Ads Top

Mtoto wako yuko salama? Wanafunzi wabainika kuvuta bangi, kuendesha danguro kwa siri

 
  Dar es Salaam. Una hakika mwanao anapokuaga nyumbani kweli anakwenda shule? Ni swali ambalo wazazi na walezi wanapaswa kufuatilia ili kupata uhakika.
Imebainika kuwa wazazi na walezi wengi wanadanganywa, wapo watoto ambao wanawahi kuamka nyumbani wakisema wanakwenda shule, kumbe wanakwenda kufanya ngono au mambo mengine yasiyo ya maana, kabla ya kwenda shule.
Aidha kwa wale ambao wanaishi bwenini, baadhi yao matendo wanayofanya yanatia ‘kichefuchefu’ hata kusikia. Swali la msingi kwa wazazi kulipatia jibu ni je, mwanao yuko salama?
Haijalishi kama shule ya msingi au sekondari au hata chuo, ni suala la msingi kwa mzazi kufuatilia na kupata jibu, hasa kutokana na baadhi ya tafiti kubainisha kuwa baadhi yao wamekuwa wakifanya mambo ya yenye kutia aibu wanapokuwa mbali na walezi au wazazi wao.
Baadhi ya watoto ni waongo kupindukia kwa wazazi wao, huku wengine wakijifanya kuwasikiliza wazazi na walezi, tofauti na ukweli wa matendo yao wanayoyafanya baada ya kuachana nao.
Mfano halisi wa matendo ya wanafunzi
Kumekuwa na ongezeko kubwa la utoro kwa wanafunzi Shule ya Sekondari ya Kata Majani ya Chai iliyopo eneo la Kipawa, Jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi mbalimbali wakiwemo wa kidato cha nne na baadhi ya wale wanaosomea sanaa wanadaiwa kuongoza kwa matendo ya kuvuta bangi na kufanya ngono wakitumia baadhi ya nyumba zilizopo jirani na eneo hilo la shule.

Akiongea katika hali ya kuonyesha kukata tamaa na kukerwa, Mkuu wa Shule hiyo, Jansinta Assey anasema “Hili tatizo limekithiri sana kwa wanafunzi wa kike na wa kiume, tulijaribu kuwabana kuwauliza wanaenda kufanya nini walitujibu wanaenda kuvuta bangi na baadhi ya wasichana walidai wanawafuata wavulana kwa ajili ya kufanya nao ngono”.
Muhimu kwa wazazi
Hapo ndipo linapokuja swali kwa wazazi wenye watoto…je unayajua anayofanya mwanao baada ya kuachana nae? Je, unafanya nini kuhakikisha kizazi chako kinakuwa salama katika hali kama hii ambayo watoto wengine wanaibika kwenda kuvuta bangi na kufanya ngono badala ya kwenda kusoma kama wanavyoaga wanavyotoka nyumbani?
Hali katika shule
Mwalimu Jansinta anasema vitendo vya uvutaji bangi na biashara ya ukahaba kwa wanafunzi wake vinachangiwa na ushirikiano haba anaoupata kutoka kwa baadhi ya vyombo vya ulinzi na usalama katika eneo hilo.

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.