Biashara ya dawa za kulevya inaonekana kushamiri nchini, huku kukiwa na maswali mengi juu ya akina nani hasa wahusika wa shughuli hii, hata inashindwa kukomeshwa
Agnes anayeshikiliwa kwa tuhuma za kukutwa na kilo 150 za dawa za
kulevya Afrika Kusini
Baadhi ya wananchi waliozungumza na mwandishi wa
makala hii, wana mashaka kwamba huenda baadhi ya vigogo au wafanyakazi
waliopewa mamlaka kupambana na dawa nchini, wanahusika kufanya biashara
hii au kuwasaidia wanaoifanya kwa manufaa yao, madai ambayo wamekuwa
wakiyakanusha vikali.
Hata hivyo baadhi ya watu ambao wamewahi kuwa
majambazi na kujihusisha na biashara haramu, akiwamo mchungaji mmoja
kutoka Arusha ambaye amewahi kuwa jambazi kabla ya kuamua kuokoka na
kumtumikia Mungu, anasema ni vigumu mno na huenda ni jambo
lisilowezekana kufanikiwa kufanya mambo mabaya nchini kama ya ujambazi
au dawa za kulevya na ukadumu katika kazi hiyo kama hauna mtandao na
wale ambao wanahusika katika kuzuia vitendo hivyo.
“Kama una mawasiliano na wenye mamlaka utafanya
biashara yoyote chafu, kama huna ni ngumu kutokamatwa, mimi nimewahi
kuwa jambazi, ninaongea haya kwa uzoefu, sio kweli kwamba ulinzi nchini
ni mbaya, bali kuna watumishi si waaminifu” anasema Mchungaji huyo.
Kwa uzoefu wake ni kuwa iko haja kwa viongozi
walioko Serikalini kama kweli wana lengo la kupambana na dawa za
kulevya, kwanza kuwachukulia hatua wote ambao waliwakagua na kuwaruhusu
wahusika wa dawa wanaokamatwa kupita.
Ni kama hakuna lengo la kupambana na dawa za kulevya
“Kama mtu amepita uwanja wa ndege, inapaswa kujulikana alikaguliwa na nani? Wote waliohusika wakamatwe mara moja, waunganishwe kwenye kesi ya hizo dawa za kulevya, hii itaonyesha kweli Tanzania tuna lengo la kupambana na dawa za kulevya, lakini kinachofanyika sasa ni usanii wa mchana kweupe,” anasema Mchungaji huyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini.
Hatua kali kwa wauza dawa
Baadhi ya wananchi akiwamo Ameria Haule, mkazi wa Ubungo anashauri kutungwe sheria kali za kupambana na dawa za kulevya.
Aidha, Juma Hamisi wa Mtongaji, na Tuma Msongwa wa
Manzese, Dar es Salaam wanasema pale ambapo mtu amekamatwa na aina
yoyote ile ya dawa za kulevya, na kukawa na uthibitisho, kusiwe na haja
ya kufanya upelelezi juu yake zaidi, badala yake hukumu itolewe mara
moja. Hali kadhalika wakashauri dhamana iondolewe, wakisemabiashara hii
ni sawa na mauaji.
Kituo cha daladala kwa Manyanya
Mojawapo ya vituo vya daladala ambavyo vinadaiwa kutumiwa kwa dawa za kulevya ni cha daladala cha Kinondoni kwa Manyanya, kama unaelekea Posta ukitokea Kinondoni.
Ubungo darajani
Katika maeneo ya Ubungo kuna watu kadhaa wanahusika na dawa hizi; Kwa mfano yuko jamaa ambaye huzunguka usiku akisambaza dawa za kulevya kwa gari lake dogo. Hali ni mbaya zaidi eneo la Ubungo Maziwa, wapo hadi akina mama kadhaa kwenye vijiwe vya vijana wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Maeneo mengine ya Tanzania
Karibu nchi nzima, kuna kashfa hii ya kuwapo kwa dawa za kulevya, huku maswali makuu yakielekezwa kwa wana usalama nchini kama ni kweli hawaoni yanayoendelea.
Iundwe tume ya siri
Baadhi ya wananchi wanashauri kuundwe kikosi cha siri kuchunguza utendaji wa askari ili kutoa mashaka ambayo yanaonekana kuongezeka miongoni kwa jamii kuwa baadhi yao huenda wanashiriki katika biashara hii ya dawa mbalimbali za kulevya yakiwemo cocaine, mirungi na bangi.
Ahadi nyingi vitendo haba
Licha ya kuwapo madai mengi miezi ya hivi karibuni ikiwemo kwamba kuna viongozi wa dini wanahusika na dawa za kulevya, wapo wabunge waliosema wanawajua wenye kufanya biashara hiyo, baadhi ya viongozi wakielezwa kuhusika.
Mbunge aja na yake
Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), amewahi kuahidi kuwa ataanika majina ya vigogo wanaofanya biashara hiyo haramu.
Tume dhaifu iwajibishwe
Hata hivyo, Lugola alisema Kamishina wa Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya, Christopher Shekiondo, anapaswa kuwajibishwa kwani ameshindwa kazi, kwani kuna wakati aliwahi kunukuliwa akisema anawajua wanaohusika na dawa hizo nchini, lakini kuna ugumu wa namna ya kuwakamata.
Orodha ya viongozi wa dini wanaohusika na dawa za kulevya
Wakati fulani mwaka juzi kulielezwa kuwa kuna orodha ya viongozi wa dini ambao wanahusika na biashara ya dawa za kulevya.
Maaskofu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania
waongea
Katika taarifa yao kujibu hilo la Rais Kikwete, Maaskofu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), walimpa Rais Kikwete saa 48 za kuwataja kwa majina viongozi wote wa Dini anaowatuhumu kuhusuka na biashara haramu ya dawa za kulenya “unga”.
Agnes na Melisa wakamatwa na kilo 150 Afrika Kusini
Tukio la hivi karibuni kabisa ni la wanawake wawili toka Tanzania, waliokamatwa Uwanja wa Ndege wa OR Tambo, Afrika Kusini wakitokea Tanzania Julai 6, mwaka huu wakidaiwa kuwa na dawa za kulevya takribani kilo 150.
WASANII NA DAWA ZA KULEVYA
Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ anasema baadhi ya wasanii na watu maarufu wamekuwa wakitumiwa kubeba dawa za kulevya kwa vile wanasafiri mara nyingi na huwa wanaonekana kutotiliwa shaka. Kwamba hata yeye kabla ya Ubunge aliwahi kuombwa afanye kazi hiyo alikataa.
Binti Kiziwi
Sisitizo la Nzowa
Akizungumzia kuhusu waliohusika kupitisha kilo 150
za dawa za kulevya kumsaidia Masogange uwanja wa ndege, Nzowa anaamini
wote watakamatwa.
Kwa mujibu wa ripoti ya ofisi ya Waziri mkuu, Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya, tatizo la dawa za
No comments: