Afrika Kusini imebanduliwa nje ya mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika
Baada ya kulazwa magoli matatu kwa
moja kupitia mikwaju ya
Penalti na Mali.
Penalti na Mali.
Timu
hizo mbili zilitoshana nguvu ya kufungana bao moja kwa moja katika
dakika tisini za kawaida na hata baada ya dakika zaidi thelathini
kuongezwa hakuna aliyefanikiwa kuona lango la mwenziye na hivyo mechi
hiyo kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti.
Kinyume na matarajio ya wengi, wenyeji wa fainali hizo Afrika Kusini ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupiga mikwaju yake na kufanikiwa kupata mkwaju wa kwanza pekee.
Mali ilijibu kwa kufunga mikwaju mitatu na katika mkwaju wa kuamua ikiwa wataendelea, mkwaju uliopigwa na mchezaji wa Afrika kusini ulipaa juu ya goli na hivyo kuwapa Mali ushindi bila kupiga mkwaju zaidi.
Mali na Ghana tayari zimefuzu kwa nusu fainali ya mashindano hayo.
Washindi wengine wawili kuamuliwa katika mechi baina ya Nigeria na Ivory Coast na Togo na Burkina Faso siku ya Jumapili.
Goli la Afrika Kusini limefungwa katika dakika ya 31 na Tokelo Rantie.
Afrika Kusini ilifuzu kucheza robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ikiwa mshindi wa kwanza kutoka kundi A, huku Mali wakitokea kundi B wakiwa washindi wa pili.

No comments: