Ads Top

BARUA YA KUOMBA TAARIFA TRA HQ


Kaka huyu akiwa na mtoto wake ambaye alikuwa akimtegemea baba yake kwa kila kitu
kwa sasa kijana huyu ajui la kufanya kutokana na halialionayo baad ya kupata ajali na pia hatambui familia yake itaishi vip 
kitamburisho cha mama yake na binti alieinama ambaye ni mremavu wa kuto kuongea 
Rosemary Enzi za uhai wake amecha mtoto mdogo akiwa hana muangalizi ikiwa mama tayali amepoteza maisha kwa ajali
marehemu Rosemary aliyefariki kutokana na ajali
moja wa majeruhi waliogongwa na gari


Kumb namba Sndf/Hq/0040/2012                 16/08/2012

KAMISHINA WA KODI ZA NDANI
S L P 1629
DAR ES SALAAM

YAH : KUOMBA TAARIFA ZA MMILIKI WA GARI  T 864 BMN GARI AMBALO
            LILIACHA NJIA NA KUWAGONGA WATU 16 SIKU YA TAREHE 31/07/2012
            HUKO TINDE MKOANI SHINYANGA .
Kwa heshima napenda kuleta Maombi ya kupatiwa taarifa za mmiliki wa gari tajwa hapo juu ili kuweza kufanya mawasiliano naye kujua ana mpango gani juu ya wananchi 16 waliogongwa na gari lake siku ya tarehe 31/07/2012 huko Tinde Mkoani Shinyanga ambapo kwa taarifa nilizo nazo tangu kutokea kwa ajali hiyo hakuna mtu aliyekwenda kuwaona na kuwapa pole wala kuwapa huduma ya aina yoyote jambo ambalo ni Ukiukwaji wa Haki za Binadamu.

Mpaka sasa wapo watu watatu ambao tayari wamepoteza maisha yao ikiwamo mama aliyeacha mtoto mdogo akiwa hana msaada wowote  na watu wengine 13 wakiwa ni majeruhi kwa kuvunjwa miguu na kwa sasa wako Hospitalini,na wengine majumbani wakiuguza majeraha pasipo na msaada wowote toka jeshi la polisi wala mmiliki wa gari hilo.

Nitashukuru iwapo nitapatiwa taarifa za mmiliki wa gari hilo ili niweze kuwasiliana naye kujua yuko tayari kuwahudumia watu hao au hayuko tayari ili kuangalia utaratibu unaofaa kwa hatua zaidi.

Asante  
BY 
Antony Sollo
Mkurugenzi SNDF

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.