Ujumbe wa Rais Kibaki kwa Wakenya
Rais wa Kenya Mwai Kibaki
anayehudumu muhula wake wa wisho , amewataka wakenya kuhakikisha kuwa
uchaguzi unafanyika kwa njia huru na ya haki watakapokwenda kwenye debe
Jumatatu.
Amesema kuwa wakenya watakuwa wanaandika historia ya nchi kwa kushiriki katika uchaguzi siku hiyo. .
Akihutubia taifa kwa kupitia kwa
televisheni ya taifa, Kibaki pia alisema kuwa serikali imehakikisha kuwa
imedhibiti usalama kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kwa amani.
Aidha amewataka wagombea kukubali matokeo ikiwa watashindwa wakati akiwataka washindi kuwa wanyeyekevu katika kupokea ushindi.
Kibaki aliapishwa kwa muhula wa pili tarehe 30
mwezi Disemba mwaka 2007 baada ya uchaguzi uliokumbwa na utata mkubwa
kiasi cha kusababisha maafa huku maelfu wakiachwa bila makao hadi leo kwa habari zaidi bofya hapa..>>>>
No comments: