Kesi ya rufaa ya Taylor kuanza leo
Taylor anasema kuwa hukumu aliyopewa haifai
Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor, anatarajiwa kuanza kukataa rufaa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita huko Hague.
Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor, anatarajiwa kuanza kukataa rufaa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita huko Hague.
Mwezi Mei mwaka jana, mahakama ilimhukumu miaka hamsini gerezani kwa
kusaidia waasi kufanya vitendo vya kukiuka haki za binadamu, katika nchi
jirani ya Sierra Leone wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya
mwaka 1991 na 2002.
Mawakili wa Taylor, waliitaja hukumu hiyo kama hujuma dhidi ya haki na kuomba hukumu yenyewe kutupiliwa mbali.
Wakati huohuo,Taylor mwenye umri wa miaka 64, amewaomba wabunge kumlipa malipo yake ya uzeeni ambayo ni dola
25,000.
25,000.
Alilaani vikali, hatua ya wabunge kutomlipa
malipo yake akisema ni ukiukwaji mkubwa wa haki yake. Taylor alinukuliwa
kwenye barua hiyo akisema kuwa anapaswa kuruhusiwa huduma za
kidiplomasia akiwa gerezani akiongeza kuwa amenyimwa haki hiyo.
Taylor ndiye alikuwa rais wa kwanza wa zamani
Afrika kuhukumiwa kifungo gerezani, kwa uhalifu wa kivita tangu kesi za
wahusika wa utawala wa NAZI baada ya vita vya pili vya dunia.
Wakati wote kesi ya Taylor ilipokuwa inasikilizwa, alisisitiza kutokuwa na hatia.
'Ukatili mkubwa'
Mahakama ya Hague iliundwa mwaka 2002 kuwahukumu
wale waliohusika pakubwa na vita vya Sierra Leone ambapo takriban watu
50,000 waliuawa.
Ilimpata na hatia Taylor, kwa makosa 11 ya
uhalifu wa kivita, yakiwemo mauaji na ubakaji na kutajwa kama mojawapo
ya uhalifu wa kinyama kuwahi kufaywa duniani.
Ili aweze kupewa almasi zilizotokana na vita,
Taylor aliwapa waasi, msaada wa silaha na usafiri pamoja na kuwapa moyo
kuendelea kupigana hali iliyochochea vita na mateso dhidi ya watu.
Mawakili wake wanasema kuwa wanakata rufaa kwa
misingi 42 wakiteta kuwa uchunguzi wa jopo lililosikiliza kesi yake
haukuweza kuthibitishwa.
Viongozi wa mashtaka hata hivyo wanatarajiwa
kusema kuwa mahakama ilifanya makosa kwa kumhukumu Taylor peke yake na
kukosa kuchukulia hatua waasi alioshirikiana nao. bofya haba kwa habari zaidi....>>>>
No comments: