Operesheni ya kijeshi imeanza dhidi ya Boko Haram ingawa wadadisi wanasema imekuja kuchelewa
Amri ya kutotoka nje usiku imetangazwa katika jimbo la Adamawa nchini Nigeria.
Jimbo hilo limeungana na mengine mawili ya
kaskazini mashariki ya, Borno na Yobe, ambako serikali inasema kuwa
wanajeshi wameanza oparesheni kubwa dhidi ya wapiganaji wa kiislamu wa
kundi la Boko Haram .
Rununu hazikuwa zifanya kazi katika baadhi ya sehemu za eneo hilo.
Maafisa wa serikali wameiambia BBC kuwa ndege za kivita huenda zikapelekwa katika oparesheni.
Walisema kuwa wanajeshi walishambulia sehemu za jimbo la Borno, ambako kundi la Boko Haram lina ngome zake.
Operesheni hiyo inakuja baada ya serikali
kutangaza hali ya hatari katika majimbo ya Borno, Yobe na Adamawa
Kaskazini Mashariki mwa nchi ambako watu 2,000 yatari wameuawa tangu
mwaka 2009.
Amri ya kutotoka nje kuanzia saa za jioni hadi asubuhi imetangazwa katika jimbo la Adamawa ili kukabiliana na wanamgambo hao.
Mwandishi wa BBC katika jimbo la Adamawa anasema
kuwa uamuzi huo unashangaza kwani hali ya usalama katika jimbo hilo sio
mbaya ikilinganishwa na majimbo ya Borno na Yobe.
Mnamo siku ya Alhamisi wanajeshi walivamia kambi
za wanamgambo katika mbuga ya wanyama na ambayo inasifika kuwa moja ya
ngome kuu za kundi la Boko Haram
Msemaji wa jeshi la Nigeria Brigedia Generali
Chris Olukolade, alisema kuwa watatumia uwezo wao wote wa kijeshi
kukabiliana vilivyo na wapiganaji wa Boko Haram.
Kwa habari zaidi bofya hapa...>>>>>>>
Kwa habari zaidi bofya hapa...>>>>>>>
No comments: