Nancy Sumari: Aelezea siri kuu ya mafanikio yake
Alipovikwa taji la umalkia wa Tanzania, wengi hawakutazamia mabadiliko yeyote katika mashindano ya ulimwengu.
Lakini yeye aliweza…akaleta nyumbani kwa mara ya kwanza, taji la Miss World Afrika.
Ni Nancy Sumari ambaye anasema, siri kuu ya mafanikio yake, ni kuthubutu na kujituma. Sumari anasema amefanikiwa katika mambo mengi kutokana na kujiamini katika kila jambo alilolifanya sambamba na kujituma.

“Utamaduni wangu ni kujiamini katika kila jambo
ninalolifanya na hiyo ndiyo siri ya mafanikio yangu. Ndiyo maana
niliweza kushinda mataji ya Miss Dar Indian Ocean, Miss Kinondoni, Miss
Tanzania na hatimaye Miss World Africa,” anasema Nancy.
Nancy hakuanza na maisha ya mafanikio kwa usiku mmoja-bali aliwahi kupitia changamoto na kazi mbalimbali kabla ya kuwa mrembo mwenye hadhi ya kimataifa.
Nancy hakuanza na maisha ya mafanikio kwa usiku mmoja-bali aliwahi kupitia changamoto na kazi mbalimbali kabla ya kuwa mrembo mwenye hadhi ya kimataifa.
Aliwahi kuuza duka la samani za nyumbani na kulipwa mshahara wa Sh 120,000 kwa mwezi.
Kwa jitihada, zake na uthubutu kama asemavyo, hivi sasa Nancy ni mhitimu mtarajiwa wa taaluma ya biashara katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Kwa jitihada, zake na uthubutu kama asemavyo, hivi sasa Nancy ni mhitimu mtarajiwa wa taaluma ya biashara katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Si hivyo tu bali ni Mkurugenzi wa Matukio wa Kampuni ya Frontline Management ambayo inahusika na masuala ya mahusiano ya umma.
Vilevile Nancy ni mwandishi wa vitabu na pia
anahusika katika kuhakikisha mtandao wa Bongo 5.com unafanikiwa
akishirikiana na mumewe.
Licha ya kazi za kiofisi Nancy pia ni mmoja wa
mabalozi wa One Billion Living muunganiko wa wanawake duniani wanaopinga
ukatili na kuelimisha wanawake.
Moja ya kazi zake za uandishi ni kitabu cha nyota
yako ambacho Nancy anasema maudhui yake yametokana na uhaba wa hadithi
za watoto zilizoandikwa na watanzania. “Mbali ya kuwa mimi ni mama kwa
wakati huu, kila nilipokwenda kwenye maduka ya vitabu, nilikosa vitabu
vya watoto vilivyoandikwa na waandishi wa Tanzania. Vingi vimeandikwa na
waandishi wa nje,”alisema.
Anasema aliamua kuandika kitabu, ambacho watoto wa
kike wa Tanzania wataweza kukisoma na kuvutiwa kufanya kile
kilichoandikwa katika kitabu hicho.
“Nyota yako ni kitabu kinachoelezea nafasi ya
mwanamke katika jamii. Kitabu hicho kinaonyesha namna gani wanawake
wenye mafanikio walivyoweza kuyapata ili kutoa mwanga kwa watoto wa
kike kusoma kwa bidii na kuzifikia ndoto zao,” anasema Nancy.
Nancy anasema hata wanawake wa majumbani wanapaswa kukisoma kitabu
hicho ambacho kwa sasa kipo katika maduka ya vitabu mbalimbali.
Mpangilio wa ratiba na maisha binafsi
Nancy anasema akiwa kama mwanamke mwenye familia anapangilia mambo yake ipasavyo ili kuhakikisha anatimiza majukumu yake yote kwa pande zote zinazomhusu.“Mwanamke amepewa kitu cha ziada, anaweza kutekeleza majukumu yote bila kusitasita. Kwa upande wangu namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kwani natekeleza majukumu yangu yote licha ya kwamba nina mambo mengi ninayoyafanya” anasema

Mama huyo wa mtoto mmoja aitwaye Zuri anasema
anaweza kumlea mtoto wake, baba wa mtoto, na majukumu mengine ikiwamo
masomo na kazi mbalimbali anazozifanya.
Anasema mara nyingi kazi hizo zimekuwa zikimchosha na anaporudi nyumbani anakutana na familia ambayo inamuhitaji
Anasema mara nyingi kazi hizo zimekuwa zikimchosha na anaporudi nyumbani anakutana na familia ambayo inamuhitaji
“Nashukuru Mungu familia yangu inanielewa hasa mtoto japokuwa ni
vigumu kwake huwa najitahidi kuwa karibu naye ili asijione mpweke”
anasema
Changamoto
Maisha hayakosi changamoto, nancy anaeleza vikwazo anavyokutana navyo katika maisha kuwa ni dharau kutoka kwa wadau.
Maisha hayakosi changamoto, nancy anaeleza vikwazo anavyokutana navyo katika maisha kuwa ni dharau kutoka kwa wadau.
Anasema anaposhughulikia masuala ya kiofisi wengi
wamekuwa wakimchukulia kama mtu asiye makini katika jambo analotaka
kulifanya.
“Unajua nakumbana na vitu vingi sana, kuna wakati
naingia katika ofisi fulani kushughulikia masuala yangu ya kikazi,
matokeo yake watu wananichukulia sivyo na kudhani kwamba sijadhamiria na
siwezi kufanya jambo hilo,” anasema

Tanzanian Shilling Converter
No comments: