Ads Top

POLISI YANASA KUMI NA NANE ZIWA VICTORIA

Na Antony Sollo Mwanza

JESHI la polisi Mkoani Mwanza liwanashikilia watu kumi na nane (18 kwa makosa mabalimbali ya kiuhalifu katika operesheni maalumu iliyofanyika Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza na katika maeneo  mbalimbali ya Ziwa Victoria.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza DCP: Ahmed Msangi imeeleza kuwa,Operesheni hiyo ilianza August 02.08.2018 hadi tarehe 03.08.2018 katika maeneo mbalimbali ya ndani ya ziwa Victoria na katika vijiji vilivyopo pembezoni mwa ziwa hilo wilayani Sengerema Mkoani Mwanza.

Operesheni hiyo maalumu ilishirikisha kikosi maalumu cha askari polisi Mkoa, Polisi Wanamaji (Police Marine) pamoja na Askari polisi toka Wilaya ya Sengerema kilichoongozwa na Operesheni Afisa Mkoa wa Mwanza SSP: Audax Majaliwa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Sengerema SSP: Mairi Wassaga na kufanikiwa kukamata watuhumiwa kumi na nane (18) wa makosa mbalimbali ambayo ni pamoja na  kupatikana na samaki wachanga kilo 125, kupatikana na nyavu haramu hamsini (50) za kuvulia samaki aina ya timba na kupatikana na bangi kilo mbili (2)pamoja na kupatikana na pombe ya moshi (gongo) lita 265, kupatikana na pikipiki moja izaniwayo kuwa ya wizi yenye namba MC 242 BDK na nyavu haramu 600 za kuvulia dagaa.

Imeelezwa kuwa kabla ya zoezi hilo jeshi la polisi walipokea taarifa toka kwa raia wema kwamba katika baadhi ya maeneo ya vijijini, pembezoni mwa ziwa Victoria na baadhi ya visiwa vilivyopo Wilayani Sengerema kulikuwa na watu waliokuwa wakijihusisha na biashara haramu ya pombe aina ya gongo, uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya aina ya bangi, wizi wa vitu mbalimbali, uvuvi wa kutumia nyavu haramu makokoro, uvuvi wa samaki wachanga na vitendo vingine vya kiuhalifu.

Baada ya kupatikana kwa taarifa hizo kuliandaliwa kikosi kazi Maalumu cha Askari polisi Mkoa kilichoshirikiana na polisi wanamaji mwanza na askari polisi toka Wilaya Sengerema hivyo msako mkali ulifanywa kwa pamoja katika maeneo yote ya majini na nchi kavu na baadae askari waliweza kufanikiwa kukamata wahalifu kumi na nane wa makosa mbalimbali.

Mpaka sasa Jeshi la Polisi lipo katika upelelezi na mahojiano na watuhumiwa wote, ili kuweza kuwabaini wale wote wanaoishirikiana  nao kwa namna moja au nyingine katika kutenda uhalifu huo ambapo Kamanda Msangi amesema kuwa uchunguzi ukikamilika watuhumiwa wote kumi na nane watafikishwa Mahakamani.

Vilevile msako mkali wa kuwatafuta watu wanaojihusisha na uhalifu wa aina kama hii katika maeneo yote ya jiji na Mkoa wa Mwanza bado unaendelea ambapo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishina wa Polisi Ahmed Msangi ametoa wito kwa wakazi wa Jiji na Mkoa wa Mwanza kuacha tabia ya kujihusisha na uhalifu kwani utawaletea matatizo na baadae kufungwa na kupelekea kutengana na familia huku akiwataka kufanya halali zitakazoweza kuwaingizia kipato sambamba na hilo Msangi amewaomba wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu mapema ili waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo vya Sheria.

MWISHO

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.