Ads Top

Wafuasi wa rais wa Misri aliyeondolewa madarakani na jeshi,Mohammed Morsi wameendelea kupiga kambi katika msikiti wa Rabaa al-Adawiya mashariki mwa mji mkuu wa Cairo

Wafuasi wa rais Morsi

Ikiwa ni siku moja tu baada ya ghasia kali kuzuka.
Waandamanaji hao wameweka vizuizi katika kambi yao na kuapa kutoondoka licha ya mapambano kati yao na vikosi vya ulinzi na usalama.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesitikitishwa na ghasia zinazoendelea nchini Misri.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari,bwana Kerry amesema kuwa wakati huu ni muhimu sana kwa taifa hilo na akatoa wito kwa serikali hiyo kuheshimu haki ya raia kuandamana kwa amani na uhuru wa kujieleza.
Mwandishi wa BBC anasema hali sasa imetulia kiasi licha ya vurugu kutokea katika viunga vingine vya mji wa Cairo

No comments:

UHURUTZ. Theme images by hanoded. Powered by Blogger.