Bafana Bafana tayari kuchuana na Angola
Baada ya kutoka sare ya kutofungana bao lolote
katika mechi yao ya ufunguzi, ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika,
wenyeji wa mashindano hayo Afrika Kusini, wanashuka uwanjani kwa mechi
yao ya pili hiyo kesho na Angola.
Baada
ya mechi yao ya kwanza kocha mkuu wa timu ya taifa ya soka ya Afrika
Kusini, Gordon Igesund, aliwashutumu wachezaji wake kwa kukosa umakini.
Igesund, ambaye ni kocha wa tatu kuliongoza
Bafana Bafana, tangu michuano ya kombe la dunia mwaka wa 2010, alikiri
kuwa wachezaji wake walionyesha mchezo mbaya katika mechi hiyo
iliyochezwa katika uwanja wa Soccer City, mjini Johannesburg.
Igesund amesema baada ya mechi hiyo, wachezaji
wake sasa ni sharti wacheze kadri ya uwezo wao na kushinda mechi
zilizosalia ili kufufua matumaini yao ya kufuzu kwa raundi ijayo.
Angola vile vile ilitoka sare ya kutofungana bao lolote la Morocco katika mechi yao ya kwanza.
Mshambulizi wa Angola, ambaye alikuwa akicheza
mechi yake ya kwanza na timu hiyo ya taifa Guilherme Afonso, amesema
sasa ana imani kuwa watashinda mechi hiyo.
Afonso, alionyesha mchezo mzuri katika mechi yao na Morocco na asema walijiufunza mengi kutoka kwa mechi hiyo.
Wakosoaji wengi wanahisi, Angola, ilipoteza
nafasi nyingi za kufunga na wachezaji wake wakiwemo aliyekuwa
mshambulizi wa Manchester United, Manucho, hawakucheza kadri ya uwezo
wao.
Kikosi cha Angola | Kikosi cha Afrika Kusini |
01 Lama 03 Lunguinha 04 Massunguna 13 Bastos 15 Miguel 20 Mingo Bile 06 Dede 16 Pirolito 18 Da Costa 09 Manucho 17 Mateus Wachezaji wa Ziada wa Angola12 Landu22 Neblu 02 Airosa 05 Fabricio 10 Zuela 14 Costa 07 Djalma 08 Dinis 11 Gilberto 21 Manuel 19 Yano 23 Afonso |
16 Khune 05 Ngcongca 11 Matlaba 14 Khumalo 21 Sangweni 08 Tshabalala 12 Letsholonyane 13 Dikgacoi 18 Thuso Phala 07 Majoro 17 Parker Wachezaji wa ziada wa Africa Kusini01 Sandilands22 Meyiwa 02 Gaxa 03 Masilela 04 Nthethe 06 Chabangu 10 Serero 15 Furman 19 Mahlangu 20 Manyisa 09 Mphela 23 Rantie |
No comments: