Ads Top

CHEKI JINSI SHEIKH PONDA ALIVYOFIKISHWA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU JIJINI DAR ES SALAAM CHINI YA ULINZI MKALI WA JESHI LA POLISI NA ASKARI MAGEREZA

 Msafara ukianza kutoka Mahakama ya Kisutu
  Ulinzi ulikuwa ni wa Uhakika
Kikosi maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani (KMKM) nacho kilikuwepo
 Ulinzi Ukiwa umekamilika nje ya mahakama
 Picha juu na chini Mfuasi wa Ponda akidhibitiwa na askari
 Mfuasi wa Sheikh Ponda Issa Ponda akijitetea mbele ya Askari wa Kutuliza Ghasia (FFU) baada ya kutolewa amri ya kuondoka  katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakati kesi inayomkabili Sheikh huyo ilipoanza kusikilizwa leo.
Wakiwapokea na kuwapongeza wenzao wanao tuhumiwa pamoja na Ponda
 Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Waislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda (katikati) akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakati kesi inayomkali ya uchochezi na wizi wa malighafi zenye thamani ya Sh.milioni 59 inayomkabili Katibu huyo na wenzake 49 ilipoanza kusikilizwa leo.
  Sheikh Ponda Issa Ponda akiwa katika basi la Magereza tayari kwa kurejeshwa Mahabusu.
  Wafuasi wa Sheikh Ponda Issa Pondawakilifuatilia gari lililombeba kiongozi wao wakati akitoka Mahakama ya Kisutu.
 Kundi la Wafuasi likiwa limejikusanya karibu na Jengo la Sophia House huku Polisi wakiwa kando yao.
 Wafuasi waliokuwa nje wakiimba wakati gari likitoka
 Wengine zaidi wakitoka Mahakama ya Kisutu.Picha na Mroki Mroki na Dende JR

Kesi ya Uchochezi na Uharibifu wa mali inayo mkabili Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake leo imeendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam huku Polisi wakiwa katika doria kali ya kuimarisha ulinzi katika viunga jirani na Mahakama hiyo ambayo imejizolea umaarufu mkubwa jijini Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla kwa jinsi inavyo endesha kesi na watu wa aina mbalimbali kufikishwa katika mahakma hiyo kabla ya baade kesi zao kuhamia Mahakama Kuu kwa hatua zaidi za kisheria.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.