Rais Jakaya Kikwete Ampokea Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais wa Benin,Dkt. Boni Yayi
Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akimkaribisha
mgeni wake Mheshimiwa Dkt.Boni Yayi wakati alipowasili katika uwanja wa ndege
wa Kimataifa wa Mwalimu julius Nyerere usiku wa Jana Usiku
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Dkt.Boni Yayi wakifurahia jambo
katika hoteli ya Kilimanjaro Jana usiku.
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais wa Benin,
Mheshimiwa Dkt. Boni Yayi amewasili nchini usiku wa jana, Jumanne, Januari 15,
2013, kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania.
Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es
Salaam, Rais Boni Yayi amepokelewa na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mara ndege yake ilipotua
kiasi cha saa tano unusu usiku.Leo asubuhi, viongozi hao wawili watafanya
mazungumzo rasmi kabla ya Rais Boni Yayi kuondoka nchini kuendelea na ziara
yake Barani Afrika.
Tanzanian Shilling Converter
No comments: