Kinachodaiwa kumuua Msanii Mangwea hiki hapa
Dar es Salaam. Wakati mazishi ya mwanamuziki marehemu Albert
Mangwea(28) maarufu kama `Ngwair’ yakitarajiwa kufanyika mjini Morogoro,
maeneo ya Kihonda baada ya mwili kuwasili nchini, hospitali
iliyomfanyia vipimo imethibitisha kuwa pombe na dawa za kulevya kupita
kiasi ndivyo vilivyomuua.
Mwili wa mwanamuziki huyo, ambaye alitamba kwenye
miaka ya 2000 na wimbo wa `Mikasi’, unatazamiwa kuletwa kesho nchini na
kuagwa Jumamosi kabla ya kusafirishwa kwenda kwao Kihonda, Morogoro kwa
mazishi.
Kwa mujibu wa taarifa Mangwea alifariki dunia juzi
kwenye Hospitali ya St Hellen, iliyopo Johannesburg, Afrika Kusini
alikokuwa amekwenda kwa shughuli za muziki.
Kifo chake
Ripoti iliyochapwa na mitandao mbalimbali ya ndani
na nje ya nchi inasema marehemu alifikwa na umauti baada ya kulewa
kupindukia, kibaya zaidi alikuwa hajala.
Siku ya kifo chake, Mangwea alianguka nyumbani kwa rafiki zake akiwa katika hali hiyo ya kulewa sana.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, baada ya kufikishwa
hospitalini, Mangwea aligundulika kulewa mara tano ya kipimo cha kilevi
kilichopitishwa na serikali ya Afrika ya Kusini, ambacho ni 416mg za
pombe kwenye kila milimita 100(kwa mlevi anayeendesha chombo cha moto).
Pia marehemu alikutwa na upungufu wa hewa ya oksijeni kwenye seli na tishu za mwili wake.
Ripoti hiyo ilibainisha kuwa Mangwea, maarufu
Ngwair, alikuwa na tatizo la kutokula chakula vizuri kabla ya kifo chake
na pia kukosa muda wa kupumzika.
Sampuli zilizopatikana mwilini mwake zinaonyesha
mkusanyiko wa dawa za kulevya mbalimbali zikiwemo heroine, cocaine chafu
na bangi ya gramu 0.08 ambavyo vilikutwa kwenye damu yake.
Kifo chake kilitokana na mshtuko wa moyo na
kushindwa kupumua, hali iliyosababisha mapigo ya moyo wake kusimama kwa
sekunde chache, na kusababisha kifo chake.
Mwili wa Ngwair ulionekana kana kwamba alitokwa na
damu nyingi puani baada ya kuonyeshwa kwa Watanzania wengi jana jioni
Johannesburg, Afrika Kusini.
Taarifa za awali zilizotolewa na rafiki wa karibu aliyepo nchini
Afrika Kusini, aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Jonathan zilidai
kuwa marehemu hakuamka tangu alipopumzika usiku wa kuamkia juzi.
M2 The P naye mahututi
Rafiki wa Ngwair aliyekuwa naye siku ya tukio,
ambaye pia ni msanii, Mgaza Pembe maarufu kwa jina la `M2 To The P’ naye
alifikishwa katika Hospitali ya St Hellen baada ya kukutwa amepoteza
fahamu akiwa na Ngwair. Msanii huyo, ambaye makazi yake yako Kibaha
mkoani Pwani, aliwahi kutamba na wimbo wa ‘M2 To the P’ na ule wa hivi
karibuni wa `Nyumbani’.
Historia ya Ngwair
Ngwair alizaliwa Novemba 16, 1982 jijini Mbeya, ni
mtoto wa mwisho kuzaliwa kwa baba akiwa mtoto wa 10 na kwa mama akiwa
mtoto wa sita. Ngwair asili yake ni Ruvuma kabila la Wangoni. Akiwa na
miaka mitano walihamia Morogoro akasoma Shule ya Msingi Bungo alipofika
darasa la tano, baba yake akapata uhamisho kwenda Dodoma. Baadaye
alisoma Shule ya Sekondari ya Mazengo kabla ya kujiunga na Chuo cha
Ufundi Mazengo.
Aliondoka lini?
Ngwair aliondoka nchini mwaka huu mwezi Machi,
tarehe 26 kwa mwaliko wa kisanii ambapo tangu kipindi hicho, amekuwa
akifanya onyesho moja kila mwezi na mara ya mwisho, onyesho lake
lilikuwa wiki mbili zilizopita.
P Funk: Ngwair Ana nyimbo 50 ambazo hazijatoka!
Paul Mathyesse, a.k.a P Funk ambaye ni
mtayarishaji aliyefanya idadi kubwa ya muziki wa Ngwair, ameiambia
Mwananchi kuwa hadi sasa haelewi nini kimetokea lakini anachofahamu kuwa
Albert Mangwea ni zaidi ya msanii kwake na ni kati ya wasanii aliofanya
nao kazi nyingi.
Alisema kila ambacho amekuwa akimfundisha na
kumwelekeza ndicho alichokifanya kwa kuwa alikuwa na uwezo wa kuimba
aina zote za muziki Hip Hop, Free style na ragga.
“Nilikuwa na Ngwair kwa zaidi ya miaka 13,
ninamfahamu vizuri na ninaujua uwezo wake, alikuwa ni zaidi ya rafiki
yaani sina neno zuri la kusema kumhusu zaidi ya kumtakia safari
njema,”alisema.
P- Funk pia ni Mkurugenzi wa Bongo Records ambayo marehemu alikuwa akifanyia kazi zake hadi anafikwa na umauti.
P –Funk anafafanua kuwa hata albamu zote mbili za
Ngwair yeye ndio amefanya ukiachilia mbali nyimbo ambazo alikuwa
akifanya moja, moja ambazo hadi sasa wanazo nyimbo 50 ambazo
hawajazitumia.
Anasema alikutana na Ngwair mwaka 2000 ambapo
alikwenda studio na rafiki yake ambaye hamkumbuki jina ilipofika wakati
wa kuimba ndio alipokigundua kipaji chake na kumsainisha mkataba na
wimbo wao kwanza ulikuwa ni ‘Gheto langu’.
Anaendelea kusema kuwa hata kumtambulisha kwa
mashabiki mikoani kwa mara ya kwanza walifanya wao ambapo aliunganishwa
kwenye ziara ya ‘wimbo wa nini cH chanzo’ wa Juma Nature,mwaka 2001.
Maneno ya mwisho aliyoandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Ilikuwa ni Mei 26 Ngwair aliweka ujumbe huu kwenye
ukurasa wake wa Twitter,”Namuhitaji Mungu kwa kila dakika kila saa,”
akitumia lugha ya Kiingereza.
Maneno ya mwisho kuzungumza na mama yake
Ilikuwa ni wiki mbili zilizopita Ngwair
aliwasiliana na mama yake na kumtaka aendelee kumwombea au waombeane na
kumwahidi angerudi Ijumaa iliyopita na hakuwasiliana naye tena hadi
anafikwa na umauti.
Baadhi ya watu aliowahi kufanya nao kazi wazungumzia kifo chake
Mchezaji Adam Nditi aliandika kupitia ukurasa wake wa Twitter R.I.P Albert Ngwair You will be missed by many Tanzanians.
Adam Nditi
Mtangazaji wa Clouds Loveness aliandika kwenye
ukurasa wake kuwa “Yani siamini Ngwair amefariki dunia nini ilichomkuta
#RIP # Ngwair r #akaCowobama
Jamani Ngwair , am in tears now ….. Jamani!. I can’t believe this. I can’t tweet The RIP….
Whyyyyy?
Mr II a.k.a Sugu
R.I.P ALBERT MANGWEA a.k.a NGWAIR...U R GONE TOO SOON MY NIGGA...
Lady Jay Dee
Ngwair ndio aliniandikia verse ya Rap, kwenye wimbo wa Jaffarai. Unaoitwa “Sio Kweli”
ASALAAM ALAYKUM, TANZANIA. IT’S JIDE ONCE AGAIN HEAR ME LOUD N CLEAR.........na maneno mengine yote yalioendelea.
I Wish i could turn back the hands of time.
Profesa Jay
PUMZIKA KWA AMANI KAMANDA Wangu Wanadamu
tulikupenda sana ila MOLA amekupenda zaidi, Jina lake LIHIMIDIWE..
Tutakukumbuka daima #COWIIZZ”.
Diamond
DAH! bado nashindwa kuamini nnachokiskia na kukiona kwenye Media.
Wasanii na watu mbalimbali wamekuwa wakiandika kwenye kurasa za kijamii kuhusiana na kifo hicho cha ghafla cha msanii huyo.
No comments: