Wachimba migodi 37 wameuawa baada ya mvua kubwa kusababisha kuporomoka kwa machimbo walimokuwa katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati
CAR ina rasilimali nyingi ya madini
Maafisa wanasema kuwa ajali hiyo ilitokea
Jumapili karibu na mji wa Ndassima, umbali wa kilomita 440 Mashariki mwa
mji mkuu,Bangui.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, siku tatu za kuomboleza zimetangazwa nchini humo.
Jamuhuri ya Afrika ya Kati, ina utajiri wa
dhahabu na almasi lakini imekumbwa na mzozo wa muda mrefu, baada ya
waasi kupindua serikali mwezi Machi.
Msemaji wa rais Prosper Ndouba, alisema kuwa anahofia kuwa watu zaidi huenda wakafariki.
"kufikia sasa idadi ya waliofariki ni 37, ingawa kuna wengi zaidi waliojeruhiwa, '' alisema bwana Ndouba
Afisaa mmoja ambaye hakutajwa jina aliambia
shirika la habari la AFP kuwa idadi kubwa ya wachimbaji walikuwa kwenye
machimbo hayo yaliyogeuka na kuwa tope baada ya mvua kubwa kunyesha na
hivyo kuwaporomokea.
Kwa habari zaidi bofya hapa..>>>>>>
Kwa habari zaidi bofya hapa..>>>>>>
No comments: