Ads Top

SERIKALI YAONYA WAKURUGENZI KUKAIMISHA WAKUU WA IDARA

Na Antony Sollo Biharamulo.

Serikali imetoa onyo kali kwa Wakurugenzi wa Halmashauri nchini
kutokaimisha wakuu wa Idara kwa zaidi ya miezi sita na kuonya kuwa Mkurugenzi atakayekaidi agizo hilo atachukuliwa hatua kali.

Akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi Mary Mwanjelwa amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri nchini  kutokaimisha  nafasi katika idara mbalimbali kwa zaidi ya miezi sita  vinginevyo hatua kali zitachukuliwa  kwa atakayekaidi agizo hilo.

Bi Mwanjelwa alisema kuwa Serikali imeshatoa waraka kwa Wakurugenzi nchini juu ya agizo la kutomkaimisha ukuu  wa idara kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita bila  kupandishwa daraja kushika nafasi hiyo vinginvyo  Mkurugenzi anapaswa kujieleza  kabla ya kuwajibishwa kwa kushindwa kutii agizo la serikali. 

Serikali imeshatoa waraka kwa Wakurugenzi  nchini juu ya agizo la kutomkaimisha ukuu  wa idara kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita bila  kupandishwa daraja kushika nafasi hiyo vinginvyo  Mkurugenzi anapaswa kujieleza  kabla ya kuwajibishwa kwa kushindwa kutii agizo la serikali “Serikali ilishatoa waraka kwa Wakurugenzi  wa Halmashauri nchini juu ya agizo la kutomkaimisha ukuu  wa idara kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita bila  kupandishwa daraja kushika nafasi hiyo vinginvyo Mkurugenzi atapaswa kujieleza  kabla ya kuwajibishwa kwa kushindwa kutii agizo la serikali”alisema Mwanjelwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo  Bi Wende  Ng`ahala  alisema agizo hilo limeshaanza kutekelezwa   baada ya kukaa kikao Maalumu cha baraza la Madiwani  hivi karibuni  kwa lengo la kupitisha wakuu wa idara walio na sifa za kuwa wakuu wa idara kamili.

“Agizo hilo limeshaanza kutekelezwa   baada ya kukaa kikao Maalumu cha baraza la Madiwani  hivi karibuni  kwa lengo la kupitisha wakuu wa idara walio na sifa za kuwa wakuu wa idara kamili”alisema Ng`ahala.

Bi Mwanjelwa anaendelea na ziara yake Mkoani Kagera kwa kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na TASAF Wilayani humo ambapo alitembelea makundi ya walengwa katika Kata za Katoke na Lusahunga ili kujionea namna ambavyo wananchi wamenufaika na fedha hizo.

Akitoa taarifa kwa Naibu waziri Mratibu wa TASAF Wilaya ya Biharamulo Bwana Wanna  Nyagarogoro  alisema zaidi ya Shilingi mil 66,833,72 zimetumika katika Mpango wa kunusulu kaya maskini katika Kata ya Nyarubungo Kijiji cha Katoke huku Kata ya Lusahunga ikitumia zaidi ya Sh Mil 160,962,813.65 na kuongeza kuwa fedha hizo zimeleta mabadiliko chanya kwenye jamii katika kuboresha huduma za Elimu,mavazi,chakula na Bima ya Afya.

Bi Mwanjelwa alisema kuwa katika kuboresha huduma na kudhibiti fedha hizo Serikali ina mpango wa kuwaingizia walengwa wa mpango huo fedha kwa njia ya MPESA na kuwataka wataalamu kuwaongoza walengwa kufanya kazi zenye ubora ili kuwa na matokeo chanya pia serikali inatarajia kuanza mchakato wa kuingiza walengwa wapya ili kuhakikisha wale ambao hawakuhaulisha kutokana na vijiji vyao kutokuingizwa katikam mpango huo  waweze kunufaika  na mpango huo.

MWISHO

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.