MATUKIO
Serikali yatoa tamko yasema watu 91 wanashikiliwa na polisi kufuatia vurugu za Matwara
Mabasi 5 ya Champion yamebeba Wanajeshi yako njiani yanakuja.
Bunge laahirishwa tena. Kupisha uchunguzi na kuepusha uchochezi kutoka kwa baadhi ya wabunge. (Kwa mujibu wa Spika)
Maeneo ya Magomeni, Chikongola, Nkanaledi, Mikindani maaskari wanaingia majumbani mwa watu na kumsomba mtu yeyote ambaye ni mwanaume awe amehusika awe hajahusika na kumkamata. Pia inaripotiwa na uhalifu unafanywa na maaskari hao hao. Jambo linaloamsha hisia kwa wananchi.
RPC anaongea na vyombo vya habari na kuwasihi wananchi waende makazini. Lakini kiuhalisia hali sio shwari.
Mahakama ya mwanzo ya Mitengo imechomwa moto
Mpaka sasa ni vita baina ya wananchi na maaskari. Mabomu yamesikika pamoja na milio ya risasi masaa 24. Na milio ya Risasi na mabomu inaendelea kusikika.
Raia wapatao 7 wameripotiwa kufariki (wengine walipelekwa hospitali ya Ndanda Ndogo na mmoja ameripotiwa kupokelewa Ligula. Nyumba za viongozi zinaendelea kuchomwa moto. Majibizano baina ya Polisi na Raia yanaendelea maeneo ya Magomeni, Nkanaledi na Mikindani.Maduka yamefungwa na hakuna huduma zozoteBarabara zimewekwa vizuizi magogo na matairi yamechomwa moto. Hakuna njia ya kupita
Maduka maeneo ya Magomeni yamechomwa moto ikiwamo pia mali za Askari magereza na uhalifu ukifanyika vidole vinawaelekea Polisi.
Afisa Usalama wa Taifa ambaye anamiliki nyumba ya wageni naye amevamiwa na kuporwa mali ikiwamo fedha katika gesti yake. Haijajulikana ni kiasi gani cha mali kilichopotea.
Mwanafunzi wa CHUNO afikishwa hospitali Ligula na majeraha ya risasi mguuni.
PICHA ZA VURUGU ZA MTWARA
Gari
ya kubebea wagonjwa Ambulance inaonekana kuteketea kwa moto baada ya
kuchomwa katika vurugu zilizoripotiwa kutokea mara kadhaa mkoani
Mtwara
Magari yanayosemekana kuwa ya Halmashauri yakiwa yamechomwa moto na waanchi wa
.Mtwara
.Mtwara
Majengo yanayotajwa kuwa ofisi zimechomwa moto
Vurugu
hizi zimetokea siku chache baada ya Wizara ya Nishati na Madini kusema
kuwa bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam na
leo hii Wananchi wa Mtwara wacharuka na kuanzisha vurugu!
Tukio hili liliendelea wakati bajeti ya nishati na madini ikiendelea kujadiliwa Bungeni.
Endelea kuwa nasi mpaka hapo baadae ambapo tutaweza kukujuza zaidi kile ambacho kinaendelea kutokea Mtwara.
Fullshangweblog
imewasiliana kwa njia ya simu usiku huu na Kamanda wa polisi wa mkoa wa
Mtwara Kamanda ACP Linus Sinzumwa, hata hivyo ACP Sinzumwa alisema yuko
kwenye kikao hataweza kuongea chochote na kukata simu
TAARIFA za awali zina arifu kuwa Mfanya Biashara, Costa Shirima anaedaiwa kujirusha kutoka gorofa ya tisa ya Hoteli ya Concord iliyopo Kariakoo Jijini Dar es Salaam inaelezwa kuwa alifariki dunia muda mfupi baada ya kujirusha na alikuwa asafiri na ndege ya saa 10 jioni kuelekea China kufuata bidhaa za maduka yake
Shirima (47), ambaye amefikwa na umauti muda mfupi baada ya
kudondoka chini ni mfanyabiashara aliyekuwa akimiliki maduka kadhaa ya
urembo wa akina mama yaliyopo jirani na Hoteli hiyo ya Concord.
Aidha taarifa hizo za awali kutoka kwa mmoja wa wanafamilia ambaye
alidai kuwa si msemaji wa familia ya Shirima ya Mwika Moshi mkoani
Kilimanjaro, nikuwa Marehemu mara kwamara alikuwa akipendelea kula
katika hoteli hiyo na siku ya tukio inadaiwa kuwa aliwaeleza watu kuwa
anapanda juu ya Hoteli hiyo kupunga upepo baada ya kuhisi hewa nzito
mahali alipokuwa.
Inadaiwa kuwa baada ya kupanda huko juu ghafla alianguka chini na
kudondokea gari dogo aina ya Toyota Corola linalofanya biashara ya Taxi
na kupoteza maisha yake na gari hilo kuharibika vibaya kutokana na
kishindo hicho.
Marehemu Shirima mbali na kuwa Mfanya Biashara wa muda mrefu
Kariakoo pia alikuwa akiendelea na Ujenzi wa Jengo la Gorofa maeneo ya
Kariakoo.
Marehemu ameacha Mjane na watoto
Majambazi
yapora mama mmoja kiasi cha shilingi milioni kumi muda mchache uliopita
na kutokomea kusikojulikana. Tukio hilo limetokea leo saa 11 jioni
inavyosemekana mdada huyo alikua akitoka benki ya CRDB tawi la
Uhuru ambapo majambazi yakiwa na pikipiki yalikua yakimfuatilia, alipotoka tu wakaligonga gari lake makusudi ndipo dada huyo
aliposimama ili angaalie nani kagonga gari yake ambapo jambazi mmoja alishuka na kumpiga risasi ya kifuani na kutokomea na kiasi hicho cha pesa.
Uhuru ambapo majambazi yakiwa na pikipiki yalikua yakimfuatilia, alipotoka tu wakaligonga gari lake makusudi ndipo dada huyo
aliposimama ili angaalie nani kagonga gari yake ambapo jambazi mmoja alishuka na kumpiga risasi ya kifuani na kutokomea na kiasi hicho cha pesa.
TUKIO LA MLIPUKO WA BOMU KATIKA KANISA KATOLIKI HUKO ARUSHA
Mmoja wa majeruhi akifikishwa hospitali
Hali ya eneo mlipuko ulipotokea
Waumini na wananchi wengine wakiwa na shauku ya kujua kilichotokea
Waumini na wananchi wengine wakiwa na shauku ya kujua kilichotokea
Ulinzi umeimarishwa
Viongozi wa Kanisa wakitoa taarifa ya kilichotokea kwa waandishi wa
habari kabla ya Balozi wa Papa kuondolewa Kanisani hapo chini ya ulinzi
mkali wa Polisi.
Wanasualama Mkoa wa Arusha, wakijadiliana jambo katika eneo la tukio
Meya wa Manispaa ya Arusha, Mh gaundence Lyimo akielekea eneo la tukio kwa miguu baada ya utaratibu wa kutumia magari kuwa mgumu kutokana na idadi kubwa ya watu na magari yaliyoziba njia.
Meya wa Manispaa ya Arusha, Mh gaundence Lyimo akielekea eneo la tukio kwa miguu baada ya utaratibu wa kutumia magari kuwa mgumu kutokana na idadi kubwa ya watu na magari yaliyoziba njia.
Magesa Mulongo akiteta na RCO wa Mkoa wa Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, magesa Mulongo akijiandaa kuzungumza na
wananchi kanisani hapo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha watu wote
waliohusika na jaribio hilo ovu, pamoja na mtandao wao wanakamatwa.
Alidai pia vikosi vya Jeshi maalumu kwa kuchunguza milipuko vitafika
eneo hilo ili kufanya uchunguzi. Taarifa za eneo la tukio zinaeleza kuwa
tayari kuna mshukiwa mmoja ameshatiwa mbaroni na yuko mikononi mwa
Jeshi la Polisi kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.
Eneo lenye utepe ndipo kitu hicho kinachodhaniwa kuwa bomu
kilipoangukia. Pichani unaweza kuona wigi za kichwani na viatu vya
waumini vikiwa vimesambaa baada ya wenyewe kuviacha, miongoni mwao
wakiwa ni majeruhi.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akizungumza na mmoja wa
mapadri wa Kanisa hilo kupewa maelezo ya kuhusu kilichotokea kanisani
hapo.
Mwanamke alioa WAUME wawili
MWANAMKE mkazi wa kijiji cha Ikandamoyo, wilayani hapa, Veronica Saleh ‘Mama Kaela’ (50), amefanya uamuzi adimu wa kuolewa na wanaume wawili ambao anaishi nao kijijini hapo.
Kijiji hicho kipo umbali wa takribani kilometa 30 kutoka mjini hapa katika Jimbo la Katavi linalowakilishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Pamoja na ndoa hiyo iliyowezeshwa na mume mkubwa kukubali kuishi na mume mdogo, imeelezwa kuwa mwanamke huyo ndiye ‘aliyewaoa’ wanaume hao kwa zaidi ya miaka saba sasa, huku akiwa na amri kuu katika nyumba, kama ilivyo katika ndoa za kawaida.
Wanaume hao ni Paulo Sabuni ‘Baba Kaela’ (60) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele (45) ambaye ni mume mdogo.
Taarifa za kuwapo kwa ndoa hiyo ya aina yake, zililifikia gazeti hili na kufanyiwa uchunguzi kwa zaidi ya wiki tatu, na hatimaye katikati ya wiki hii, wahusika walikubali wao wenyewe kuzungumzia suala hilo. Kwa mujibu wa maelezo ya mwanamke huyo ambaye alionekana kuwa msemaji wa familia hiyo, yeye na mumewe mkubwa, walifika kijijini hapo miaka 24 iliyopita, wakitoka kijiji cha Usumbwa mpakani mwa Chunya, Mbeya na Tabora.
Wakiwa kijijini hapo mume wake aliendelea kufanya kazi ya ukulima wakati yeye mama (Veronica), pamoja na kilimo hujihusisha na upishi na uuzaji wa pombe ya kienyeji ya iitwayo kayoga.
Mwanamke huyo ambaye amesema ana watoto wanne, Alfred (20), binti mwenye miaka 16 (ambaye ameolewa) na wengine wawili wa kiume, mmoja akisoma darasa la sita na mdogo ana miaka saba, amesema hana shida na waume wake.
Ingawa wanandoa hao walizungumza kwa hadhari, majirani walikiri kuwa mwanamke huyo anaishi na wanaume hao wawili kwa amani na kwamba mwanamke huyo ndiye mwenye sauti na si waume zake.
“Si siri tena sasa, tumeshawazoea, kwani wanaishi kwa amani ila yule mume mdogo anaishi kwenye nyumba aliyoachiwa na marehemu baba yake, lakini anashinda kwa mume mkubwa, ambapo inajulikana kijijini hapa kuwa ni nyumba kubwa. “Basi pale ni mambo yote, kula na kunywa, mama huyu amewapangia zamu wanaume hao kama afanyavyo mume mwenye wake wengi. Ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni,” alisema mkazi mmoja kwa masharti ya jina lake kutoandikwa gazetini. Ilielezwa, kwamba wanaume hao wana akili timamu na hawatumii kilevi cha pombe kama ilivyo kwa mke wao.
Hata hivyo, mume mkubwa anapewa sifa za upole tofauti na mume mdogo anayetajwa kuwa mkorofi kiasi cha mara kadhaa kumchapa makofi mkewe anapomuudhi.
Majirani wanadai kwamba Mama Kaela na mumewe Paulo, walipofika kijijini hapo, walipokewa na kuishi maisha ya kawaida, lakini baadaye mama huyo alianza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Arcado, ambaye naye alilazimika kuachana na mkewe wa ndoa anayefahamika kijijini hapo kwa jina la Mama Pere.
Ilielezwa na mashuhuda hao kwamba mume mkubwa alipobaini uhusiano huo, alikuja juu, lakini mwanamke huyo inadaiwa alimweleza mumewe huyo, atake asitake lazima wataishi wawili, vinginevyo ataachana naye, ndipo mume mkubwa alipokubali kuishi na mume mwenza.
Katika maisha ya kawaida katika familia hiyo, inaelezwa kwamba katika baadhi ya siku ikitokea kuwa mama huyo amechoka kupika, mume mdogo huchukua jukumu la kupika na kumwandalia chakula na maji ya kuoga mume mkubwa.
“Lakini mara nyingi kwa mfano, ikiwa ni zamu ya mama huyo kulala kwa mumewe mkubwa, basi humfulia nguo zake kisha anakwenda kwa mumewe mdogo nako anamfulia nguo.
“Ndivyo wanavyoishi, nasi sasa tumewazoea ila yule mama ni mkali na ana sauti pale kwake kwa wanaume wale ila tunaona kama ana wivu sana kwa huyu mdogo ambaye naye pia ana wivu kwa mkewe huyo, labda anahofia kuwa mama huyo anaweza kuongeza mwanamume mwingine,” anasema mmoja wa majirani hao.
Hakuna mazuri yasiyokuwa na machungu, japo familia hiyo inaelezwa kuwa na amani, mtoto wao mdogo nusura avuruge uhusiano wa wanandoa hao, baada ya kuibuka mzozo wakati wa maandalizi ya ubatizo wake.
Kwa sababu anazojua mama, ingawa inafahamika kuwa wote ni watoto wa mume mkubwa, mke huyo katika hati za ubatizo aliandikisha ubini wa mtoto huyo kuwa ni Mlele (akimaanisha kuwa mtoto wa mume mdogo), lakini mume mkubwa aliweka pingamizi kanisani akidai yeye ndiye baba halali wa mtoto huyo.
Kwa mujibu wa mwanamke huyo, yeye na Arcado ni waumini wa madhehebu ya Katoliki wakati Paulo ni Mpentekoste. Madai ya mzozo wa uhalali wa `ubaba’ wa mtoto huyo, yalithibitishwa na baadhi ya wakazi wa kijiji hicho, akiwamo mwalimu wa dini wa Kigango cha Kanisa Katoliki Uruira, Mashaka Abel. Walisema miaka sita iliyopita, mtoto huyo akiwa na umri wa mwaka mmoja, alifanyiwa taratibu za ubatizo, lakini ilishindikana, kutokana na wanaume hao, kila mmoja kudai ndiye baba mzazi wa mtoto.
“Lilikuwa jambo la kustaajabisha sana, kwani familia hiyo ilifanya maandalizi yote ya sherehe ya ubatizo wa mtoto huyo, lakini siku hiyo kanisani wakati huo ilikuwa ni kigango cha Katumba ambacho sasa ni Uruira, sakata lilianzia pale Padri alipomwuliza mama wa mtoto huyo ubini wa mtoto naye akasema ni Mlele.
“Hapo ndipo mume mkubwa alipopinga na kudai kuwa mtoto yule si wa Arcado bali wake na yeye ndiye baba halali. Padri hakuamini, aliuliza tena na tena na majibu yakawa ni yale yale, ndipo ubatizo ukashindikana,” alisema Katekista Abel.
Kazi ya kutafuta undani wa ndoa hiyo haikuwa rahisi kutokana na mazingira ya woga na usiri uliokusudiwa kubaki, ambapo awali mama alisema kwamba mume wake ni Paulo pekee japo siku ambayo mwandishi wa habari hizi alifika kijijini hapo na baadaye nyumbani kwa wanandoa hao na kumkuta mume mdogo (Arcado akimsaidia mkewe kukoroga pombe. Awali katika utambulisho, walidai kuwa ni mtu na mdogo wake na kusita kuzungumzia maisha yao ya kifamilia.
Mke wao ambaye alionekana wazi kuwa ni msemaji mkuu alifoka na kuja juu, akidai kuwa hayuko tayari kuzungumzia uhusiano wake na wanaume hao wawili, ingawa alikiri kuwa wanaishi pamoja.
"Kwa hiyo umefunga safari yote hii kutoka huko ulikotoka ili uje kwangu mie Veronica … nasema sitaki kabisa mtu kuja hapa na kutaka kunivurugia mpangilio wa maisha yangu, kwanza nani alikueleza hayo, wambea wakubwa hao yanawahusu nini watu hao?” alihoji.
“Mie mume wangu ni huyu Paulo basi … sasa leo umeniachia vurugu ndani ya nyumba nitapigwa na huyo mume wangu Paulo, kwani mmenishikisha ugoni?” alifoka Mama Kaela. Hata hivyo, mume mkubwa alidai kuwa hatamwadhibu mkewe huyo na kwamba wataendelea kuishi pamoja na mdogo wake Arcado kwa amani. Hata hivyo, akina mama wengi kijijini hapo wanalaani kitendo cha mama huyo kuishi na wanaume wawili ambapo waliomba uongozi wa Kanisa uingilie kati, ili mama huyo aweze kufunga ndoa na mume mmoja.
Lakini kwa upande mwingine, baadhi walimpongeza mwanamke huyo wakidai kuwa kitendo hicho ni cha kijasiri kwa mwanamke, kumudu kuishi na wanaume wawili na kuwa na mamlaka juu yao
HUU NI UNYAMA WA KUTISHA IRINGA ,KIJANA ACHOMWA KISU UTUMBO WATOKA NJE ,
mpenzi mdau wa mtandao huu kwanza naomba radhi kwa picha hizi za kusikitisha ila ndio hali halisi ya mambo inatisha sana
Kijana kizito Kimeya (28) mkazi wa kijiji cha Mkoga kata ya Isakalilo Manispaa ya Iringa akiwa Hospitali ya mkoa wa Iringa kupatiwa matibabu baada ya kuchomwa kisu na utumbo wake kutoka nje
Miguu ikiwa imekatwa katwa mapanga na wauwaji hao ambao hawakufanikiwa kutimiza azmayao
hapa utombo ukiwa nje baada ya kuokolewa na afisa mtendaji wa kata hiyo ya Isakalilo Iringa mjini
Ni vigumu kuamini kama kweli kuna binadamu na wanywa damu ila kutokana na matukio kama hayo ndipo unaweza kuamini kuwa wapo binadamu na wanywa damu baada ya watu wanne ambao majina yao yametajwa na kijana huyo kudaiwa kumchoma visu kijana huyo pichani baada ya kumfuma akiiba mahindi ya mabichi maarufu kama Gobo katika shamba lao Kijana huyo alichomwa kisu na kucharangwa mapanga na baada ya wahusika kutenda unyama huo walimchukua na kumweka katika mfuko wa sarufeti na kujaza mchanga na kisha kumtupa mtoni kabla ya na kusindwa katika maji kwa masaa zaidi ya matano na baadae maji kusaidia kuupasua mfuko huo na mchanga wote kumwagika na kijana huyo kujisaidia kujikokota hadi nje kavu na kukutwa porini siku ya pili yake majira ya saa 1 usiku na wasamaria wema.
AJALI MBAYA YATOKEA WATU WAWILI WAPOTEZA MAISHA BAADA YA KUGONGWA NA LORI
ni ajari mbaya yawapata jamaa hawa hatimae kupoteza maisha ni dreva wa pikipiki na abilia wake wamepata ajali kwa kugongwa na loli
NJIA LAHISI YA KUPUNGUZA VIBAKA MTAANI
kibaka auwawa na wananchi wennye hasila kali
mfanya biashara ndogondogo wa chalinze akicomlewa katika taili la lori
Wananchi wakiwa wamemzunguka kijana aliyenusurika kufa baada ya kuchomolewa uvunguni mwa lori mjini Chalinze.
Akiwa amekaa chini kwa maumivu.
Akisaidiwa na Askari wa usarama barabarani (Trafiki)
Baadhi ya watu wakiwa wanaliangalia Lori hilo huku wakiwa hawaani kama kijana huyo amenusurika kufa.
Mfanyabiashara ndogo ndogo wa Chalinze mjini ambaye jina lake halikuweza kupatikana jana alipasuka kichwani na kunusurika kufa baada ya kuchomolewa katika taili la Lori ambalo linafanya shughuri ya kutengeneza barabara,
Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa saba mchana stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani karibu na njia panda ya kwenda Tanga na Morogoro mjini Chalinze wakati kijana huyo alipo kuwa akijalibu kuvuka barabara kubwa ndipo alipotokewa na tukio hilo.
Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa saba mchana stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani karibu na njia panda ya kwenda Tanga na Morogoro mjini Chalinze wakati kijana huyo alipo kuwa akijalibu kuvuka barabara kubwa ndipo alipotokewa na tukio hilo.