Ads Top

TAARIFA YA MAUAJI YA KINYAMA KATIKA KIJIJI CHA MSOWELO WILAYANI KILOSA –MKOANI MOROGORO.

PICHA ZA MABAKI NA MAZISHI YA MAREHEMU JOSEPH MACHOKAA
mahali ambapo alikuwa ametupwa
wakati wa mazishi yake

baadhi ya wakina mama wakiomboleza
watoto wa marehem
Mheshimwa, M/Kiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninayo heshima kuleta taarifa ya mauaji ya kinyama yaliyofanyika tarehe 09/03/2012, katika kijiji cha Msowelo huko wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

Mheshimiwa M/Kiti, kabla ya kueleza kwa kina lengo la waraka huu napenda kuitambulisha Asasi hii kama ifuatavyo:

Asasi hii ya Shinyanga Nguvukazi Development Foundation [SNDF] imesajiliwa septemba 2011 kwa mujibu wa sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali ya mwaka 2002, na kupatiwa  cheti cha usajili namba 00NGO/00004985, na inafanya shughuli zake kwa ngazi ya Kitaifa

Baada ya kusajiliwa, Asasi hii ilijiunga uanachama katika kituo cha sheria na haki za binadamu [LHRC] na kwa mantiki hiyo asasi hii inatarajia kuzindua Dawati la Sheria Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kusaidia jamii katika masuala ya kisheria ikiwemo kutatua migogoro mbalimbali kwa njia ya amani na Asasi hii inatarajia kupanua wigo wa shughuli zake katika sehemu mbalimbali kwa kadri uwezo utakapopatikana.

Mh. M/Kiti naomba kuwasilisha kwa masikitiko makubwa taarifa ya kuuawa kwa mwananchi mmoja mkazi wa kijiji cha Msowelo Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro Ndugu Joseph Machokaa ambaye aliuawa tarehe 09/03/2012 huko Msowelo.

Mh. M/Kiti, naelewa kuwa Serikali yetu ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania inaheshimu na inathamini sana haki za binadamu na ndiyo sababu kubwa iliyopelekea Viongozi wetu kusaini mkataba wa kimataifa wa kulinda na kudumisha haki za Binadamu kwa raia.

Mh. M/Kiti kilichotokea Msowelo ni kinyume kabisa na matarajio ya wengi na imedhihirisha wazi udhaifu wa baadhi ya viongozi wa Serikali katika kusimamia matatizo ya wananchi, ni aibu! Ni fedheha, na ni ukiukwaji wa Sheria na haki za binadamu!

Baadhi ya taasisi za Serikali zimethibitisha jinsi ambavyo haziko tayari kusikiliza matatizo ya Wananchi na kuyatatua kwa kufuata misingi ya Sheria kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, kwani wapo Mahakimu wa Mahakama mbalimbali, Watumishi wa Jeshi la Polisi na idara mabalimbali za Serikali ambao nao kazi zao zinatekelezwa kwa matakwa ya mtu apendavyo.

Kwa mantiki hii, napenda kukufahamisha wewe, pamoja na kamati yako tukufu ya ulinzi na usalama juu ya matatizo yaliyotokea kwa wananchi wa kijiji cha Msowelo kushindwa kuripoti tukio la mauaji muda wa siku takribani 29 tangu mwananchi huyo auawe kinyama akitoka kwenye vyombo vya Sheria kudai haki yake.

Kwa kuwa  mahusiano kati ya Jeshi la Polisi Wilaya ya Kilosa na wananchi ni mabaya, wananchi hao wamekaa kimya bila kutoa taarifa za mauaji hayo na kupelekea mwananchi huyo mwili wake kuliwa na  wanyama na kubakia mifupa, wakati tayari walikuwa wakijua ni nini kilichotokea dhidi ya marehemu JOSEPH MACHOKAA ambapo marehemu alikuwa akifuatilia  majibu ya barua aliyokuwa amemwandikia Hakimu wa Mahakama ya Msowelo kwa kesi namba 205 ya mwaka 2010, alipofika Mahakamani marehemu aliulizia majibu yake lakini kukatokea kutoelewana na Mheshimiwa Hakimu pamoja na Mlalamikaji baada ya marehemu kuhoji na wahusika kushindwa kueleza viliko vielelezo vya kesi hiyo jambo lililopelekea mzozo, hivyo  hakimu huyo alimtishia maisha Marehemu kwa maneno kuwa nanukuu “umenishtaki kwa msajili wa Mahakama kuu na kwa Hakimu wa wilaya, “utaona matokeo yake”,

Baada ya marehemu kutoka tu mahakamani alikuja kutoa taarifa za vitisho hivyo kwa mtu aliyekuwa karibu naye ikiwa ni tahadhari kwa yale yaliyosemwa endapo yangetekelezwa kumbe kweli yakatekelezwa ambaye amejitambulisha kwangu siku ya mazishi .

Mheshimiwa mwenyekiti mimi nikiwa Mkurugenzi wa Asasi ya Kiraia ya Shinyanga Nguvu kazi Development Foundation (SNDF). Nilipokea vielezo kutoka kwa JOSEPH MACHOKAA ambaye sasa ni marehemu tangu mwezi wa pili ili kuweza kulishughulikia swala lake hilo kwa kushirikiana na wanasheria kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu, tukiwa tunajiandaa swala hilo nilipata taarifa  zisizo rasmi juu ya kupotea kwa marehemu kwa njia ya utatanishi kwamba siku ya tukio alikwenda mahakamani na aliporudi alirudisha baiskeli ya jirani yake salama alipoondoka tu hakuonekana tena hadi tarehe  02/04/2012.

Baada ya  jirani zake kutomuona kwa mda mrefu walianza kumtafuta  na baadaye walibaini kwamba  ameuwawa na mimi nilipewa taarifa kwa njia ya ujumbe wa simu, ndipo na mimi nilichukua hatua kwenda  Polisi makao makuu Dar es Salaam na kuonana  na viongozi wa jeshi hilo na kuwapa taarifa hizo zisizo rasmi  juu ya mauaji hayo na wao wakachukua hatua za kuwasiliana na uongozi wa jeshi hilo mkoa wa Morogoro na mkoa walituma Polisi wa wilaya ya Kilosa kwenda eneo la tukio na walipofika inasemekana Polisi hao walitoa vitisho kwa wananchi, hivyo hawakupata ushirikiano wa kutosha kwa ajili ya ufumbuzi wa tatizo hilo.

Zipo taarifa za kuchukuliwa kwa watoto wa marehemu na watumishi wa Idara ya Uhamiaji na kupelekwa kusikojulikana kwa kutumia gari la serikali, jambo ambalo hadi sasa linawapa hofu wananchi wa kijiji hicho. Hivyo naomba kamati yako ishughulikie pia kujua watoto wa marehemu waliko kwa vile kuna hofu ya watoto hao pia kuwa wameuawa. Aidha majina ya watoto waliopotea ni Peter Joseph(miaka 30), Betson Joseph(28), Asnath Joseph(18), mwanamke mmoja ambaye jina lake lake halikufahamika kwani alifika kutoke nyumbani kwao Kenya baada ya kupata taarifa za kuuawa kinyama kwa marehemu JOSEPH MACHOKAA pamoja na watoto wawili wa mama huyo wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka mitatu na mwingine miezi minne ambao ni raia wa Kenya.

Kufuatia wananchi kutishiwa  kuuwawa mara kwa mara  hawana IMANI na jeshi la Polisi wilayani Kilosa pamoja na watendaji wa ngazi mbali mbali ikiwemo Mahakama kwani wamekuwa wasaliti wao kwa kutotekeleza kero na matatizo yao.


Hivyo kwa niaba ya wananchi hao tunaomba Waziri wa Mambo ya ndani, Waziri wa Katiba na Sheria wafike kijiji cha Msowelo ili kusikiliza matatizo ya wananchi ikiwemo kuwajengea IMANI kwa kuwa kifo chenye utata cha marehemu JOSEPH MACHOKAA pamoja na kupotea kwa watoto wake ambao walikuwa wanamtafuta baba yao ili kujua aliko, kimewashtua sana na sasa hawana  IMANI hata na viongozi wa Serikali, kwa vile matatizo haya wameyafumbia macho muda mrefu na wamekuwa wakishirikiana na waharifu.

Niombe pia vyombo vya dola viweze kuwatia Mbaroni wahusika au watuhumiwa, kwa vile tayari watuhumiwa wapo kwa mujibu wa mashuhuda ambao ni Mh. hakimu mahakama ya mwanzo wakishirikiana na mlalamikaji.

Nitashukuru  kama kamati hii italipatia ufumbuzi tatizo la wananchi wa kijiji cha Msowelo kwa kuwaomba Mawaziri niliowataja hapo juu kufika kijijini hapo mapema.

Pamoja na barua hii, naambatanisha vielelezo mbalimbali pamoja na picha za watoto na mabaki ya mwili wa marehemu pamoja na mazishi yake.

Asante.


Nakala:-
1.    Waziri wa mambo ya ndani.
2.   Waziri wa katiba na sheria.
3.   IGP - Said Mwema.
4.   Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
5.   Mkurugenzi, Kituo cha Sheria na haki za Binadamu Makao Makuu.
6.   Msemaji wa kambi ya Upinzani Bungeni.
 habari na
Antony Sollo Mwanaharakati na mtetezi wa haki za Binadamu: +255787565533   

 
 

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.