Ads Top

Ujumbe wa Rais Barack Obama kwa Wakenya


Rais wa Marekani Barack Obama amewaomba wakenya ambako babake alizaliwa kujiepusha na ghasia pamoja na vitisho katika uchaguzi mkuu unaokuja.
Alituma ujumbe wake kupitia mtandao wa You tube na kuanza ujumbe wake kwa kiswahili.
Alisema uchaguzi ulikuwa fursa nzuri kwa wakenya kuungana kuonyesha kuwa wao sio watu wa makabila bali taifa linaloweza kujivunia.
Uchaguzi mkuu wa Kenya uliokumbwa na utata mwaka 2007 ulisababisha ghasia na vurugu ambapo watu zaidi ya 1,000 waliuawa
Wakenya watapiga kura tarehe 4 mwezi Machi, kumchagua rais na waakilishi wengine, katika uchaguzi mkuu wa kwanza tangu ule uliokumbwa na ghasia kwa habari zaidi bofya hapa..>>>

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.