Ads Top

RC GABRIEL FEDHA ZA UMMA ZIKO SALAMA

Na Antony Sollo Geita

MKUU wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel amesema kuwa fedha zinazotolewa na Serikali kwa sasa ziko salama na kusisitiza kuwa biashara ya upigaji dili kwa fedha za umma, ubabaishaji kwa sasa havina nafasi katika mkoa wake na kwamba Geita ni mkoa salama kwa fedha za umma

Mkuu Huyo wa Mkoa ameyasema hayo jana mjini Geita wakati akimkaribisha Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk Harrison Mwakyembe wakati alipokuwa akitoa taarifa ya maendeleo ya mkoa kuhusiana na sahughuli mbalimbali za maendeleo ya mkoa na uwekezaji

Gabriel alisema kabla hajahamishiwa mkoani Geita akitokea mkoani Tanga, aliikuta Geita ikiwa imesheheni wapiga dili na watu wanaotumia fedha za umma vibaya na kuonya kuwa kwa sasa watumishi wa aina hiyo hawana nafasi kwenye uongozi wake

Akitolea mfano wa matumizi mabaya ya fedha za umma, alisema kuanzia mwaka huu alibaini  kiasi cha fedha Sh bilioni 55 zikiwa zimetumika vibaya katika ujenzi wa vyumba vya madarasa vya shule ya msingi Nyakumbu majengo ambayo hayaendani na fedha zilizotumika

Mhandisi Gabriel alisema “ Mimi nashangaa watu wa Mungu wanomba makanisani Mungu atupe utajiri, wakati tayari Mungu alishatoa utajiri kwa watu wa mkoa wa Geita, sasa niwashauri waombe Mungu ili kukamata wezi na mafisadi Geita”,

Aliongeza kuwa mkoa wa Geita ni mkoa uliobarikiwa na kuomba kuwa   takwimu za kiuchumi zinazotolewa kuhusu uchumi wa mikoa mbalimbali kitaifa na kimataifa zinatakiwa zipitiwe upya ili kutoa hali halisi kwamba Geita ndiyo mkoa unaoongoza kwa kuzalisha dhahabu kwa wingi kuliko mkoa wowote hapa nchini

Mhandisi huyo alisema kuwa kwa ushirikiano wa Serikali na Kampuni ya magazeti ya Serikali (TSN) wamebaini kuwa mkoa wa Geita una fursa nyingi za kiuchumi ambazo zilikuwa hazijawekwa bayana kwa umma na wawekezaji wa ndani na nje , hivyo kuwaomba wandishi wa habari kumpatia ushirikiano kwa kutangaza fursa za kiuchumi zilizopo kwa manufaa mapana ya maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk Avemaria Semakafu  alisema kuwa amefarijika na mabadiliko ya utendaji yalyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Gabriel na kushauri Chuo cha Veta kinachojengwa mkoani Geita kichikite katika kutoa taaluma inayohusu uchimbaji, uchakataji wa raslimali zilizo katika mkoa wa Geita hasa madini, samaki na asali

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali Dk Hassan Abbas alisema kuwa kitengo chake kitaunga mkono kwa dhati juhudi znazofanywa na Mkuu wa mkoa wa Geita katika kuwaletea wananchi maendeleo ili zifahamike vyema kwa umma na kuifanya Geita kuwa kitovu cha dhahabu nchini

Dk Abbas alisema katika kufanikisha azma hiyo, .atatuma timu tatu za wandish.i wa habari kutoka TBC,.Idara ya Habari Maelezo na .Kampuni ya  magazeti ya serikali kwa madai kuwa teknolojia kwa sasa imebadilika hivyo ni vyema kutumia teknojia ya habari kutoka kwenye vyombo hivyo vya umma.

“ Mimi Mkuu wa mkoa nitakuunga mkono kwa kukuletea timu tatu, ya anga, majini na nchi kutoka kwenye vyombo vya serikali, nikimaanisha anga ni TBC, majini ni Idara ya Habari Maelezo na Nchi kavu ni vyombo vya magazeti ya umma –TSN”, alisema.

Kwa upande wake Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk Harrison Mwakyembe alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Geita kwa utendaji kazi uliotukuka na kuuomba uongozi wa TSN kuendelea kuwaruhusu wandishi wa habari kutoa ushirikiano kwa serikali kuendelea kuandika na kutangaza habari za ukweli juu ya fursa za kichumi zilizopo mkoani Geita.

“ Taarifa hii uliyoitoa leo Mkuu wa mkoa ni ya aina yake, nimetembea mikoa mingi lakini sijawahi kuona uwasilishaji wa taarifa ya namna, ni taarifa iliyosheheni weledi mkubwa isiyotiliwa shaka na inayoaminika, hongera sana”, alisema Dk Mwakyembe

Kuhusu kusitishwa kwa chaneli za umma zlizokuwa zinarusha matangazo yake kupitia visumbusi vya Azama, DSTV na Zuku alisema kuwa kuna upotoshaji kwa umma unaosambazwa kupitia mitandao ya kijamii kwamba serikali haitaki wananchi wake wapate taarifa kupitia visumbusi hivyo, jambo ambalo alisema halina ukweli wowote.

“ Ukweli ni kwamba, vyombo hivyo vilikiuka sheria ya kurusha matangazo kinyume na usajili, na sisi kama serikali tulikuwa hatujazungumzia jambo kwakuwa wamiliki wa visumbusi hivyo walipeleka shauri mahakamani, na kwakuwa sasa tumeshinda tumechukua hatua stahiki ya kuzuia wizi kwani, walipaswa kuonyesha taarifa zao bure na sio kuwaibia wananchi kama walivyokuwa wanafanya”, alisema

MWISHO

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.