SUALA LA AJIRA LAWA KIZUNGUMKUTI
KWA KILE KILICHOZUNGUMZWA KUWA HALI MPYA,NGUVU MPYA NA KASI MPYA CHAJIDHIHIRISHA HIVI KARIBUNI NA BADO KINAENDELEA KUJIDHIHIRISHA
NA; mwandishi wetu Mbwana Ramadhania(anaripoti zaidi)
Kutokana na soko la ajira kuwa gumu na hali hiyo hadi kupelekea watu wa jinsia ya kike yaani wanawake wameonekana wakijihusisha na kazi ya ukonda wa magari ya abiria aina ya dala dala na mengineyo yakiwemo magari aina ya DCM kwa barabara ya magari ambapo hapo awali watu wa jinsia hiyo hawakuonekana wakijihusisha na kazi hiyo
Aidha ;Wanawake wengi hivi sasa wameonekana wakipeana changamoto wao kwa wao kupitia kazi hiyo kwani hivi jana mida ya asubuhi walionekana wasichana wawili wakiwa wanaitia abiria na kupelekea kitendo hicho kuwa changamoto kwa wanawake wenzao ambao walikuwa wakipita pembeni na wengine wakiwa wamelipanda hilo gari
Aidha ;mwanaripota wetu mwengine kwa jina aitwaye Mohamedi A. Nyamka aliweza kuonana ana kwa ana na miongoni mwa makonda hao wa jinsia ya kike sehemu za Mbagala Rangi tatu hivyo maongezi yao yalikuwa kama yafuatayo;
Mohamedi Nyamka (mwandishi);habari za saa hizi dada!
Kondakta(msichana);safi tu kaka
Mohamedi Nyamka (mwandishi) ;Hivi kwanini sasa hivi ninaona wanawake walio wengi wanajihusisha na ukondakta ukitofautisha na hapo awali?
Kondakta(msichana) ; Aaah! Ujue kaka siku hizi hali ya maisha imebadilika na sisi tumeona ni vyema tubadilike kwani wanawake walio wengi wanaona ukondakta na kazi ya wanaume pekee kumbe la hasha hilo si kweli na sisi pia utegemezi uliokithiri kwa wanaume tunaona kuwa wanaume wenyewe wametuchoka na ndio maana tumeona ni vyema tujihusishe na kazi hizi, pia ninapenda kuwasihi wanawake wenzangu kuwa hii ni ari mpya na kasi mpya hivyo basi tujishughulishe tuache utegemezi kwa wanaume zetu kwani kazi ya ukondakta hata sisi tunaweza hususani kama mimi nilipata tabu hapo awali tu na tangia hapo hadi sasa nimezoea ninajionea kawaida tu kwani mwanzo mgumuuu!!!
Aidha ;mwanaripota huyo Mohamedi A. Nyamka hakuishia hapo aliendelea kwa kuwapa ushauri wanawake wengine kuwa wasione ajabu kazi ya ukondakta kwa mwanamke kwani nayo ni ajira kama ajira nyinginezo hivyo alimalizia kwa kusema tunapomuelimisha mwanamke nisawa na kuwa tumeielimisha jamii
No comments: