Kundi D leo linakamilisha mzunguko wa pili kwa timu 16 zinazowania taji la ubingwa wa Kombe la Afrika barani Afrika kwa mwaka 2013.
Kipindi cha pili kimeanza, Ivory Coast ingali ikiongoza kwa goli 1, huku Tunisia ikiwa haijapata kitu.
Bao la Ivory Coast lilifungwa kunako dakika ya 19 na mshambuliaji wake Gervinho.
Ivory Coast sasa ina alama sita katika kundi hilo baada ya kushinda mechi yao ya kwanza dhidi ya Togo.
Tunisia ina kikosi imara kitakachopigana kuwaangusha miamba hao wa soka barani Afrika.
Tunisia imekuwa ikishiriki mara kwa mara katika fainali za Kombe la Afrika, Lakini wamefanikiwa mara moja tu kutwaa kombe hilo ilipoandaa michuano hiyo mwaka 2004.
Wamekuwa katika fainali hizo tangu mwaka1994, ikiwa ni nchi pekee ya Afrika kufanya hivyo, lakini huenda walitarajia kupata mafanikio zaidi kutokana na wachezaji iliokuwa nao wakati wote huo.
Kocha wa Tunisia Sami Trabelsi ni kipenzi cha mashabiki nchini Tunisia akiwa mchezaji maarufu wa sehemu ya ulinzi katika timu ya taifa, akishiriki katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka1996 na 2000, pamoja na zile za mwaka 1998 nchini Ufaransa.
Ivory Coast inajivunia nyota wake kadhaa wanaosakata kabumbu ndani na nje ya nchi hiyo.
Miongoni mwao ni Didier Drogba anayechezea nchini Uchina, Yahya Toure, mchezaji bora wa soka barani Afrika mwaka 2013 na pia tegemeo la timu ya Manchester City ya England, Wengine pamoja na timu wanazochezea kwenye mabano:
No comments: