Chelsea na Arsenal ni ushidi tu
Frank Lampard kwa mara nyingine
tena amedhihirisha kuwa bado angali mmoja wa wachezaji wa kutegemewa wa
Chelsea pale alipoiongoza timu yake kuilaza Wigan kwa magoli manne kwa
mmoja, na kumaliza ukame wa Chelsea wa kutoshinda katika mechi nne
mfululizo.
Ushindi huo sasa umemuondolea kocha wa Chelsea Rafael Benitez mzigo aliokuwa nao.Lampard alifunga bao la tatu la Chelsea na kwa sasa anakaribia rekodi iliyowekwa na Boody Tambling ambaye aliifungia Chelsea jumla ya magoli 202.
Ramireza aliifungia Chelsea bao lake la kwanza kabla ya Edin Hazard kufunga bao la pili.
Kufikia wakati wa mapunziko Chelsea ilikuwa kifua mbele kwa magoli mawili kwa yai.
Katika kipindi cha pili Shaun Maloney alifufua matumaini ya Wigan kwa kuifungia bao hilo.
Lakini juhudi zao zilionekana kugongwa mwamba pale Lampard alipoongeza la tatu kisha Marko Marin kuongeza la nne.
Ushindi huo sasa umeisukumu Chelsea hadi nafasi ya tatu mbele ya Tottenham.
Katika mechi nyingine Santi Cazorla alifunga bao kunako dakika ya hamsini na kuisadia Arsenal kujizolea alama tatu muhimu dhidi ya Sunderland.
Arsenal iliyokuwa ikicheza na wachezaji kumi pekee sasa inashikilia nafasi ya tano kwenye msururu wa ligi kuu.
Carzola alivurumisha kombora kali iliyowapita walinda lango wa Sunderland pamoja na mlinda lango wao, baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Theo Walcott.
Carl Jenkinson alipewa kadi nyekundu baada ya kumfanyia mchezaji wa Sunderland madhambi.
Sunderland hata hivyo haikutumia fursa hiyo kufunga, licha ya mashambulizo makali katika lango la Arsenal.
No comments: