Papa akutana na waandishi wa habari
Papa Francis aliyechaguliwa hivi karibuni, amekutana
na waandishi wa habari mjini Rome akisema kuwa atapenda kanisa maskini
lenye lengo la kuwasaidia maskini.
Katika hatua ambayo Vatikani imesema
inaonesha uwazi zaidi, Papa mpya alizungumza na mamia ya waandishi wa
habari na alisema alichagua jina la Mtakatifu Francis wa Assisi kwa
sababu alikuwa mtakatifu wa amani, matumizi haba na kutumikia maskini
"Wakati wa uchaguzi wa papa mpya kando yangu alikuwa Askofu wa Sao Paulo, Claudio Hummes.

Tanzanian Shilling Converter
No comments: