Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, John Tendwa Juu ya vyama vya siasa kutii agizo la kutoanzisha kambi za mafunzo ya kulinda amani maarufu kwa jina la mgambo
Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, John Tendwa
OFISI ya
Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini John Tendwa, imevitaka vyama vya
siasa kutii agizo la kutoanzisha kambi za mafunzo ya kulinda amani
maarufu kwa jina la mgambo , huku ikisisitiza kwamba itachukua hatua za
kisheria kwa chama chochote kitakachokiuka , ikiwemo kukifuta.
Aidha
ofisi hiyo imesema kuwa Katiba ya nchi imempa jukumu kila mwananchi
kulinda amani na usalama wa nchi,pia kujilinda yeye mwenyewe na mali
zake kwa kutoa taarifa katika vyombo vya dola pale anaposikia au kuona
mtu anataka kufanya au anafanya uhalifu au amemdhuru mtu.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dares Salaam na ofisi hiyo katika taarifa
yake iliyoitoa kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na Rajab Juma kwa
niaba ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini,John Tendwa kufutia Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kutangaza hivi karibuni
kinakusudia kuanzisha kambi za mafunzo ya kujilinda kwa
vijana wake nchi nzima.
Alisema
suala hilo lilitangazwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na
kuandikwa katika vyombo vya habari kabla ya chama hicho, kuwasiliana na
taasisi husika ikiwemo ofisi hiyo ili kupata ushauri kuwa jambo
wanalotaka kufanya ni sahihi .
“Hivyo
Katiba ya nchi na katiba za za vyama vya siasa ,hazina maana kila
mwananchi au kikundi fulani wafanye mafunzo ya kijeshi au ukakamavu ili
kufanikisha jukumu hili.
“Jukumu
la vikundi kama hivi ni kutoa taarifa kwa vyombo vya dola na si
kupambana na wahalifu au watu wanaotaka kuwadhuru wenye jukumu la
kupambana na wahalifu ni vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo vipo
kisheria, mojawapo ikiwa ni Jeshi la Polisi,” alisema Juma.
Juma
alikitaka chama hicho na vyama vingine vinavyofikiria au kufanya
jambo hilo kuacha mara moja kwani kufanya hivyo ni kukiuka Sheria
za Nchi ikiwemo Sheria ya Vyama Vya Siasa ya mwaka 1992 kifungu cha
9(2)(C) cha sheria hiyo kinakataza chama cha siasa kuruhusu kutumika,
kushabikia au kutumia nguvu ili kufanikisha malengo yake ya kisiasa.
Alisema
chama cha siasa kutoa mafunzo ya kutumia nguvu kwa wanachama wake, ili
kutekeleza jambo lolote lile ikiwamo kujilinda ni mojawapo ya masuala
yanayokatazwa na Sheria ya Vyama vya Siasa.
Aliongeza
kuwa kifungu cha (20) cha Sheria ya Vyama Vya Siasa kinasema uamuzi wa
Msajili ni wa mwisho na hauwezi kukatiwa rufaa mahakamani.
Akizungumzia
kuhusu madai kuwa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wana kambi za mafunzo ya
kupambana na vijana wake kama kisingizio cha kuvunja
sheria hiyo alisema hayana msingi.
“
Kama CCM wanakiuka sheria ni jukumu la CHADEMA, kila Chama na kila
Mtanzania ,kuto taarifa na ikiwezekana na ushahidi katika taasisi
husika, ikiwemo Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa ili suala hili
lishughulikiwe kisheria,” alisisitiza.
Msajili huyo
aliviasa vyama vya siasa kutumia muda wao kufanya shughuli za siasa ili
kuchangia maendeleo ya nchi, badala ya kutumia uwezo wao na muda wa
kubuni mambo yanayoleta mtafaruku na kuhatarisha mani na utulivu wa nchi
yetu.
“Amani ikitoweka
vyama vya siasa vitakuwa katika makaratasi tu.Kutakuwa hakuna mikutano
wa kamati kuu, hakuna ‘press conference’ yaani mikutano na waandishi wa
habari, hakuna operesheni ya kuzunguka nchi nziman.k. Demokrasia
hutekelezwa na kukua mahali penye amani na utulivu,” alisema.

Tanzanian Shilling Converter
No comments: