Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa wamesema “hawatakubali wala kuvumilia” hujuma dhidi ya chama chao
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe
akizungumza kwenye kongamano la chama hicho lililofanyika jana jijini
Dar es Salaam. Picha na Fidelis Felix.
Dar es Salaam. Viongozi hao kwa
nyakati tofauti jana walisema hujuma hizo zimekuwa zikifanywa na Chama
Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Serikali ambayo imekuwa ikitumia vyombo
vya dola na kwamba sasa wanapanga ugaidi wa kuwateka maofisa wa ngazi ya
juu wa Chadema.
Suala la ugaidi liliibuka kwa nguvu katika wiki ya
kwanza ya Bunge la Bajeti na sasa limehamia nje ya chombo hicho cha
kutunga sheria kutokana na Chadema kuwatuhumu CCM na Serikali yake
kwamba wanapanga njama za kuwateka maofisa wakuu wa chama hicho.
Jana Dk Slaa alipokuwa akimkaribisha Mbowe
kufungua Mkutano wa Mafunzo na Mipango ya Vuguvugu la Mabadiliko ‘M4C’
na Kongamano la Katiba Mpya kwa Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, alisema
taarifa walizonazo zinaonyesha kuwa CCM ndiyo wanaofanya vitendo vya
kigaidi wakishirikiana na Serikali.
“Tuna taarifa zote zinazoonyesha kwamba CCM ndiyo
magaidi wakishirikiana na Serikali yake, lakini sisi tuko makini kuliko
hata Serikali ya CCM na tuko makini kuliko hata Usalama wa Taifa na
umakini huu ndiyo utakaotupeleka Ikulu mwaka 2015,”alisema Dk Slaa.
Hata hivyo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,
Nape Nnauye alipotafutwa kujibu tuhuma hizo alisema hakuna jipya ambalo
Chadema wamelisema.
“Kuna jipya katika hilo, ni yale yale ya kawaida
na jana (juzi) Mwingulu alizungumza vizuri sana bungeni. Hiyo ni sawa na
mchawi anapomwangia mtu na kufa anakuwa wa kwanza kwenda kulia msibani,
nchi siku yoyotete haijengwi kwa ngonjera za maneno bali inajengwa kwa
mipango,”alisema Nape.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani,
Pereira Ame Silima alipotakiwa kutoa msimamo wa Serikali juu ya tuhuma
hizo alisema, “Mimi siwezi kuzungumza ila mtafute Waziri (Dk Emmanuel
Nchimbi),”alisema Silima.
Alipotafutwa Dk Nchimbi kupitia simu yake ya mkononi, ilikuwa ikiita bila kupokewa.
Alipotafutwa Dk Nchimbi kupitia simu yake ya mkononi, ilikuwa ikiita bila kupokewa.
Kauli ya Mbowe
Kwa upande wake Mbowe alisema, CCM imekuwa ikitumia mbinu mbalimbali kuhakikisha inakisambaratisha chama hicho bila mafanikio.
Kwa upande wake Mbowe alisema, CCM imekuwa ikitumia mbinu mbalimbali kuhakikisha inakisambaratisha chama hicho bila mafanikio.
“Watu wa Usalama wa Taifa wakishirikiana na CCM
wamekuwa wakifanya mipango ya kutaka kuwateka maofisa wetu. Hawa watu ni
wepesi sana na msiwaogope hata kidogo,”alisema Mbowe huku akishangiliwa
na wanachama na makada waliofurika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Blue
Pearl.
Mbowe alisema: “Ukiona chama chochote tawala
kinatumia jeshi la polisi kutengeneza ushahidi wowote wa kihalifu hiyo
ni dalili ya hatari kwa mustakabali wa usalama wa nchi.”
Mbowe alisema mbinu za sasa za CCM zinatokana na kushindwa kukivuruga chama hicho kwa propaganda kuwa ni chama cha familia, ukabila, ukanda na baadaye udini.
Mbowe alisema mbinu za sasa za CCM zinatokana na kushindwa kukivuruga chama hicho kwa propaganda kuwa ni chama cha familia, ukabila, ukanda na baadaye udini.
Katiba na Elimu
Kuhusu mchakato wa Katiba Mpya, Mbowe alisema ikiwa itafika Aprili 30 mwaka huu bila hatua zozote kuchukuliwa, watamwamuru mjumbe wa tume hiyo kutoka Chadema, Profesa Mwesiga Baregu kujiondoa.
Kuhusu mchakato wa Katiba Mpya, Mbowe alisema ikiwa itafika Aprili 30 mwaka huu bila hatua zozote kuchukuliwa, watamwamuru mjumbe wa tume hiyo kutoka Chadema, Profesa Mwesiga Baregu kujiondoa.
Chadema kinataka Serikali iwasilishe bungeni, muswada wa Sheria
ya Marekebisho ya Katiba ili yafanywe marekebisho mbalimbali kuhusu
uwakilishi katika Bunge Maalumu la Katiba.
“Serikali inaona hili kama mchezo, sasa acha wakae kimya na baada ya Aprili 30 mwaka huu watachagua kusuka au kunyoa,”alisema Mbowe.
“Serikali inaona hili kama mchezo, sasa acha wakae kimya na baada ya Aprili 30 mwaka huu watachagua kusuka au kunyoa,”alisema Mbowe.
Kuhusu elimu, Mbowe alieleza kushangazwa na kile
alichosema kuwa ni Serikali kutofahamu sababu za wanafunzi kufanya
vibaya katika mitihani yao.
“Serikali eti haijui na kama haijui basi Waziri
Mkuu (Mizengo Pinda) hatakiwi kuwa hapo alipo, kwani haiwezekani watoto
wanafeli halafu anaunda tume,”alisema Mbowe na kuongeza:
“Mwaka 2011 waliunda tume ambayo ilitoa mapendekezo 27 lakini ripoti hiyo ilifichwa hadi mimi juzi (Jumatano) nilipoisoma bungeni wabunge wa CCM wakabaki vichwa chini.”
Alisema kuundwa kwa tume nyingine ambayo itatumia fedha za walipakodi ni kuwaumiza Watanzania ilhali tatizo na chanzo kinajulikana.

Ugaidi bungeni
Juzi wakati wa mjadala wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, wabunge wa CCM na Chadema kwa nyakati tofauti walituhumiana kwa ugaidi kiasi cha kusababisha vurugu na kutoelewana miongoni mwao.
Juzi wakati wa mjadala wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, wabunge wa CCM na Chadema kwa nyakati tofauti walituhumiana kwa ugaidi kiasi cha kusababisha vurugu na kutoelewana miongoni mwao.
Alhamisi akisoma maoni ya Kambi ya Upinzani, Mbowe
alisema ugaidi ni ubunifu wa polisi na Serikali kwa ajili ya
kuwabambikia kesi zisizo na dhamana kwenye mahakama maofisa wa vyama vya
upinzani.
Kutokana na hotuba hiyo, Mbunge wa Iramba
Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba aliishambulia hotuba ya Mbowe akieleza
kuwa wanahusika kupanga kumdhuru mwandishi wa habari.

Tanzanian Shilling Converter
No comments: