Wanajeshi 13 wa SA wauawa CAR
Wanajeshi wa Afrika Kusini
Wanajeshi 13 wa Afrka
Kusini waliuawa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wakati waasi
walipouteka mji mkuu, Bangui, Jumapili. Haya yalitangazwa na Rais Jacob
Zuma.
Bwana Zuma alisema Afrika Kusini "inajivunia" wanajeshi wake waliopambana na "waasi".
Bwana Zuma alisema wanajeshi wengine 27 walijeruhiwa, na mmoja hajulikani alipo.
"Ni kipindi cha huzuni kwetu sisi… Twajivunia
wanajeshi wetu 200 waliopambana na waasi," aliuambia mkutano wa
waandishihabari katika mjii mkuu, Pretoria

Tanzanian Shilling Converter
No comments: