Ziara ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda wilayani Mbinga akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiweka jiwe la Msingi la ujenzi wa mtambo wa
kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa Kampuni ya Andoya Hydroelectric
Company katika kijiji cha Lifakara wilayani Mbinga akiwa katika ziara
ya mkoa wa Ruvuma Julai 21, 2013. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni
hiyo, Menas Andoya
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akizindua mradi wa kupeleka umeme Mbambabay
katika wilaya mpya ya Nyasa kutoka kwenye kituo cha kuzalisha umeme
cha Mbinga akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 21, 2013. Kulia ni
Mkewe Tunu na Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Thabiti Mwambungu.
Watatu Kulia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiendesha pikipiki wakati alipozindua Mradi wa
Pikipiki wa Kikundi cha SACCOS ya vijana wa Mbinga kwenye uwanja wa CCM
mjini Mbinga akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma Julai 21, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akiwapongeza baadhi ya waendesha pikipiki wa Mbinga baada ya kuzindua
mradi wa pikipiki za kikundi cha SACCOS ya vijana wa Mbinga kwenye
uwanja wa Mpira wa CCM mjini Mbinga akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma
Julai 21, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe
Tunu wakizungumza na Mzee Andrea Mapunda (84) wakati alipotembelea
shamaba la kahawa la mzee huyo katika kijiji cha Masumuni wilayani
Mbinga wakiwa katika ziar ya mkoa wa Ruvuma Julai 21, 2013.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akihutubia mkutano wa hadhara
No comments: