Chenga: Miaka 34 ya kuishi na nyoka
Bagamoyo. Ni mnyama hatari, mwenye sumu kali, anaogopwa, anaua, anaweza hata kukuachia ulemavu.
Hata hivyo Nobert Joseph Chenga, ameweza kucheza na kuishi na nyoka kwa miaka 34 sasa.
Siku hii, namkuta Chenga, maeneo ya Bagamoyo, akiwa katika moja ya kazi zake za kusaka na kufuga nyoka.
Alikuwa mchovu kwa sababu ya shughuli nzito ya kukamata nyoka kutoka mapori ya Miono, wilayani Bagamoyo.
Nilishuhudia nyoka wa aina mbalimbali wenye sumu wakiletwa katika mifuko maalumu.
Chenga mwenyewe ameshika fimbo maalumu ya kuwasogeza au kukamata nyoka.
Wanapofika, Chenga anafungua mkoba kwa ustadi
kisha kuwaweka katika chumba, akitumia fimbo hiyo kuwasogeza mahali
panapohitajika kukaa.
Wakati mwingine anawashika, kwa mikono lakini kwa
namna ambayo nyoka hao hawawezi kuuma. Anawapanga katika vyumba
alivyovipa majina kwa mfano; Black Mamba, Boom Slag. Green Mamba, Cobra,
Msanga na African Venom.
Nyoka mmoja mweusi, niliyeambiwa anaitwa Black
Mamba, akiwa na urefu wa zaidi ya futi tano, anaponyoka mikononi mwa
Chenga, tukio lililonifanya nitimue mbio. Si mimi tu niliyetimua mbio,
bali hata wasaidizi wa Chenga waliokuwa eneo hilo walikimbia. Hii ni
kutokana na Chenga kuthibitisha kuwa nyoka huyo akikuuma, huchukui
dakika tano, kabla ya kubadili jina na kuitwa marehemu.
Ananionyesha alama kadhaa za kuumwa na nyoka,
mikononi na miguuni mwake. Lakini bado anaishi nao, anawafuga na
anaendelea kuwakamata ili wawe wengi zaidi.
Mapenzi na nyoka yalianza 1979
Chenga alianza kupenda nyoka mwaka 1979. Mapenzi
hayo kwa nyoka, hayakuja hivihivi, bali yalimwingia baada ya kupewa
zawadi ya chatu mwenye kilo 60, akiwa mkoani Mwanza.
kwa habari zaidi bofya hapa..>>>>
kwa habari zaidi bofya hapa..>>>>

Tanzanian Shilling Converter
No comments: