Ads Top

VIJANA TUNAMAONI GANI? KUHUSU KUELEKEA KUPATA KATIBA MPYA

KATIBA IJAYO IANGALIE SUALA HILI
BAADHI YA WABUNGE KUJIINGIZA KATIKA BIASHARA NI CHANZO CHA KUPANDA KWA  GHARAMA ZA MAISHA YA WATANZANIA.
Kupanda kwa gharama za maisha kwa wananchi wa tanzania ni tatizo linaloitafuna nchi hii kwa kasi kubwa kuliko wakati wowote tangu kung’atuka kwa muasisi wa taifa hili hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere ambapo katika kipindi hiki zimejitokeza dosari kubwa kwa kasi kubwa kwa kuwa na matabaka katika nchi na kusababisha makundi ya walionacho na wasionacho kuwa kubwa kupindukia.
Hali hii ikiendelea kukumbatiwa Taifa linakwenda kupoteza mwelekeo na kuwa nyumba ya kujifichia watu wasio na nia nzuri jambo ambalo litasababisha wananchi hasa walio na kipato cha chini kuendelea kuichukia Serikali na matokeo yake kusababisha kuvunjika kwa amani.
Nilichojifunza kuwa hali hii inasababishwa na viongozi wetu ni pale kulipotokea tatizo la mafuta ,tulishuhudia jinsi Bunge letu lilivyokuwa na watu ambao walikuwa hawawezi kuchukua hatua yoyote kwa vile baadhi yao ni wadau wa biashara ya mafuta kwa kushirikiana na watu mbalimbali na kama kweli wasingekuwa ni washirika wangechukua hatua za haraka kudhibiti tatizo hilo la upandishaji wa bei ya mafuta.
Nashindwa kuelewa kwa nini kipindi cha utawala wa awamu ya kwanza kulikuwa hakuna viongozi wa serikali kujiingiza katika biashara kama ilivyo sasa hivi ambapo hali hii ni mbaya ukizingatia hata Bunge letu limesheheni wabunge wafanya biashara na wasio na uzalendo  kuliko kipindi cha awamu ya kwanza angalia wabunge wetu pamoja na viongozi wa serikali wanavyofanya biashara ndani ya ofisi za serikali na jinsi pia hata baadhi ya wabunge wetu wanavyoshabikia uozo katika mashirika na taasisi za serikali ni aibu na ni fedheha kwa serikali kuwa na watendaji wasio na uzalendo kiasi hiki.
Binafsi kupanda kwa bei ya vyakula,gharama za usafiri,pamoja na mambo mengine kunatokana na viongozi wa serikali pamoja na baadhi ya wabunge kujiingiza katika biashara na ili iwe si luhusa kwa viongozi kujihusisha na biashara kama ilivyokuwa katika kipindi cha awamu ya kwanza ni lazima sasa katiba ijayo ni lazima iweke wazi ushiriki wa wawakilishi [wabunge] na biashara iwe ni mwiko kwa viongozi kujihusisha na biashara aina yoyote kwa vile huwezi kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja.
Ipo mifano mingi inayoonyesha jinsi watu wanavyotumia gharama kubwa kuingia bungeni mimi huwa najiuliza hivi hawa watu watazirudishaje gharama hizo kwani bungeni kuna biashara gani mpaka mtu atumie gharama kubwa kiasi hicho.
Utaona mtu anaweka rehani mpaka nyumba ya milioni miambili ,lengo  kwenda bungeni je kuna nini huko?
Hivi gharama za kutetea wananchi zinakuwa kubwa kiasi hicho ? ni utetezi kweli au ni kutetea tumbo?
Kwa maoni yangu katiba ijayo watumishi wa serikali wakiwamo wabunge iwe ni mwiko kujiingiza katika biashara yoyote.
  Mwandishi wa makala hii ni mwanaharakati na mtetezi wa Haki za Binadamu 
Mr Antony Sollo
antonyjilala@yahoo.com:0787565533

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.