Ads Top

Mabaharia watano wa India waliotekwa nyara mwezi uliopita nje ya mwambao wa Nigeria wameachiliwa huru, kwa mujibu wa kampuni yao

Jeshi la Nigeria likipiga doria katika Niger Delta
Mabaharia hao wa meli ya mafuta walitekwa wakati watu waliojihami na silaha tele walipoingia kwa nguvu ndani ya meli yao, SP Brussels, katika eneo la mafuta la Niger Delta kusini mwa Nigeria.
Taarifa ya kampuni ya meli hiyo, Medallion Marine, ilieleza kuwa mabaharia hao ni wazima lakini haikueleza iwapo ililipa kikombozi.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.