Ads Top

FAINALI YA KOMBE LA POLISI JAMII HATIMAYE LAFIKA TAMATI HUKU TIMU YA CNN KUIBUKA BINGWA

katika viwanja vya michezo hapa Kishapu kulikuwa na mchezo wa Fainali ya kombe la Polisi Jamii mchezo ulioshirikisha timu ishirini toka Jimbo la Kishapu ambapo Timu ya CNN ya Kata ya Songwa imeibuka mbabe kwa kuifunga timu ya UKENYENGE FC kwa magori mawili kwa moja 2/1 na kufanikiwa kulibeba Kombe la Polisi Jamii Jimboni humo ikiwemo zawadi kwa mchezaji bora na Golikipa bora pamoja na Kocha Bora ambapo walioibuka kidedea katika kubeba zawadi hizo ni kama ifuatavyo.
Mchezaji Bora katika mchezo huo alieibuka mshindi ni ALLY mchezaji wa timu ya Ukenyenge FC na kujinyakulia kitita cha Tshs 10,000/= ambapo kwa upande wa Golikipa Bora WAMBURA SORONYO aliibuka mshindi na kujinyakulia zawadi ya Tshs 10,000/= ambapo kwa upande wa Kocha Bora Afande Oscer Shani kutoka kituo cha Polisi Maganzo alifanikiwa kupata zawadi ya Tshs 10,000/= zawadi ambazo zilikabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Ndugu Wilson Elisha
Imeandariwa na ANTONY SOLLO DAWATI la Michezo Kishapu Shinyanga



No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.