Ads Top

MAKALA KUHUSU MAENDELEO YA SEKTA YA KILIMO


Mapuli Simon Lukanya : Mkulima anayetarajia Makubwa kupitia  Sekta
ya kilimo.

Na Antony Sollo

Hii ni Makala Maalumu iliyoandaliwa na Mwandishi wa Habari wa gazeti la Tanzania Daima na Mapuli Simon Lukanya Mkulima na mkazi wa Kijiji cha Sanjo Kata ya Usagara Wil.aya ya Misungwi Mkoani Mwanza.

Tanzania Daima ilitembelea shambani kwa mkulima huyo ili kujionea namna Mapuli alivyo na ndoto ya kuwa mkulima mkubwa wa mazao mbalimbali ikiwemo ufugaji wa Nyuki ambapo baada ya kufika katika maeneo ya mkulima huyo yaliyoko katika kitongoji cha Isasabudaga alikutana na Shamba kubwa la mpunga lenye ukubwa wa ekari sita ambazo zimepandwa mpunga,huku ekari tatu zikiwa ni maalumu kwa ajili ya kilimo cha bustani.

Tanzania Daima pia imepata fursa ya kuona shamba lenye ukubwa wa ekari thelathini ambapo katika shamba hilo imepandwa miti aina ya mikaritusi kwa ajili ya utunzaji wa mazingira ambapo miti hiyo itatoa miti aina ya mirunda kwa ajili ya shughuli za ujenzi.

Katika hatua nyingine Mapuli amelieleza Tanzania Daima kuwa,pamoja na kuwa na maeneo yenye ukubwa wa ekari zipatazo arobani ni ekari saba tu ambazo zilipatikana na kufanikiwa kupanda zao la muhogo kwa ajili ya matumizi ya chakula na biashara.

Akizungumza na Tanzania Daima Mapuli alianza kwa kusema.

Mimi kwa jina naitwa Mapuli Simon Lukanya,ni mkaazi wa Kijiji cha Sanjo Kata ya Usagara Wil.aya ya Misungwi Mkoani Mwanza ni mkulima mdogo ambaye nina ndoto ya kupata mafaniki makubwa kutokana na Sekta ya Kilimo.
Nilianza kujishughulisha na shughuli za kilimo nikiwa na ndoto ya kuwa mkulima mkubwa ambapo hadi sasa nimejiendeleza mwenyewe bila msaada wowote toka katika taasisi yoyote ya binafsi au Serikali.

Changamoto.

Kuhusu changamoto anazokumbana nazo Mapuli anasema, moja ya changamoto anazoona kuwa ni kikwazo cha maendeleo yake ni pamoja na Mtaji,zana za kilimo,pamoja na ushauri wa kitaalamu toka kwa wataalamu wa Sekta ya Kilimo pamoja na Mvua.

Katika hatua nyingine Mapuli amewaomba wadau wa maendeleo ikiwemo Serikali pamoja na taasisi binafsi kusaidia namna ya kumpatia Elimu juu ya ukulima wa kisasa pamoja na kumpatia mafunzo ili kukuza uelewa juu ya matumizi mbalimbali ya zana za kilimo pamoja na mabadiliko ya tabia nchi.

Mapuli amewaomba wadau mbalimbali wa masuala ya kilimo ndani na nje ya nchi wajitokeze kwa ajili ya kumpa ushirikiano wa karibu katika masuala ya kifedha,ushauri wa kitaalamu pamoja na uwezeshaji ili aweze kutimiza ndoto yake 

 

Mapuli Simon Lukanya akiwa shambani kwake maeneo ya Sanjo Kata ya Usagara Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza. Picha na Antony Sollo



Mapuli Simon Lukanya akifurahia jinsi mwaka huu unavyoonyesha matumaini kwake baada ya kulima mara kadhaa na kukwamishwa na mvua kama alivyoeleza kuwa moja ya changamoto kubwa kwake ni pamoja na mvua kushindwa kunyesha jambo analoona ni kikwazo kikubwa cha mafanikio yake.Picha na Antony Sollo







No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.