Ads Top

Rais Jakaya Kikwete Asaini Kitabu Cha Maombolezo na Kutoa Heshima za Mwisho Kwa mwili wa Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini Kati la Kanisa la Kiinjili cha Kilutheri Tanzania (KKKT)

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini Katika Kanisa la Kiinjili cha Kilutheri Tanzania (KKKT)Jana, Alhamisi, kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Arusha.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia ya Askofu Thomas Laizer wa Dayosisi ya Kaskazini Kati nyumbani kwa Askofu mara baada ya kuwa ametoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Arusha jana, Alhamisi, Februari 14, 2013. Picha zote na Freddy Maro-IKULU

Rais Jakaya Kikwete na viongozi wengine mbalimbali kesho wanatarajiwa kuwaongoza maelfu ya waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa  Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati Askofu Dk Thomas Olmorjor Laizer (69).

Askofu Laizer  aliyefariki dunia katika hospitali ya Seliani Mjini Arusha Februari 7, mwaka huu anatarajiwa kuzikwa katika viwanjavya Kanisa Kuu la KKKT Arusha Mjini.
Rais Kikwete na viongozi wengine wa Kitaifa akiwemo Rais Mwinyi, Rais Mkapa na waliowahi kuwa Mawaziri Wakuu Sumaye na Lowassa ambao Viongozi  tayari wameshawasili mkoani Arusha kwa ajili ya shughuli hiyo.


Mazishi hayo  pia yanatarajiwa kuhudhuriwa na  na Maskofu  wa Kanisa la KKKT kutoka Dayosisi zaidi ya 20, Askofu kutoka Jumuiya ya CCT  pamoja na Maskofu kutoka Kanisa Katoliki.


Viongozi  wa madhehebu ya KKKT kutoka nchini Marekani  na Ujerumani pamoja na Vyuo mbalimbali alivyowaji kusoma Marehemu Askofu   Dakta Thomas Ole Laizer  nao tayari wamewasili Mkoani Arusha  kuhudhuria
mazishi ya Kiongozi huyo. 


Ibada ya mazishi  itakongozwa  na Mkuu wa Kanisa la KKKT  Askofu Dk Alex Malasusa

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.