TAIFA STARS YAAHIDI KUFANYA KWELI KATIKA MCHEZO WAO DHIDI YA MOROCCO
Kocha wa Timu ya Taifa, Kim Poulsen na Nahodha Juma Kaseja
wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika hoteli ya Pullman ilikoyo
Marrakech, Morocco. Stars inashuka Jumamosikupambana na timu ya taifa ya Morocco katika
mchezo wa kufuvu kucheza fainali za kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.Na
Mpiga Picha wetu
MARRKECH Morocco
Huku
Timu ya Taifa Taifa Stars ikikabiliwa na mechi muhimu kesho (Jumamosi)
dhidi ya Morocco kusaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia,
Kocha Kim Poulsen amesema amejiandaa kucheza mpira wa kasi na wenye pasi
za uhakika ili kuivuruga beki ya Morocco.
Kocha
huyo ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari na kusisitiza
kuwa ni muhimu kuhakikisha Morocco hawaupati mpira kwa urahisi.
“Wachezaji
wako katika hali nzuri kabisa na wana ari ya kushinda mechi hii…tuna
nguvu na tunajua namna ya kuwapiga Morocco,” alisema kocha huyo.
Alisema
suala si mchezaji gani anaanza au washambulizi ni wangapi, bali ni kazi
itakayofanyika uwanjani na ubora wa wachezaji wa Taifa Stars,
inayofurahia udhamnini mnono wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Alisema
Morocco ni timu kubwa na ina wachezaji wengi wa kulipwa lakini
inafungika na Taifa Stars itaweka nguvu kuanzia mwanzo wa mechi.
“Unapocheza
mechi kama hii inabidi uweke nguvu dakika za kwanza za mechi ili umpe
mpinzani wakati mgumu kwa hivyo dakika za mwanzo zitakuwa muhimu sana
katika mechi hii,” alisema.
Poulsena
alisema baadhi ya watu nchini Morocco bado wanaamini kuwa ushindi wa
mechi ya awali Jijini Dar es Salaam wa 3-1 dhidi ya Morocco ulikuwa wa
kibahati tu. “Tunataka kuwadhihirishia kuwa tunaweza na Taifa Stars sio
timu ndogo kama wanayodhani.”
Alisema mazingira ya kambi ni mazuri kabisa na wachezaji wote wako katika hali nzuri na tayari kwa mchezo huu.
“Katika
hali ya kawaida ungetegemea hujuma nyingi ikiwemo hoteli mbovu, viwanja
vibovu vya mazoezi na kadhalika lakini hapa ni tofauti kabisa…kwani
mazingira ni mazuri,” alisema Poulsen.Taifa Stars imeweka kambi katika Hoteli ya Pullman iliyoko nje kidogo ya Mji wa Marrakech.
Naye
nahodha wa Taifa Stars, Juma Kaseja alisema wamefanya mazoezi ya
kutosha hasa ikizingatiwa kambi ilianzia Addis Ababa, Ethiopia ambako
walicheza mechi ya kirafiki na Sudan na kutoa sare ya 0-0 kabla ya
kuelekea Marrakech.
“Morocco ni timu kubwa, tunapaswa kuiheshimu lakini sio kuiogopa…tutapambana ili timu ipate matokeo,” alisema Kaseja.
Naye
Meneja wa Bia ya Kilimanajro Premium Lager, George Kavishe, akizungumza
kutoka Dar es Salaam alisema wao kama wadhamini wa Taifa Stars wana
imani kubwa sana na Stars na wanaitaka iwape Watanzania raha kwa mara
nyingine kwa kushinda mechi hiyo.
“Tumewaona wakifanya vizuri nyumbani kwa kushinda mechi tano mfululizo na sasa ni muda wa kupata ushindi nje,” alisema.Stars
iko katika kundi C pamoja na Ivory Coast, Morocco na Gambia. Kundi hilo
linaongozwa na Ivory Coast yenye pointi 7, Tanzania 6, Morocco 2 na
Gambia 1.
Mechi ya kesho itapigwa katika Uwanja wa Marrakech saa tatu usiku kwa saa za Morocco ambayo itakuwa saa tano kamili Tanzania.
Baada
ya Morocco Stars itacheza na Ivory Coast nyumbani Jumapili ijayo na
mechi ya mwisho itakuwa dhidi ya Gambia Septemba mwaka huu
No comments: