Ads Top

WAWILI WAJERUHIWA, MMOJA AFARIKI KATIKA VURUGU MJINI MOROGORO LEO

Mwili wa Alli Zolla aliyedaiwa kuuwa na polisi kwa kupigwa risasi kichwani wakati wa vurugu zilizotokea leo asubuhi katika stendi ya mabasi Msamvu ukiwa hospitali ya mkoa wa Morogoro.

Kijana Hashimu Seif aliyepigwa risasi mguuni akiwa hospitali.

Kijana Frank Valimba akionyesha majeraha aliyoyapata tumboni kutokana na vurugu hizo.

KIJANA mmoja aliyejulikana kwa jina la Alli Zolla anadaiwa kuuwa na polisi kwa kupigwa risasi kichwani kwenye vurugu zilizotokea leo wakati wa maandamano ya wanachama wa Chadema ya kuwapokea viongozi wao kwa ajili ya mkutano. Mbali na kifo hicho pia vijana wawili Frank Valimba (19) na Hashimu Seif (22) wamejeruhiwa kwa kupigwa risasi mmoja tumboni na mwingine mguuni.
Akizungumza kwenye mkutano uliofanyika jioni hii katika Viwanya vya Shule ya Msingi, Kiwanja cha Ndege, Mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu aliueleza umati mkubwa wa watu ulihudhuria mkutano huo, kwamba mchakato wa kulishitaki jeshi la polisi la mkoani hapa kuhusiana na mauaji hayo umeshakamilika na kwamba wananchi walioshuhudia mauaji hayo amewaomba kutoa ushirikiano kwenye kesi.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.