Maelfu ya wafuasi wa Mohammed Morsi wameandamana usiku kucha na kisha kukita kambi kando ya msikiti wakitaka Morsi aachiliwe
Waandamanaji wamekita kambi kutaka Morsi aachiliwe
Hata hivyo hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na jeshi licha ya onyo
kutoka kwa waziri wa maswala ya ndani nchini humo Mohammed Ibrahim,
kwamba mamlaka itajibu vitisho vyovyote dhidi ya usalama kutoka kwa
waandamanaji hao.
Zaidi ya wafuasi 70 wanaotaka Morsi
kurejeshwa madarakani waliuawa baada ya ghasia kuzuka kati ya
waandamanaji na vikosi vya jeshi hapo Jumamosi.
Waziri wa mambo ya nje nchini humo amezitaka
pande zote kwenye mgogoro huu kujizuia na kusababisha ghasia, siku moja
baada ya ghasia nchini humo kusababisha vifo vya watu 70.
Kwenye mahojiano na BBC,Nabil Fahmy alisema kuwa pande zote zinapaswa kujizuia na kuchochea ghasia kwa kutumia vurugu.
Mnamo siku ya Jumamosi, wafusai wa aliyekuwa
rais Morsi, walikabiliana na polisi pamoja na maafisa wengine wa usalama
huku maelfu ya waandamanaji hao wakiendelea kupiga kambi.
Wakati huohuo, rais wa muda Adly Mansour amemuamuru waziri wake mkuu kulikabidhi jeshi mamlaka kuwakamata raia.
Mwandishi wa BBC Jim Muir ambaye yuko mjini
Cairo anasema kuwa baadhi ya watu wanaiona hii kama dalili ya wasiwasi
na mwanzo wa serikali kuanza kupambana na waandamanaji waliokita kambi
katika msikiti wa Rabaa al-Adawiya .
Waziri wa mambo ya ndani, Mohamed Ibrahim
amekuwa akionya mara kwa mara kuwa waandamanaji hao watatawanyishwa
karibuni , ingawa waandamanaji wenyewe wanasema hawatabanduka.
Kulikuwa na ghasia siku ya Jumapili, huku watu wawili wakiuawa mjini Cairo.
Mwishoni mwa wiki wapiganaji kumi wa kiisilamu
waliuawa na jeshi katika Rasi ya Sinai ambako wamezidisha mapigano kwa
mujibu wa shirika la habari la serikali la Mena
No comments: