku nne bora zikirejea zile zilizozoeleka.
Hata kama itakuwa ni kwa muda, lakini Arsenal, Chelsea, Manchester City na Manchester United zimerejea maeneo zinakopenda kuita nyumbani.
Arsenal na United zilirejea baada ya karamu kubwa za mabao, huku Chelsea na City zikitoa sare.
Arsenal iliifunga Southampton mabao 6-1, idadi ambayo ni kubwa kwa Washika Bunduki wa London waliokuwa na mabao mawili tu ya kufunga katika mechi tatu zilizotangulia.
Hata hivyo, Arsenal pia kwa mara ya kwanza msimu huu imeruhusu bao, langoni akiwa amerejea golikipa namba moja, Wojciech Szczesny, aliyeonekana kutotulia vyema langoni kama Vito Mannone aliyedaka mechi mbili zilizopita.
Nyota mpya wa The Gunners, Lukas Podolski alipata bao la pili la msimu, huku Gervais Lombe Yao Kouassi ‘Gervinho’ akifunga mawili na kijana The Walcott naye akipachika bao. Mawili walijifunga Southampton wenyewe.
Swansea walioanza kwa kasi msimu na kukalia uongozi wa ligi, wameanza kufungwa, baada ya kuchambuliwa mabao 2-0 na Aston Vlla ambayo msimu uliopita ilikosa makali.
Huu ni ushindi wa kwanza kwa Aston Villa, waliopata mabao kupitia kwa Matthew Lowton  na mchezaji wake mpya kutoka Genk ya Uholanzi, Christian Benteke, raia wa Ubelgiji na Kongo.
Timu nyingine iliyokuwa ikijidai juu ya msimamo wa ligi ni West Bromwich Albion ambao wamekung’utwa mabao 3-0 na timu ngumu ya Fulham.
Alikuwa ni mkongwe Dimitar Berbatov aliyetokea Manchester United dakika za mwisho za usajili msimu huu aliyewafungia wageni mabao mawili, moja kwa penati. Jingine lilitiwa kimiani na Steve Sidwell, mechi ikikaribia kumalizika.
Ilikuwa siku mbaya kwa Peter Odemwingie wa Fulham, aliyepata kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumkwatua Sascha Riether.
Norwich iliendelea na rekodi yake ya kutoshinda mechi hata moja, baada ya suluhu yake nyumbani dhidi ya West Ham United wanaofundishwa na mkongwe Sam Allardyice.
Mashetani Wekundu waliungana na Arsenal kwa karamu ya mabao, siku hii ambayo mchezaji wa, Paul Scholes  alicheza mechi ya 700.
United walicheza dhidi ya timu isiyotabirika ya Wigan inayofunzwa na Roberto Martinez, ambapo Scholes aliungana na Javier Hernandez; Alexander Büttner na Nick Powell kufunga.
Mfungaji mpya wa United, Robin van Persie hakupata kitu kwenye mechi hiyo, na aliingia dakika ya 71. Pia Hernandez alikosa penati iliyodakwa na kipa Ali Al-Habsi, kama alivyokosa RVP mechi iliyopita dhidi ya Southampton.
Queens Park Rangers (QPR) ilitoshana nguvu na  Chelsea kwa kutoka suluhu, ikidhihirisha maneno kwamba Chelsea licha ya kushinda mechi zilizotangulia, haikuwa imekaa imara sana.
Mechi ilishuhudia mchezaji wa QPR, Anton Ferdinand akikataa kumpa mkono John Terry anayedaiwa kumtukana kibaguzi na Ashley Cole aliyemtetea Terry mahakamani.
Vijana wa Roberto Mancini nao walishindwa kuwabanjua Stoke City, baada ya kutoka nao sare ya bao 1-1.
Stoke walitangulia kufunga kupitia kwa mkongwe Peter Crouch kwa ‘mkono wa mungu’. City walikomboa bao kupitia kwa mchezaji mpya, Javi Garcia.
Michael Owen aliyesajiliwa na Stoke kama mchezaji huru baada ya dirisha la usajili kufungwa, aliingia dakika ya 90 kuchukua nafasi ya Crouch. Bila shaka ataanza siku zijazo.
Ukame wa ushindi umezidi kuiandama Liverpool ya Brendan Rodgers, baada ya kuambulia sare ya bao 1-1 nyumbani kwa Sunderland.Liverpool walitanguliwa kutunguliwa katika dakika ya 29 kupitia mchezaji mpya kutoka Wolverhampton Wanderers, Steven Fletcher, kabla ya Luis Suarez kupunguza majonzi dakika ya 71.
MSHAMBULIAJI
  
 Emmanuel Okwi.
MSHAMBULIAJI nyota wa Simba, Emmanuel Okwi ameitaka Yanga kuonana na viongozi wa Simba kama ina nia ya kumsajili kwa ajili ya msimu ujao.
Pamoja na hivyo, Okwi amesisitiza, ndoto yake ni kucheza soka la kulipwa barani Ulaya na kesho au keshokutwa ataanza safari ya kwenda nchini Italia kufanya majaribio katika klabu ya Parma.
Akizungumza jana kutokea Kampala, Uganda, Okwi alisema ameshitushwa na taarifa za yeye kujiunga na Yanga na kusisitiza kuwa anapenda kuishi maisha kwa kufuata taratibu.
“Ninaweza kucheza Yanga kwa kuwa soka ni kazi yangu, lakini bado nina mkataba na Simba. Waambie Yanga wazungumze na Simba halafu nitazungumza nao, lakini hayo yaliyoelezwa wasiyafuatilie,” alisema.
Alipoulizwa kuwa kuna baadhi ya wadau wa Yanga wakiongozwa na mtoto wa kigogo mkubwa kabisa walimfuata Kampala na kuzungumza naye jijini Kampala kwa ajili ya kufanya usajili ajiunge na Yanga, alisema: “(kicheko), hapa Kampala ninakutana na Watanzania wengi sana, wako Yanga wengine Simba. Sidhani kama ni vibaya kuzungumza na mtu, sina uadui,” alisema.
Jana, mashabiki wa Simba walikuwa katika hofu kuu kuhusiana na taarifa za Okwi kusaini kuichezea Yanga kwa ajili ya msimu ujao. Hata hivyo, mkataba wa Okwi unaomalizika Julai mwakani.
Okwi alikataa kulizungumzia suala hilo na kusisitiza anataka kumalizia suala lake la kupata Visa kwa ajili kwenda nchini Italia kwa ajili ya majaribio.
“Nafikiri nitapata leo ili nianze safari mapema, sasa niko kwenye ubalozi wa Italia, niache nishughulikie kwanza. Tunaweza kuzungumza vizuri zaidi baadaye,” alisema.
Pamoja na maelezo hayo ya Okwi, taarifa za uhakika zinaeleza Yanga imekuwa ikifanya naye mazungumzo kwa lengo la kuvunja mkataba wake na Simba kwa kitita kikubwa cha fedha.

Uhispania mabingwa Euro 2012

Uhispania
Ni dhahiri kwamba timu ya Uhispania ndio iliothibitisha mchezo bora zaidi katika fainali na Italia
Uhispania waliandikisha historia kwa maarifa ambayo sio rahisi kuiga, kwa kuifunga Italia magoli 4-0 katika fainali ya Euro 2012 usiku wa Jumapili, mjini Kiev, Ukraine.
Licha ya mchezo mzuri wa Italia, vijana wa meneja wa Uhispania, Vicente del Bosque walithibitisha kwamba kimataifa wanaweza kujigamba wao ndio wenye mchezo bora zaidi duniani, kwa kuzingatia namna walivyoichezea timu ya Italia, na kuwalazimisha kusalimu amri.
David Silva aliifungia Uhispania bao la kwanza, na kabla nusu ya kwanza ya mchezo kumalizika, mchezaji mpya wa Barcelona, Jordi Alba aliandikisha bao la pili, baada ya kukimbia kwa kasi na kumalizia kwa ustadi kabisa.
Ingawa Italia walikuwa na upungufu wa mchezaji mmoja, baada ya kumpoteza mchezaji wa zamu wa tatu Thiago Motta baada ya kujeruhiwa, walicheza kwa bidii, lakini wataalamu wa kandanda kwa upande wa kupokezana mpira, Uhispania, waliwadunisha kabisa.
Fernando Torres aliingia kama mchezaji wa zamu, na akafanikiwa kuubadilisha mchezo, na akiandikisha bao la tatu la Uhispania, kabla ya mwenzake katika klabu ya Chelsea, Juan Mata, kuandikisha bao la nne na la mwisho la Italia, na ambalo bila shaka liliwavunja moyo kabisa mashabiki wote wa Italia.
Mchezo huo bila shaka umeyazima matamshi ya baadhi ya watu ambao awali walimlazimu kocha wa Uhispania Del Bosque na wachezaji wake kujitetea katika mkutano na waandishi wa habari, kabla mechi ya fainali kuanza, kwamba mchezo wao katika mashindano ya Euro 2012 umekosa msisimko.
Lakini usiku wa Jumapili mambo yalikuwa tofauti.
Maarifa yote yaliyowawezesha kuwa mabingwa wa Euro 2008 na vile vile Kombe la Dunia la mwaka 2010 nchini Afrika Kusini yalijitokeza.
Ilikuwa ni fainali ambayo ilimvunja moyo kabisa kocha wa Italia, Cesare Prandelli, lakini bila shaka haikuwa fedheha kushindwa na timu yenye maarifa ya hali ya juu kiasi hicho.
Italia itaweza kujivunia namna ilifika katika fainali, licha ya kushindwa kwa magoli mengi na timu ambayo ilikuwa ni wazi imo katika kiwango cha pekee.

Chris Hughton meneja mpya Norwich City

Klabu ya Norwich City imemteua meneja wa Birmingham City, Chris Hughton kuwa meneja wake mpya.
Chris Hughton meneja mpaywa Norwich City
Chris Hughton meneja mpaywa Norwich City
Hughton ambaye enzi zake za kusakata kandanda aliwahi kuichezea klabu ya Tottenham na timu ya taifa ya Jamhuri ya Ireland akicheza nafasi ya ulinzi, alifanikiwa kuifikisha Birmingham katika hatua ya kucheza mechi za mwisho kuwania kupanda ngazi ya Ligi Kuu ya England msimu uliopita ambapo walitolewa na Blackpool.
Norwich hawakuwa na meneja tangu Lambert alipoondika katika klabu hiyo na alitangazwa kushika hatamu za kuinoa Aston Villa tarehe 2 mwezi huu wa Juni.
Kupitia mtandao wa kijamii wa tweeter klabu ya Birmingham iliandika: "Klabu ingependa kumshukuru Chris Hughton na kikosi chake kwa jitahada walizoonesha kwa muda wa miezi 12. Kazi ya kumsaka meneja mpya imeanza."

Kocha afariki saa 24 baada ya mkataba.


 Manuel Preciado
Kocha mpya aliyeteuliwa juzi Manuel Preciado amefariki saa 24 baada ya kutangazwa kama Kocha wa klabu ya Uhispania, Villarreal.
Kocha huyo ambaye hapo zamani alikua kocha wa Sporting Gijon alifariki kutokana na mshtuko wa moyo akiwa na umri wa miaka 54.
Kifo chake kimetokea saa 24 baada ya kukubali mkataba wa kuiongoza klabu ya Villareal iliyoshuka daraja, ambapo mkataba wake ulikua wa kuanza msimu wa mwaka 2012 hadi 2013.
Preciado alifutwa kazi na Sporting Gijon mnamo mwezi Januari licha ya kuiwezesha klabu hio kupanda daraja mara mbili kuingia Ligi kuu ya Uhispania, La Liga.
Mnamo mwezi Aprili mwaka 2011, klabu yake ya Sporting Gijon iliikwamisha klabu maarufu ya Real Madrid kwa kuvunja rekodi yake ya miaka tisa bila kupoteza kwenye uwanja wa nyumbani safari hii ikiwa chini ya Jose Mourinho.
Wakati wake wa uchezaji soka Preciado alicheza kama beki aliyeanzia uchezaji wake katika klabu ya Racing Santander na pia kushiriki mechi za vilabu kama Linares, Mallorca, Alaves, Ourense na Gimnastica.
Baada ya kustaafu kama mchezaji mwaka 1992, akaanza shughuli za ukufunzi akianzia klabu ya Gimnastica na pia kuifunza Racing B, Racing Santander, Levante na Murcia kabla ya kujiunga na Sporting Gijon mwaka 2006.
Baadaye aliiwezesha klabu hio kupanda daraja hadi Ligi kuu ya Uhispania katika msimu wake wa pili na kukaa na klabu hio kwa kipindi cha miaka sita.
Kocha mpya aliyeteuliwa juzi Manuel Preciado amefariki saa 24 baada ya kutangazwa kama Kocha wa klabu ya Uhispania, Villarreal.
Kocha huyo ambaye hapo zamani alikua kocha wa Sporting Gijon alifariki kutokana na mshtuko wa moyo akiwa na umri wa miaka 54.
Kifo chake kimetokea saa 24 baada ya kukubali mkataba wa kuiongoza klabu ya Villareal iliyoshuka daraja, ambapo mkataba wake ulikua wa kuanza msimu wa mwaka 2012 hadi 2013.
Preciado alifutwa kazi na Sporting Gijon mnamo mwezi Januari licha ya kuiwezesha klabu hio kupanda daraja mara mbili kuingia Ligi kuu ya Uhispania, La Liga.
Mnamo mwezi Aprili mwaka 2011, klabu yake ya Sporting Gijon iliikwamisha klabu maarufu ya Real Madrid kwa kuvunja rekodi yake ya miaka tisa bila kupoteza kwenye uwanja wa nyumbani safari hii ikiwa chini ya Jose Mourinho.
Wakati wake wa uchezaji soka Preciado alicheza kama beki aliyeanzia uchezaji wake katika klabu ya Racing Santander na pia kushiriki mechi za vilabu kama Linares, Mallorca, Alaves, Ourense na Gimnastica.
Baada ya kustaafu kama mchezaji mwaka 1992, akaanza shughuli za ukufunzi akianzia klabu ya Gimnastica na pia kuifunza Racing B, Racing Santander, Levante na Murcia kabla ya kujiunga na Sporting Gijon mwaka 2006.
Baadaye aliiwezesha klabu hio kupanda daraja hadi Ligi kuu ya Uhispania katika msimu wake wa pili na kukaa na klabu hio kwa kipindi cha miaka sita.

 Dirk Kuyt ahama Liverpool


Mchezaji wa safu ya mbele ya Uhalonza Dirk Kuyt ameihama klabu ya Liverpool na kujiunga na Fenerbahce ya Uturuki kwa mkataba wa miaka mitatu. Mshambuliaji huyo anaihama Liverpool baada ya kipindi cha miaka sita.
Kuyt mwenye umri wa miaka 31 alihamia uwanja wa Anfield mnamo mwaka 2006 na kushiriki mara 250 akifunga jumla ya mabao 71.
Taarifa ya Liverpool iliyotolewa kufuatia hatua hio imesema kua Kila mmoja anamtakia Dirk kila la heri na kumshukuru kwa mchango wake.
Aliposajiliwa, Kuyt alisema wakati huo, Kwangu mimi, Liverpool ni ndoto iliyokamilika. Hapana cha kuilinganisha nayo klabu hii, yenye sifa na historia ya kujivunia, alisema.
Mechi yake ya kwanza kushiriki ilikua dhidi ya West Ham United mwezi Agosti mwaka 2006, alipoingia kuchukua mahala pa Peter Crouch ambapo upande wake uliondoka na ushindi wa 2-1.
Bao lake la kwanza lilipatikana mwezi mmoja baadaye alipofunga bao la kwanza katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Newcastle.
Baadaye alipendwa na mashabiki wa Liverpool, kivutio kikiwa mchangon wake katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Everton kwenye uwanja wa Goodison Park mwaka 2007 kisha alipofunga 3- peke yake dhidi ya Manchester United, mahasimu wakuu wa klabu kutoka Anfield.
Kuyt ambaye ameshiriki mara 80 kwa Timu yake ya Taifa ya Uholanzi, pia alifunga dhidi ya AC Milan katika mchuano wa Ligi ya mabingwa mwezi Mayi mwaka 2007.
Msimu uliopita mshambuliaji huyo alipata shida kupata nafasi katika kikosi kikuu, akishiriki mara 22 pekee na kuletwa kama mchezaji wa ziada mara tano katika mechi tisa za mwisho wa msimu.
Kwa wakati huu mchezaji huyo aliyesajiliwa kutoka klabu ya Utrecht yuko pamoja na wenzake wa Timu ya Taifa ya Uholanzi wakijinoa kwa ajili ya michuano ya Ulaya 2012 ambapo Wadachi watachuana na Denmark katika mechi yao ya ufunguzi jumamosi ijayo.
Mshambulizi matata Asamoah Gyan hayuko kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ghana kilichotajwa na Kocha Kwesi Appia.

Asamoah and Dede Ayew nje



Asamoah Gyana na Dede Ayew wote nje
Wengine waliotemwa ni mwamba wa Chelsea Michael Essien na Andre 'Dede' Ayew ambaye ana jeraha.
John Paintsil na aliyekuwa nahodha wa Ghana John Mensah nao pia hawamo.
katiuka kikosi chake kipya kocha Appiah amewajumuisha wachezaji sita wapya wengi wakiwa wanachezea soka la kulipwa ulaya. hata hivyo amejumuisha wachezaji tisa toka ligi ya nyumbani.
Asamoah Gyan aliamua kujiondoa toka timu ya taifa baada ya kushambuliwa na mashabiki baada ya uchezaji wake duni katika michuano ya kombe la bara afrika la hivi majuzi.
ilikuwa inatarajiwa kwamba angelirejea katika timu kabla ya mwezi ya Juni.
kwa upande wa Ayew , alifanyiwa upasuaji hivi majuzi nae Essien alisema atashughulika zaidi na timu yake ya Chelsea.
Kikosi Cha Ghana
Golkipa: Adam Kwarasey (Stromsgodset, Norway), Robert Dabuo (Wa All Stars), Daniel Adjei (Liberty Professionals), Ernest Sowah (Berekum Chelsea)
Walinzi: Samuel Inkoom (Dnipro, Ukraine), Daniel Opare (Standard Liege, Belgium), Harrison Afful (Esperance, Tunisia), Richard Kissi Boateng (Berekum Cheslea), Masawudu Alhassan (Genoa, Italy), John Boye (Rennes, France), Lee Addy (Dalian Aerbin, China), Daniel Addo (Arsenal Kyiv, Ukraine) Rashid Sumaila (Dwarfs), Jerry Akaminko (Manisaspor, Turkey), Isaac Vorsah (Hoffenheim, Germany)
Viungo: Anthony Annan (Vitesse Arnhem, Netherlands), Derek Boateng (Dnipro, Ukraine), Emmanuel Agyemang Badu (Udinese ,Italy), Rabiu Mohammed (Evian, France) Richard Mpong (Medema) Albert Adomah (Bristol City, England), Christian Atsu (Rio Ave, Portugal), Ishamel Yartey, (Servette, Switzerland), Sulley Muntari (AC Milan, Italy), Kwadwo Asamoah (Udinese, Italy).
Washambulizi: Jordan Ayew (Marseille, France), Dominic Adiyiah (Arsenal Kyiv, Ukraine), Ben Acheampong (Kotoko), Emmanuel Baffour (New Edubiase), Emmanuel Clottey (Berekum Chelsea)

AKWI SASA DAU LAKE LIMETAJWA KUWA NI MILIONI 500

                                           Emmanuel Okwi

SIMBA imesema ipo tayari kuwauza wachezaji wake, Emmanuel Okwi na Shomari Kapombe katika Klabu ya TP Mazembe huku dau la Okwi likiwa dola 300,000 ambazo ni zaidi ya Sh milioni 500.
Hivi karibuni klabu hiyo ya DR Congo iliripotiwa kuwataka wachezaji hao ambao wameonyesha uwezo mkubwa msimu huu na kuiwezesha Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Bara pamoja na kuifikisha kwenye hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema kwa upande wa Kapombe, dau lake ni Sh milioni 160.
“Sisi bado hatujapata ofa maalum kutoka kwa TP Mazembe lakini wakiileta tupo tayari kuwasikiliza kwa kuwa kama unavyojua tupo kibiashara.
“Kwa upande wa Kapombe wakitoa milioni 160 hakuna tatizo lakini kwa Okwi dau lake ni kuanzia dola 300,000,” alisema Kamwaga.
Iwapo Simba itafanikiwa kuwauza wachezaji hao, itakuwa imefikisha idadi ya wachezaji wanne waliouzwa katika klabu hiyo iliyowahi kutinga fainali ya Klabu Bingwa Dunia lakini ikafungwa na Inter Milan kwa mabao 3-1. Wengine waliouzwa katika klabu hiyo ni Patrick Ochan na Mbwana Samatta walioondoka Msimbazi Julai, mwaka jana.


               
HOMA YAZIDI KUPANDA KWA MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA 

 
kikosi cha simba
ni meshi ambayo inatalajiwa kuwa ngumu mechi itachezwa may 6 2012 katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam
                                                                       
     kikosi cha yang

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.